Elections 2010 FFU wakimbiza wafuasi wa chadema iringa , slaa akwama kuhutubia

PayGod

JF-Expert Member
Mar 4, 2008
1,259
57
FFU WAKIMBIZA WAFUASI WA CHADEMA IRINGA ,DK SLAA AKWAMA KUHUTUBIA




"
Hapa tupo gado akitua tu Dk Slaa tunaye"
"
Ila hawa wananchi mbona ni wengi sana itakuwaje hawawezi kufanya fujo"
"
Jamaa hakuna kulala hadi kieleweke twendeni uwanja mwingine kama huu hapa wamezuia"
"
Mzee salama hapa ama ?kwani kuna nini ni vita ?"
"
Hapa tupo kamili kwa lolote "kama wanazungumza

Askari wa kikosi cha kutuliza ghasia (FFU) mkoa wa Iringa wakiwa wamejipanga kwa lolote katika viwanja vya uwanja wa shule ya msingi Mlandege mjini Iringa ambako ulipangwa mkutano wa mwisho wa mgombea urais wa Chadema Dk Willibrod Slaa ambaye hata hivyo hakuweza kutua katika uwanja huo kama njia ya kukepa mbinu za CCM kutaka kuvuruga mkutano wake huo iwapo angetua katika uwanja huo leo asubuhi
Wanafunzi wa shule ya msingi Mlandege mjini Iringa wakiwa wamejifungia ndani ya vyumba vyao vya madarasa kuhofu usalama wao baada ya polisi wa FFU kutanda kuzunguka majengo ya shule hiyo ambayo yapo jirani na uwanja wa mkutano uliokuwa ukifanywa na mgombea ubunge wa Chadema jimbo la Iringa mjini Mchungaji Peter Msigwa baada ya mgombea urais Dk Willibrod Slaa kushindwa kutua kuhofu fujo kati yake ya polisi hao ambao walikuwa wakipinga mkutano huo kuhutubiwa na mgombea urais
Polisi wa FFU wakilinda eneo la mkutano ambao lilipaswa kuhutubiwa na mgombea urais wa Chadema Dk Slaa ambaye hata hivyo ameshindwa kuhutubia katika viwanja hivyo vya Mlandege
Wanafunzi wa shule ya msingi Mlandege wakichungulia madirishani baada ya walimu wao kukimbia madarasani kuhofu mabomu muda mfupi baada ya FFU kutua eneo hilo na kuwataka wananchi kutawanyika kabla ya viongozi wa Chadema kujitoa mhanga na kuangua kilio cha kuomba msahama mbele ya askari hao
Hapa uwanja wa Mwembetogwa Iringa ambako ilipaswa Dk Slaa kufanya mkutano wake wa kampeni leo asubuhi japo imeshindikana
Askari wa FFU mjini Iringa wakiwa wamepiga kambi katika uwanja wa Mwembetogwa kuzuia mgombea urais wa Chadema Dk Slaa kufanya mkutano eneo hilo ,kulia ni mwananchi akijikaza kupita kiume eneo hilo ambalo wananchi walitawanywa .




Na Francis Godwin,Iringa


NGOMA nzito Iringa mgombea wa urais kupitia Chama cha Demokrasi na Maendeleo (Chadema), Dk Wilbroad Slaa amegonga mwamba kutaka kufanya mkutano wa kampeni bila kibali katika viwanja viwili tofauti mjini Iringa, baada ya Polisi wa kutuliza ghasia (FFU) kutanda katika viwanja vyote kuzuia mikutano hiyo kwa madai kwamba haina baraka za Tume ya Taifa ya Uchaguzi.



Polisi waliokuwa na silaha kali na mabomu ya kutoa machozi, walifanikiwa kuwatawanya maelfu ya wafuasi wa chama hicho waliokuwa wakiendelea kukusanyika kwa wingi katika uwanja wa Mwembtogwa mjini hapa kuanzia saa mbili na nusu asubuhi.

Baada ya kutawanywa, wananchi hao walielekea katika uwanja wa Shule ya Msingi Mlandege walikotangaziwa kwamba Dk Slaa angetumia jukwaa la mgombea udiwani wa kata ya Kwakilosa, kuwasalimia wananchi wa jimbo la Iringa Mjini kabla hajaendelea na ziara yake ya mikutano ya kampeni katika majimbo ya Njombe Kaskazini, Njombe Magharibi na Songea Mjini.
 
Duh!!! Hawa polisi ni Chadema nini? Wanavyozidi kumpa umaarufu!!! Kura zote kwa Dr wa ukweli!!!!!!!!!!!!!!!!
 
JANA 28/10/2010, PIA FFU WALIWATAWANYA WANANCHI, NA HIVI NDIVYO ILIKUWA JANA




FFU WATAWANYA MAELFU YA WANANCHI WALIOKUWA WAKIMSUBIRI DK SLAA IRINGA MJINI


FFU wakipita mitaani eneo la uwanja wa Mwembetogwa kuwatawanya wananchi waliokuwa wakimsubiri DK SLAA leo
Hapa wananchi wakitawanyika baada ya FFU kuwataka kutawanyika katika uwanja huo
Mgombea ubunge wa Chadema jimbo la Iringa mjini Mchungaji Peter Msigwa akiwaomba radhi wananchi kwa kuchelewa kufika Dk Slaa leo


ASKARI wa kikosi cha kutuliza ghasia (FFU) leo wamelazimika kuwatawanya maelfu ya wakazi wa jimbo la Iringa mjini ambao walikuwa wakiendelea kumsubiri mgombea urais kupitia chama cha Demokrasia na maendeleo (chadema ) Dk Willibrod Slaa katika uwanja wa Mwembetogwa.

Huku wananchi wa eneo la Kihesa wakilazimika kumzua mgombea huyo wa nafasi ya Urais Dk Slaa wakimlazimisha kuhutubia majira ya saa 1.20 usiku wakati akitokea uwanja wa Ndege Nduli.

Wananchi hao ambao walifika katika uwanja huo wa mikutano yapata majira ya saa 6 mchana waliendelea kumsubiri mgombea huyo wa nafasi ya Urais huku wakiimba nyimbo za kumkaribisha Ikulu jambo lililopelekea askari wa FFU ambao walikuwepo kwa wingi katika mkutano huo kwa ajili ya kuulinda mkutano huo kulazimika kutumia vipaza sauti kuwatawanya wananchi hao ambao waliendelea kusubiri hadi majira ya saa 1 usiku wakiamini kuwa mgombea huyo angefika kuwahutubia.

Kabla ya wananchi hao kutawanywa na FFU mgombea ubunge wa jimbo la Iringa mjini Mchungaji Peter Msigwa pamoja na mjumbe wa kamati kuu ya Chadema Taifa Chiku Abwao walipata kuwaomba radhi wananchi hao kuwa mgombea huyo ambaye alikuwa akitokea Dodoma amechelewa kufika kutokana na matatizo yaliyo nje ya uwezo wake .

Askari hao wakiwa katika magari zaidi ya matatu huku wakiwa wameshehena mabomu ya machuzi katika nguo zao waliwataka wananchi hao kuondoka katika eneo hilo kabla ya kutumia nguvu zaidi katika kuwatawanya huku baadhi ya magari yakizunguka katika mitaa mbali mbali wakipiga king'ora kuashiria hali ya hatari .

Hata hivyo kwa mujibu wa mjumbe wa kamati kuu ya Chadema Taifa Chiku Abwao mgombea urais huyo wa Chadema atafanya mkutano wake huo wa kampeni kesho majira ya asubuhi katika viwanja hivyo na kuwaomba radhi wananchi ambao walijitokeza kwa wingi katika uwanja huo .

Alisema kuwa baaada ya kumaliza mkutano huo ambao kimsingi ulipawa kufanyika leo ataendelea katika jimbo la Njombe Magharibi linalogombewa na Thomas Nyimbo (Chadema) na kufanya mikutano katika kata karibu zote za jimbo hilo kama sehemu ya kuhitimisha kampeni zake ndani ya mkoa wa Iringa.

Awali mgombea ubunge katika jimbo hilo la Iringa mjini akiwahutubiwa wananchi hao awalitaka kutoichagua CCM katika jimbo hilo jumapili na kuwa pamoja na mbinu chafu za CCM kugawa fulana na vyakula ila bado amewataka wananchi kukihukumu chama hicho jumapili.

DK Slaa kabla ya kuingia mkoani Iringa jana alikuwa na mikutano yake ya mwisho ya kusisitiza watazania kujitokeza kwa wingi jumapili kuchagua Chadema ambapo alianza katika mkoa wa Dar es Salaam wilaya ya Temeke, Morogoro ,Dodoma na mkutano wa mwisho ulipaswa kufanyika mkoa wa Iringa katika viwanja hivyo vya Mwembetogwa
 
Kweli watu wa CCm hawajui saicology, hapa kila mkazi wa Iringa atajiuliza kwanini polisi wazuie mkutano wa DR Phd na impact yake ni kuwa kila aliyeenda kumtazama na kufurushwa na polisi atampa kura Dr Slaa kwa hasira.
 
Timua timua ya polisi iringa naona itakuwa imeongeza kura za Dr Slaa
CCM bwana ivi hawajui umaarufu wa Dr Ndo unakua?
 
Kweli watu wa CCm hawajui saicology, hapa kila mkazi wa Iringa atajiuliza kwanini polisi wazuie mkutano wa DR Phd na impact yake ni kuwa kila aliyeenda kumtazama na kufurushwa na polisi atampa kura Dr Slaa kwa hasira.

Hii ni kweli. Hapa kila mtu atatoka akijua kuwa CCM ni majangili wa demokrasia na kura zao zote kwa Dr. Slaa
 
We chama kiko chini ya Makamba!!! Hakuna strategic thinking!! Never!!
 
WALIJARIBU KUTUKIMBIZA ILA ILISHINDIKANA WATU TULIONDOKA BAADA YA KUAMBIWA Dr HAWEZI KUHUTUBIA KUTOKANA NA KUZUILIWA NA POLISI
 
Askari wetu nao ni wajinga wajinga hawajui kuwa DR atakuwa RAIS? Sema tu yule mzee (SLAA) hana kinyongo,angewachinjia baharini wakuu wao
 
FFU hao hao wataweza kutumiwa kuvuruga uchaguzi sehemu ambazo CHADEMA inapendwa. CCM are capable of all kinds of evil.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom