Felix Mrema, Edward Lowassa na Rostam Aziz wamsupport Andrew Chenge Kupitia Bank M

payuka

JF-Expert Member
Jun 17, 2010
832
0
Nadhani wanataka endapo EL atapendekezwa na Rais kuwa tena PM, asipate shida ya kupitishwa na wabunge. Maana idadi ya kura itabidi itoshe. Lakini kikubwa zaidi, ni kuhakikisha kuwa Bunge linatumika kufukia na kunyamazisha uwezekano wa mijadala yenye kuumiza baadhi ya wahusika kama ilivyokuwa kipindi kilichopita.

Ni wakati wa kutengeneza njia kwa uchaguzi wa 2015 na kwa kuanzia, itabidi watu wasafishwe kikamilifu kabisa. Nadhani katika hatua hiyo, wapinzani wasipokuwa wamoja, wataanza kupunguzwa ndani ya mjengo kwa kutumia taratibu na kanuni za Bunge.
Hapo kwenye red mkuu, nakubaliana nawewe ndiyo lengo la purukushani zote.
 
Mchili

JF-Expert Member
Aug 19, 2009
726
195
Inabidi watanzania waandamane na mawe wawakong'ote wabunge kwa kuwasaliti na kumpitisha Chenge kuwa Spika.
 
Jan 8, 2010
40
70
Jamani jamani nchi hii inataka kwenda wapi? Watu hawana haya! Ukishakuwa na doa tosha kupumzika hizi nafasi watu wasiwe kama wawezaliwa kuongoza tu.hivi wanauchungu na nchi hii au wana lawo jambo? Watanzania tuwe makini nawaomba
 
Bi. Mkora

JF-Expert Member
Oct 29, 2010
375
170
Mwenye kujua ukweli wa jambo hili atujuze jamani, maana kuna tetesi nimesikia kuna kiasi kikubwa ( approx. 2 millions USD) cha pesa kimechangwa na Felix Mrema wa Arusha, EL na Rostam Aziz kupitia Bank M ( Account gani mi Sijui).

Lengo likiwa ni kum-support ndugu Andrew Chenge Kufanikisha Kuchukua Kiti Cha Uspika. Sababu kubwa ya Felix Mrema Kuchangia mbio hizo inasemekana ni kutokana na Kashfa za ndugu yake wa TANROAD ( Bomu linalosubiriwa Kulipuka) kumgusa Andrew Chenge.

Mwenye Kufahamu lolote ni vizuri akaliweka jamvini ili lifahamike kiuwazi, maana maandalizi ya kuimaliza CCM ndo yameshaanza kushika kasi.

Nawakilisha!

Anything is possible kwa Tanzania.
 
EDOARDO

Senior Member
Oct 4, 2010
115

:sad:Hao mafisadi wanatumia pesa zao kuwahonga Watu wasio na pesa lakini wana nafasi fulani katika jamii. Sasa hao wawakilishi wetu wasipokuwa makini wakaendekeza njaa, mapenzi ya mafisadi yatatimizwa. Hapo kuna namba hatari sana kwa ushawishi wa kutumia pesa mfano namba EL, RA na FM. Kama wakiboronga wameumiza Tanzania.
 
Safari_ni_Safari

JF-Expert Member
Oct 5, 2007
23,311
2,000
Waacheni wazidi kuchimba kaburi lao...wamejiruzuku miaka mitano ijayo kwa kuchakachua sasa wanarudia madudu...2015 watakuwa kaburini
 
Reyes

Senior Member
Sep 1, 2010
188
0
wanataka kutuchagulia hata waziri mkuu kivuli, yaani wanataka kuingiza madudu yao hata upinzani
Mungu atusaidie
 
Shomoro

Senior Member
Aug 22, 2010
111
195
Hizo namba ulizotaja zote(EL,RA,na FM) ni namba mbaya kabisa kwa siasa zinazohusisha fedha kwa hapa nchini!
Najua FM amefurahia sana kuangushwa kwa Batilda, lakini kumbe ame-bank kwa nduguye wa Tanroads!
Kwa hawa watu walivyo, wana uwezo wa kuinfluence sehemu kubwa ya Bunge, hasa ukizingatia kuwa wabunge wengi kwa sasa ni wa kuja, na fedha zao nyingi walizitumia kuhonga, kwahiyo kwasasa wako apeche-alolo, ni rahisi kudanganyika!
"Cool"
 
Sir John

Senior Member
Aug 19, 2010
177
0
wakati wa lunch nilikuwa naongea na wafanyakazi wenzangu na wengi wao wanasema hawatashangaa CHENGE ikiukwaa uspika. watu watajazwa mahela mpaka wasikie kichefuchefu siku ya kupiga kura wanaona Andrea Chenge tu. Ni jambo la kusikitisha lakini
Ni ulimbukeni wa wabunge utakua tu,kwanini wasichukue hela na wakapiga kura kwa Sitta au mwingine yeyote?
 
Overcomer

New Member
Nov 2, 2010
1
0
Tuseme ukweli, bila vijisenti, Chenge hauziki kama Nguruwe Pemba. Tusubiri tuone. Nasikia EL anajiandaa kuingia ikulu 2015. Hivi atauzika kweli? OOOOH, nilisahau kuwa Tanzania anayeamua mshindi wa kura ni anayehesabu na kuchakachua, na siyo wapiga kura. Watanzania jiandaeni 2015, kama mmestaajabu ya Musa 2010, Mtaona ya Firauni 2015.
Eeeh Mungu mwenye enzi yote muumba wa mbingu na nchi,wewe umesema katika maneno yako kwamba Haki uinua Taifa,tunaomba haki kwa Taifa letu la Tanzania tunajua haki yako ikisimama ee Bwana ,hakuna fisadi yoyote atakalia kiti cha ukuu wa nchii,tunaomba eeh Mungu Baba ututetee wanyonge wa Tanzania maana sasa ni mwisho wa wezi kutawala na kutumia hela kutawala Taifa letu zuri.
Bwana tunajua hujatuweka Tanzania kwa makosa kwa kusudi hilo tunaomba eeh Bwana utuwezeshe tufurahie rasilimali ulizotubariki nazo na amani.
 
PapoKwaPapo

JF-Expert Member
Jun 5, 2008
380
0
jamani kwangu mimi chenge na sitta ni wale wale hakuna mwenye afadhali, wacha tutaabike kidogo kwasababu waswahili wanasema mkataa pema pabaya panamwita........tulimkataa Slaa sasa wacha watuonyeshe ngoma inavyochezwa.
 
Gosbertgoodluck

JF-Expert Member
Mar 3, 2008
2,862
0
Mwenye kujua ukweli wa jambo hili atujuze jamani, maana kuna tetesi nimesikia kuna kiasi kikubwa ( approx. 2 millions USD) cha pesa kimechangwa na Felix Mrema wa Arusha, EL na Rostam Aziz kupitia Bank M ( Account gani mi Sijui).

Lengo likiwa ni kum-support ndugu Andrew Chenge Kufanikisha Kuchukua Kiti Cha Uspika. Sababu kubwa ya Felix Mrema Kuchangia mbio hizo inasemekana ni kutokana na Kashfa za ndugu yake wa TANROAD ( Bomu linalosubiriwa Kulipuka) kumgusa Andrew Chenge.

Mwenye Kufahamu lolote ni vizuri akaliweka jamvini ili lifahamike kiuwazi, maana maandalizi ya kuimaliza CCM ndo yameshaanza kushika kasi.

Nawakilisha!
Fedha haziwezi kufua dafu mbele ya nguvu ya umma.
 
sensa

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
396
170
Tanzania si kisiwa cha amani tena,kimegeuka kuwa KISIWA CHA UFISADI.
 
Edo

JF-Expert Member
Jun 11, 2008
728
170
Tatizo, kwenye mchujo wa CC ya CCM Sitta atapita?, lakini wakikosea wakaingia kwenye kura, Sitta atawatoa jasho!
 
msafiri.razaro

JF-Expert Member
Oct 12, 2010
1,102
2,000
Duh, Sasa naona kufuru hii, uchaguzi huu umewafanya wajiamini sana maana hata TAKUKURU wako mifukoni mwao, Jamani chonde tuzunmzie KATIBA MPYA na TUME HURU YA UCHAGUZI, siummesikia jeuri ya makamba, 2015 wao pia.
 
RayB

JF-Expert Member
Nov 27, 2009
2,753
1,250
Na kuonyesha kuwa CCM ya mafisadi imemwandaa Chenge kuwa spika TAKUKURU imesema haijapata sababu ya kutosha kumhusisha Chenge na sakata lile la rushwa sasa jiulize kwa nini watoe tamko leo hii wakati chenge anagombea hiyo nafasi. OMG mtajuuuuuta kumchagua kikwete na CCM yake huu ni upuuzi kupindukia yaani tunafanywa ni wajinga wa kutupwa hapa lol na akipita yeye tunarudi zama za Msekwa mambo ya kaa chini usiungumze OMG my Tanzania is drowning

BREKING NYUUUUUZZZZ: TAKUKURU YATOA TAMKO JUU YA CHENGE

Bosi wa TAKUKURU Dk. Edward Hosea

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
YAH: UCHUNGUZI KUHUSU TUHUMA ZA RADA

Tunapenda kuujulisha umma kuwa uchunguzi na ushahidi uliokusanywa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) pamoja na Shirika la Upelelezi - SFO la Uingereza kuhusu tuhuma za Rushwa katika ununuzi wa Rada, umeshindwa kumhusisha Bw. Andrew Chenge katika tuhuma hizo.

TAKUKURU inawaomba wananchi waendelee kutoa ushirikiano kwa chombo hiki kwa kutoa taarifa za kuwafichua wale wote wanaojihusisha na Rushwa kwani jukumu hili ni la kila mmoja wetu.

Imetolewa na
Doreen J. Kapwani,
Afisa Uhusiano-TAKUKURU
Novemba 08 , 2010
S. L.P. 4865,
Dares Salaam.

Simu: 2150043-6/2150360
Nukushi: (022) 2150047
Baruapepe:dgeneral@pccb.go.tz
Mtandao Prevention and Combating of Corruption Bureau
 
Paka_Shume

Member
Jun 22, 2007
59

Yaleyale yakufunga paka kengele...Cheyo ndio aliyemshauri Mkapa kuundwa kwa TAKUKURU wakati akiwa Waziri wa Sheria. Na Mkapa akampa get go, kwa hiyo watu wote waliko huko ni yeye ndio aliwaingiza, kwa hiyo ni vigumu kumshutumu na skendeli zote. It is sad lakini ndio ukweli..
 
Top Bottom