Felix Mrema, Edward Lowassa na Rostam Aziz wamsupport Andrew Chenge Kupitia Bank M | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Felix Mrema, Edward Lowassa na Rostam Aziz wamsupport Andrew Chenge Kupitia Bank M

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by payuka, Nov 8, 2010.

 1. payuka

  payuka JF-Expert Member

  #1
  Nov 8, 2010
  Joined: Jun 17, 2010
  Messages: 832
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Mwenye kujua ukweli wa jambo hili atujuze jamani, maana kuna tetesi nimesikia kuna kiasi kikubwa ( approx. 2 millions USD) cha pesa kimechangwa na Felix Mrema wa Arusha, EL na Rostam Aziz kupitia Bank M ( Account gani mi Sijui).

  Lengo likiwa ni kum-support ndugu Andrew Chenge Kufanikisha Kuchukua Kiti Cha Uspika. Sababu kubwa ya Felix Mrema Kuchangia mbio hizo inasemekana ni kutokana na Kashfa za ndugu yake wa TANROAD ( Bomu linalosubiriwa Kulipuka) kumgusa Andrew Chenge.

  Mwenye Kufahamu lolote ni vizuri akaliweka jamvini ili lifahamike kiuwazi, maana maandalizi ya kuimaliza CCM ndo yameshaanza kushika kasi.

  Nawakilisha!
   
 2. payuka

  payuka JF-Expert Member

  #2
  Nov 8, 2010
  Joined: Jun 17, 2010
  Messages: 832
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Nadhani jamaa watatumia Nguvu Kubwa ya Pesa ili kufanikisha azma yao, na mwisho wa siku wataweza kuzima mijadala mingi tu ya kifisadi.
   
 3. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #3
  Nov 8, 2010
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,174
  Likes Received: 892
  Trophy Points: 280
  Wabumge "La Saba" na "Fom Foo" wa CCM kaeni mkao wa kula.

  Kura kwa Samuel Sita
   
 4. Ngisibara

  Ngisibara JF-Expert Member

  #4
  Nov 8, 2010
  Joined: Jan 2, 2009
  Messages: 2,083
  Likes Received: 431
  Trophy Points: 180
  Inawezekana kwani vita ndani ya CCM iliyoko mbele kuelekea 2015 si lelemama, tayari wameshaanza kujipanga wakiamini kuwa watapewa ulinzi wote wa dola kutoka kwa JK wakati utakapofikia huku wakiwa wamesahau kuwa wadanganyika watakuwa wameshachoka mbaya na watakuwa hawasikii la mjumbe wala mkuu wa kaya na hapo ndipo mbanduebandue ya Kenya itakapopiga hodi Tanzania...Over my neck Lowassa hawezi kuwa eti Rais wangu bora nijifirieko mbali nijue mmoja
   
 5. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #5
  Nov 8, 2010
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Nsubiria wadau wachangie, binafsi sina cha kusema.
   
 6. K

  Kichakoro JF-Expert Member

  #6
  Nov 8, 2010
  Joined: Sep 10, 2008
  Messages: 1,545
  Likes Received: 1,293
  Trophy Points: 280
  Lisemwalo lipo..... Huoni courage aliyokua nayo CHENGE hata ya Kumshutumu SITA hadharani ni kubwa kuliko kasha alizokua nazo. so something is boiling......
   
 7. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #7
  Nov 8, 2010
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  mhhhh
   
 8. payuka

  payuka JF-Expert Member

  #8
  Nov 8, 2010
  Joined: Jun 17, 2010
  Messages: 832
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Nakubaliana na wewe mkuu, nadhani tusubiri na kama kuna ukweli tutajua!
   
 9. K

  Kiti JF-Expert Member

  #9
  Nov 8, 2010
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 228
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Tuseme ukweli, bila vijisenti, Chenge hauziki kama Nguruwe Pemba. Tusubiri tuone. Nasikia EL anajiandaa kuingia ikulu 2015. Hivi atauzika kweli? OOOOH, nilisahau kuwa Tanzania anayeamua mshindi wa kura ni anayehesabu na kuchakachua, na siyo wapiga kura. Watanzania jiandaeni 2015, kama mmestaajabu ya Musa 2010, Mtaona ya Firauni 2015.
   
 10. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #10
  Nov 8, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Hizo namba ulizotaja zote(EL,RA,na FM) ni namba mbaya kabisa kwa siasa zinazohusisha fedha kwa hapa nchini!
  Najua FM amefurahia sana kuangushwa kwa Batilda, lakini kumbe ame-bank kwa nduguye wa Tanroads!
  Kwa hawa watu walivyo, wana uwezo wa kuinfluence sehemu kubwa ya Bunge, hasa ukizingatia kuwa wabunge wengi kwa sasa ni wa kuja, na fedha zao nyingi walizitumia kuhonga, kwahiyo kwasasa wako apeche-alolo, ni rahisi kudanganyika!
   
 11. Power to the People

  Power to the People JF-Expert Member

  #11
  Nov 8, 2010
  Joined: Jul 11, 2007
  Messages: 1,193
  Likes Received: 238
  Trophy Points: 160
  wakati wa lunch nilikuwa naongea na wafanyakazi wenzangu na wengi wao wanasema hawatashangaa CHENGE ikiukwaa uspika. watu watajazwa mahela mpaka wasikie kichefuchefu siku ya kupiga kura wanaona Andrea Chenge tu. Ni jambo la kusikitisha lakini
   
 12. payuka

  payuka JF-Expert Member

  #12
  Nov 8, 2010
  Joined: Jun 17, 2010
  Messages: 832
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Kama Kawaida, NGUVU YA PESA achana nayo! Inawapiga kikumbo hadi TAKUKURU simchezo.
   
 13. r

  realtz7 Senior Member

  #13
  Nov 8, 2010
  Joined: Oct 23, 2010
  Messages: 110
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  itajinyonga chenge akiwa spika na may be itakuwa mwisho wa ccm ya sasa na kuanzishwa live udkteta na kulipizana vsasi, apewe sitta, wabunge waeu shauri yenu msituangushe kuleni hela na Sitta apite hope hata JK anatamani sitta apite
   
 14. njiwamanga

  njiwamanga Member

  #14
  Nov 8, 2010
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 35
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nguvu ya pesa haishindi nguvu ya umma.Alipofukuzwa Zito bungeni umma uliungana kuwazomea safari tutawapiga mawe wabunge wakimchagua Chenge wapinzani watafanya kazi kirahisi ya kuomba umma uamue
   
 15. Mallaba

  Mallaba JF-Expert Member

  #15
  Nov 8, 2010
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 2,560
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  may be??????:rip:
   
 16. njiwamanga

  njiwamanga Member

  #16
  Nov 8, 2010
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 35
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni VIZURI SANAAAAAX1000000000 Ili umma uwaondoe kwa urahisi nguvu ya pesa haiwezi kushinda nguvu ya umma
   
 17. M

  Mndamba Namba 1 Senior Member

  #17
  Nov 8, 2010
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 113
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Binafsi nimeshangaa sana na ujasiri aliokuwa nao mbunge mteule Chenge wakati alikuwa kimya kama nyau,nahisi kuna jambo nyuma ya pazia....................tusubiri yetu macho
   
 18. Ehud

  Ehud JF-Expert Member

  #18
  Nov 8, 2010
  Joined: Feb 12, 2008
  Messages: 2,696
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Chenge yupo kwenye kundi linalotaka kumtoa rais wa 2015 kwa hiyo wanafanya wawezavyo ikiwamo kuwatukana watanzania ili malengo yao yafanikiwe
   
 19. A

  A Lady Senior Member

  #19
  Nov 8, 2010
  Joined: Apr 28, 2009
  Messages: 103
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wacha wamuweke Chenge! hata wakiamua warudishe EL. Am sorry but nataka wadanganyika waadhibiwe kisawasawa ili ikifika 2015 au hata isifike wajue jinsi ya kudai haki yao! Maana naona somo haliwaingii akilini. Hawa watu lao moja kuanzia JK mwenyewe, kuinyonya nchi yetu mpaka ipate anorexia.
   
 20. Recta

  Recta JF-Expert Member

  #20
  Nov 8, 2010
  Joined: Dec 8, 2006
  Messages: 854
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Nadhani wanataka endapo EL atapendekezwa na Rais kuwa tena PM, asipate shida ya kupitishwa na wabunge. Maana idadi ya kura itabidi itoshe. Lakini kikubwa zaidi, ni kuhakikisha kuwa Bunge linatumika kufukia na kunyamazisha uwezekano wa mijadala yenye kuumiza baadhi ya wahusika kama ilivyokuwa kipindi kilichopita.

  Ni wakati wa kutengeneza njia kwa uchaguzi wa 2015 na kwa kuanzia, itabidi watu wasafishwe kikamilifu kabisa. Nadhani katika hatua hiyo, wapinzani wasipokuwa wamoja, wataanza kupunguzwa ndani ya mjengo kwa kutumia taratibu na kanuni za Bunge.
   
Loading...