Ferry ya Kigamboni ni sawa na 'Mobile Bridge', sio Meli - Je, wanaovuka Selander nao walipie? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ferry ya Kigamboni ni sawa na 'Mobile Bridge', sio Meli - Je, wanaovuka Selander nao walipie?

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by kichwat, Jan 6, 2012.

 1. kichwat

  kichwat JF-Expert Member

  #1
  Jan 6, 2012
  Joined: Mar 4, 2010
  Messages: 1,822
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 145
  Ndugu wana JF. Kumekuwa na upotoshaji mkubwa kuhusu upandishaji wa gharama za ferry Kigamboni. Wakati watu wengi wakijadili kuhusu nauli ya sh. 100 kwenda sh. 200, kiukweli gharama zilizopandishwa hasa ni za vitu vingine kama magari, maguta, etc.Pia, hoja halisi hapa ni ukweli kwamba kivuko cha Kigamboni ni sawa na 'mobile bridge' kuvusha watu mita mia 2 au 3 tu. Pantoni pale hazitumiki kama MELI kama ilivyo kwenye vivuko vya kule ziwa Victoria. Na kama ni halali kulipia guta sh. 1,800 kuvuka Kigamboni, basi ni bora tukaanzisha utaratibu huo pia kwa wenzetu wanaovuka madaraja mengine kuingia mjini (Selandar, Jangwani, Ubungo, etc.) na hata pale kwa Mkapa kuelekea Mtwara.Nawasilisha.
   
Loading...