Ferdinand Omanyala: Mtu wa Kwanza Afrika Mashariki na Kati kukimbia mbio za mita 100 chini ya sekunde 10

Tony254

JF-Expert Member
May 11, 2017
16,017
16,427
Huyu kijana wa miraba minne aiseeh anatingisha dunia sasa hivi. Baada ya kuwa Mkenya wa kwanza kufika semi-finals za 100 metres huko Tokyo olympics, sasa amekimbia mita mia moja chini ya sekunde kumi. Awa mtu wa kwanza Africa Mashariki na kati kufanya hivyo.

Hata Afrika Kaskazini ya Waarabu Tunisia, Egypt, Morocco hawajawahi kutoa mwanariadha aliyekimbia 100m chini ya sekunde kumi. Mashindano yalifanyika nchini Austria na alikimbia 9.96 seconds katika mbio za kwanza, halafu akakimbia 9.86 seconds katika fainali.

Halafu tonesha na hii sentensi ................. "8th fastest man in the world".
Yaani baada ya kuchoka kupiga dunia nzima kwenye mbio za masafa marefu, sasa tumeamua kuja kupiga dunia kwenye mbio fupi za mita mia moja.
 
Kenya imeshinda medali nyingi za olympiki kushinda nchi yoyote hapa Afrika.

Huyu kijana wa miraba minne aiseeh anatingisha dunia sasa hivi. Baada ya kuwa Mkenya wa kwanza kufika semi-finals za 100 metres huko Tokyo olympics, sasa amekimbia mita mia moja chini ya sekunde kumi. Awa mtu wa kwanza Africa Mashariki na kati kufanya hivyo.

Hata Afrika Kaskazini ya Waarabu Tunisia, Egypt, Morocco hawajawahi kutoa mwanariadha aliyekimbia 100m chini ya sekunde kumi. Mashindano yalifanyika nchini Austria na alikimbia 9.96 seconds katika mbio za kwanza, halafu akakimbia 9.86 seconds katika fainali.

Sio SIFA, atachanika msamba akose watoto. Vitu vingine ni vya kukuhatarisha sana kwa ajili tu ya kupata kibati walichokipaka rangi ya dhahabu
 
Sio SIFA, atachanika msamba akose watoto. Vitu vingine ni vya kukuhatarisha sana kwa ajili tu ya kupata kibati walichokipaka rangi ya dhahabu
Na pesa je? Hawa wakimbiaji wanapata mihela kibao tu.
 
Sio SIFA, atachanika msamba akose watoto. Vitu vingine ni vya kukuhatarisha sana kwa ajili tu ya kupata kibati walichokipaka rangi ya dhahabu
Watu wanachomoka na kitita cha hela $50,000 kwa sekunde tisa, wengine kwa muda wa masaa mawili na dakika chache tu. Tena hata hilo bati la Olimipiki unalolizungumzia linaandamana na mengine mengi sio sifa tu. Wathamini wanalipa hela nyingi za ziada moja kwa moja kwa wanariadha.

Wanariadha nao wanajenga profile zao pia kama wanaspoti 'pro', ili waweze kualikwa kwenye michuano mingine. Kwa mfano ya Diamond League ambayo huwa inalipa hela ndefu kupindukia. Huku wakizidi kupeperusha bendera na kupigia nchi zao promo.

Wanaochanika misamba bure ni kama yule mwenzenu, sijui Simbu. Ambaye licha ya mazoezi magumu na kukimbia kwenye michuano karibia yote, kote duniani. Hela ambazo huwa zinazawadiwa wanaoshika hata nambari ya tatu tu, huwa anazitafuna sana na kula nazo bata, kwenye ndoto. :D
 
Back
Top Bottom