Ferooz: Bora niugue UKIMWI kuliko kutumia dawa za kulevya

Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
16,515
28,487
ferouz.jpg


Msanii wa kizazi kipya Ferooz amefunguka na kusema ni bora mtu apate virus vya Ukimwi kuliko kutumia madawa ya kulevya kwani anadai mtu akitumia dawa za kulevya mwisho wake ni kuaibika na kushindwa kufanya mambo ya msingi katika jamii.

Akizungumza kwenye kipindi cha eNewz Ferooz alidai kuwa yeye anaona ni bora mtu apate Ukimwi kwani itawezekana mtu huyo kuishi kwa matumaini, huku akiendelea kufanya mambo yake ya msingi katika jamii na kudai tofauti na mtumiaji wa dawa za kulevya kwani hataweza kufanya jambo lolote la maendeleo.

“Madawa ya kulevya ni zaidi ya kupata HIV, ni mara kumi upate Ukimwi kuliko ukiwa unatumia madawa ya kulevya, sababu Ukimwi unaweza kuishi kwa matumaini na ukatumia madawa za ARVs ukaishi miaka mingi ukadumu,lakini madawa ya kulevya utaadhirika na hautafanya kitu chochote katika maisha yaani utakuwa ‘nothing’ (bure) katika maisha, kwa hiyo ni tatizo baya zaidi hivyo madawa ya kulevya si ya kuyasogelea kabisa,” alisema Ferooz.

Mbali na hilo Ferooz alieleza kuwa wasanii wengi wanajikuta wanaingi kwenye matumizi ya madawa ya kulevya kutokana na msongo wa mawazo kwa kazi zao kutochezwa kwenye vyombo vya habari na kazi hizo kutopokelewa vyema na mashabiki jambo ambalo linawapelekea kuwaza sana hivyo wengine wanaona njia ya kupunguza mawazo hayo ni kunywa viroba kama si kwenda kutumia dawa za kulevya.

Chanzo: IPP Media
 
Kwangu Mimi UKIMWI usikilizie kwa jirani.
Bora nipige madawa ya kulevya nikapona kuliko kupata ngoma na kuendelea kyishi kwa matumaini.
 
Nimeon interview yake moja hiv. Aliuzwa kama anatumia anakataa lakini hana ujasiri wa kusema hatumiii ni mdogo then kutovua shades imeleta more doubts
 
ukimwi kwa saivi umekua kama mafua .ata mtu akiumwa tunapoelekea utaskia nnakaukimwi kamenibana
Hahahaa ...tena na hii hali ya mvua kalinibana juzi kati, nikapiga mazoezi kimtindo aaahhh saivi yaani fuleshi tu mwana.
 
bigonzo Bange sio madawa ya kulevya. Ni sera tu za mababiloni ndio zinasababisha ionekane ni madawa. Ila ukiichunguza kisayansi mneli sio madawa ya kulevya.
 
Hebu tumuangalie Ferooz wa sasa halafu tulinganishe hii kauli yake na muonekano wake je,vinafanana.
images
images
 
Back
Top Bottom