Female Genital Mutilation: Tabia ya kutahiri wanawake inabidi ikemewe!

Mwaka huu haugawanyiki kwa mbili ukienda wilaya ya Serengeti na Tarime kuanzia December kuelekea X-mas kunakuwa na shamrashamra za FGM nadhani ndio kipindi muafaka cha kampeni maana kule japokuwa serikali ipo lakini mambo ni hadharani na wakifanya FGM mwaka huu ni mpaka 2014 japokuwa siku hizi wanasema wanatahiri ki-CCM ndio lugha wanayotumia wakimaanisha wanatahiri kisasa kwa kuchuna kidogo. NGO zinazodeal na haya mambo nadhani kule zina kazi za kufanya.
 
Kwa mantiki nzima ya kutahiri wanawake ni nini? Naomba kueleweshwa, kwa kuwa kwetu hakuna kitu hicho!
 
Kwa mantiki nzima ya kutahiri wanawake ni nini? Naomba kueleweshwa, kwa kuwa kwetu hakuna kitu hicho!

Eti kuwafanya mabinti wasiwe na hamu ya tendo la ndoa ili watulie nyumbani. Hivyo hata wakiolewa nasikia huwa ni shida sana kusisimuliwa na kuwa tayari kushiriki kwa furaha tendo hilo na waume zao. Huishia kuumia tu kwani wanakuwa hawajasisimuliwa vya kutosha kuwafanya watoe ile fluid ya kuzuia maumivu pale mume anapokuwa anaingia. Pia kwenye kuzaa napo nasikia ni kasheshe. Kwa kifupi ni ukatili usiofaa kuendekezwa hata kidogo.
 
Back
Top Bottom