Nadhani wanataka endapo EL atapendekezwa na Rais kuwa tena PM, asipate shida ya kupitishwa na wabunge. Maana idadi ya kura itabidi itoshe. Lakini kikubwa zaidi, ni kuhakikisha kuwa Bunge linatumika kufukia na kunyamazisha uwezekano wa mijadala yenye kuumiza baadhi ya wahusika kama ilivyokuwa kipindi kilichopita.
Ni wakati wa kutengeneza njia kwa uchaguzi wa 2015 na kwa kuanzia, itabidi watu wasafishwe kikamilifu kabisa. Nadhani katika hatua hiyo, wapinzani wasipokuwa wamoja, wataanza kupunguzwa ndani ya mjengo kwa kutumia taratibu na kanuni za Bunge.
Mwenye kujua ukweli wa jambo hili atujuze jamani, maana kuna tetesi nimesikia kuna kiasi kikubwa ( approx. 2 millions USD) cha pesa kimechangwa na Felix Mrema wa Arusha, EL na Rostam Aziz kupitia Bank M ( Account gani mi Sijui).
Lengo likiwa ni kum-support ndugu Andrew Chenge Kufanikisha Kuchukua Kiti Cha Uspika. Sababu kubwa ya Felix Mrema Kuchangia mbio hizo inasemekana ni kutokana na Kashfa za ndugu yake wa TANROAD ( Bomu linalosubiriwa Kulipuka) kumgusa Andrew Chenge.
Mwenye Kufahamu lolote ni vizuri akaliweka jamvini ili lifahamike kiuwazi, maana maandalizi ya kuimaliza CCM ndo yameshaanza kushika kasi.
Nawakilisha!

Hizo namba ulizotaja zote(EL,RA,na FM) ni namba mbaya kabisa kwa siasa zinazohusisha fedha kwa hapa nchini!
Najua FM amefurahia sana kuangushwa kwa Batilda, lakini kumbe ame-bank kwa nduguye wa Tanroads!
Kwa hawa watu walivyo, wana uwezo wa kuinfluence sehemu kubwa ya Bunge, hasa ukizingatia kuwa wabunge wengi kwa sasa ni wa kuja, na fedha zao nyingi walizitumia kuhonga, kwahiyo kwasasa wako apeche-alolo, ni rahisi kudanganyika!
Ni ulimbukeni wa wabunge utakua tu,kwanini wasichukue hela na wakapiga kura kwa Sitta au mwingine yeyote?wakati wa lunch nilikuwa naongea na wafanyakazi wenzangu na wengi wao wanasema hawatashangaa CHENGE ikiukwaa uspika. watu watajazwa mahela mpaka wasikie kichefuchefu siku ya kupiga kura wanaona Andrea Chenge tu. Ni jambo la kusikitisha lakini
Tuseme ukweli, bila vijisenti, Chenge hauziki kama Nguruwe Pemba. Tusubiri tuone. Nasikia EL anajiandaa kuingia ikulu 2015. Hivi atauzika kweli? OOOOH, nilisahau kuwa Tanzania anayeamua mshindi wa kura ni anayehesabu na kuchakachua, na siyo wapiga kura. Watanzania jiandaeni 2015, kama mmestaajabu ya Musa 2010, Mtaona ya Firauni 2015.
Mwenye kujua ukweli wa jambo hili atujuze jamani, maana kuna tetesi nimesikia kuna kiasi kikubwa ( approx. 2 millions USD) cha pesa kimechangwa na Felix Mrema wa Arusha, EL na Rostam Aziz kupitia Bank M ( Account gani mi Sijui).
Lengo likiwa ni kum-support ndugu Andrew Chenge Kufanikisha Kuchukua Kiti Cha Uspika. Sababu kubwa ya Felix Mrema Kuchangia mbio hizo inasemekana ni kutokana na Kashfa za ndugu yake wa TANROAD ( Bomu linalosubiriwa Kulipuka) kumgusa Andrew Chenge.
Mwenye Kufahamu lolote ni vizuri akaliweka jamvini ili lifahamike kiuwazi, maana maandalizi ya kuimaliza CCM ndo yameshaanza kushika kasi.
Nawakilisha!
Na kuonyesha kuwa CCM ya mafisadi imemwandaa Chenge kuwa spika TAKUKURU imesema haijapata sababu ya kutosha kumhusisha Chenge na sakata lile la rushwa sasa jiulize kwa nini watoe tamko leo hii wakati chenge anagombea hiyo nafasi. OMG mtajuuuuuta kumchagua kikwete na CCM yake huu ni upuuzi kupindukia yaani tunafanywa ni wajinga wa kutupwa hapa lol na akipita yeye tunarudi zama za Msekwa mambo ya kaa chini usiungumze OMG my Tanzania is drowning
BREKING NYUUUUUZZZZ: TAKUKURU YATOA TAMKO JUU YA CHENGE
Bosi wa TAKUKURU Dk. Edward Hosea
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
YAH: UCHUNGUZI KUHUSU TUHUMA ZA RADA
Tunapenda kuujulisha umma kuwa uchunguzi na ushahidi uliokusanywa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) pamoja na Shirika la Upelelezi - SFO la Uingereza kuhusu tuhuma za Rushwa katika ununuzi wa Rada, umeshindwa kumhusisha Bw. Andrew Chenge katika tuhuma hizo.
TAKUKURU inawaomba wananchi waendelee kutoa ushirikiano kwa chombo hiki kwa kutoa taarifa za kuwafichua wale wote wanaojihusisha na Rushwa kwani jukumu hili ni la kila mmoja wetu.
Imetolewa na
Doreen J. Kapwani,
Afisa Uhusiano-TAKUKURU
Novemba 08 , 2010
S. L.P. 4865,
Dares Salaam.
Simu: 2150043-6/2150360
Nukushi: (022) 2150047
Baruapepe:dgeneral@pccb.go.tz
Mtandao Prevention and Combating of Corruption Bureau