Felix Mrema ahojiwa polisi kwa kutishia maisha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Felix Mrema ahojiwa polisi kwa kutishia maisha

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MziziMkavu, May 19, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  May 19, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,615
  Trophy Points: 280
  MBUNGE wa Arusha Mjini kwa tiketi ya CCM, Felex Mrema jana alihojiwa kituo cha polisi kwa zaidi ya dakika 40 kwa tuhuma za kumtishia maisha mwandishi wa habari.

  Habari zilizolifikia gazeti hili zimeeleza kuwa mbunge huyo alikamatwa jana majira ya saa 7:00 mchana na kuhojiwa katika kituo kikuu cha polisi mjini hapa kwa kutoa maneno ya vitisho kwa mwandishi wa gazeti la Arusha Raha, Fortunatus Rutta.


  Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha, Matei Basilio alithibitisha taarifa za kuhojiwa kwa mbunge huyo kwenye kituo hicho kikuu cha polisi mjini hapa.


  Mbunge huyo anadaiwa kutoa maneno ya vitisho kwa mwanadishi huyo baada ya kuripoti taarifa ambazo mbunge huyo hakutaka ziandikwe.


  Habari iliyomchukiza mbunge huyo ni ile iliyotolewa na gazeti hilo na kueleza kuwa yupo katika hali mbaya kisiasa na kwamba kundi linalosadikiwa kumpigia kampeni limeanza mbio hizo mapema na kabla ya wakati muafaka.


  Ilidaiwa kuwa mbunge huyo pia amekuwa akitumia majukwaa kujipigia kampeni mapema kwa wazi licha ya kushutumiwa na baadhi ya viongozi wa chama chake kwa kukiuka ratiba yao.


  Mbunge huyo pia aliripotiwa na gazeti hilo kuwa aliingiza mila na desturi za mila ya Kimaasai katika eneo la Terat alipofanya ziara hivi karibuni na kukutana na vikwazo baada ya baadhi ya wananchi kukataa mbunge huyo kuhutubia kwa sababu mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kuhoji alikuwa wapi miaka iliyopita.


  Mara baada ya taarifa hizo, mbunge huyo anadaiwa alimtishia kwa maneno mwandishi huyo katika eneo la Manispaa ya Arusha na kumweleza kwamba siku zake za uandishi wa habari zinahesabika kwa sababu taarifa anazoandika dhidi yake, hazimpendezi.


  Kamanda Basilio alisema kuwa sheria haichagui mtenda kosa na kwamba taratibu hizo zikikamilika, mbunge huyo ataitwa na jeshi hilo na sheria kufuata mkondo.


  Mmoja wa viongozi wa Chama cha Waandishi wa Habari Arusha (APC), Claud Gwandu, ambaye pia ni mhariri mkuu wa gazeti hilo, alisema kuwa ni kweli mwanadishi wake ametishiwa na taarifa zimeshafikishwa kituo kikuu cha polisi na kwamba wanasubiri atiwe mbaroni.


  "Mpaka jana tulishaandika maelezo na tunasubiri Jeshi la Polisi limtie mbaroni na kufuatwa kwa taratibu nyingine," alisema Gwandu.


  Chanzo: Gazeti la Mwananchi
   
 2. K

  Kagasheki Member

  #2
  May 19, 2010
  Joined: Apr 12, 2010
  Messages: 34
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huyu jimbo kashalipoteza siku nyingi ni suala la muda tu kumuachie mwenzake nae alitawale.Hivyo vitisho anavyovitoa vinazidi kumdhalilisha zaidi kwa wapiga kura wake ambao wameshamchoka.
   
 3. Y

  Yetu Macho JF-Expert Member

  #3
  May 19, 2010
  Joined: Jun 15, 2008
  Messages: 223
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Mzee mzima akubali tu matokeo akaendelee kulima maua. Hilo jimbo si lake tena kwa namna yeyote ile. 2005 walitumia kila njama ikiwemo wizi wa kura(maana huu ndo mchezo wa CCM) kumpokonye Lema wa TLP ambae wote tuliamini lilikua liwe lake. Sasa vita ni inaanzia ndani ya chama.

  Haponi mtu mzee. Mdororo wa uchumi unaanza kupungua so biashara ya maua itaanza rudia chart yake so ni bora kuelekeza nguvu zako huko.

  Yetu macho
   
 4. Jethro

  Jethro JF-Expert Member

  #4
  May 19, 2010
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 2,223
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  Huyo bwana nasikia ndio Tycoon wa mjini hapo hata mbwabwaje vipi navyosikia kushinda kwake hua ni mipango swafi na hukaaa kimya tuuu huko wagombea wengine mwapalangana na hupita bila ubishi, na uhakika wapinzani wake watatumia pesa nyingi sana kuwaweka sawa UVCCM Arusha Mjini(Wilaya nzima)
   
 5. N

  Nyauba JF-Expert Member

  #5
  May 19, 2010
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 1,098
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Jamaa naona muda wake ndo wafikia ukingoniiii..ni wakati wa arusha mjini kuwa na mbunge mpyaaa...

  kila la kheri mbunge mtarajiwa wa arusha mjini dk batilda burian.
   
 6. andrewk

  andrewk JF-Expert Member

  #6
  May 19, 2010
  Joined: Apr 13, 2010
  Messages: 3,103
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  :target:
   
Loading...