Feminist huoana, wife material huolewa. Je, unaoa/kuolewa au mnaoana?

Girland

JF-Expert Member
Jan 24, 2016
1,824
2,841
Je Wewe utaoa /kuolewa au utaoana na mwenza wako wa maisha? Maisha yamebadilika Sana zamani ungesikia, mwanamke akisema "huyu ni mume wangu, nimeolewa miaka mitano iliyopita ".Sasahivi utasikia "kuanzia tuoane 🤔ni mwaka sasa "!Je wewe ni muumini wa mrengo upi?

Mfumo wa haki sawa (feminism) unalenga kuleta usawa Kati ya mwanamke na mwanaume. Mfumo huu unapingana na ule halisia (ambao wanauita mfumo dume)!.

Lakini mfumo huu umeishia kuvunja ndoa nyingi na kuzalisha idadi kubwa ya "Single mothers ",kwa sababu ndoa ni ndoa pale ambapo mwanamke atakubali kuolewa!

Sasa "feminisiti "mje hapa mtuambie kwenye ndoa mnataka haki zipi? Kwanini hamkubali kuolewa na mnataka kuoana na waume zenu?

Upande wa pili sifa tele ziwaendee wanawake wanaojielewa (wife material), Hawa hawajikwezi na hawana makuu, ndoa zao zinadumu niamini mimi ni mwanamke ndiye anasababisha ndoa kuendelea au kuvunjika.
 
Mi nataka kumuoa huyu. Sijui atakubali au pengine atataka "anioe" au tuoane. Kazi sana yaani
Screenshot_20190326-152123~2.jpg
 
Mi nataka kumuoa huyu. Sijui atakubali au pengine atataka "anioe" au tuoane. Kazi sana yaani
View attachment 2464131
Kwahyo akiingiza 20m aajiri wafanyakazi au anataka kusema mwanaume ndio apige deki 😂😂😂😂😂😂 hawa wazungu wanatuzuzua sana na haya mambo ya haki sawa siku tukistuka mambo yashaharibika. Wamejua kutuvuruga kuanzia kwenye familia usipokua na familia imara huwez kuwa na nchi thabiti yenye watu wenye msimamo imara
 
Feminist wengi ni mishangazi wameachika wanawarubuni mabinti wadogo wanao chipukia , kwahiyo hii inapelekea ongezeko la single mom kila kukicha .Mim nilishasema mwanamke kama nimekutolea mahari jua kabisa mfumo dume utakuhusu, siwezi kukubali kuharibu future za watoto kwa ujinga huo wa feminists
 
Kwahyo akiingiza 20m aajiri wafanyakazi au anataka kusema mwanaume ndio apige deki 😂😂😂😂😂😂 hawa wazungu wanatuzuzua sana na haya mambo ya haki sawa siku tukistuka mambo yashaharibika. Wamejua kutuvuruga kuanzia kwenye familia usipokua na familia imara huwez kuwa na nchi thabiti yenye watu wenye msimamo imara
Yaani anaamini kwa kipato chake hawezi kumtii mumewe!
 
Back
Top Bottom