Félicien Kabuga: Mahakama ya Ufaransa yaamuru mshukiwa wa mauaji ya kimbari nchini Rwanda ashtakiwe Tanzania

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,000
9,861
Mahakama moja ya kukata rufaa nchini Ufaransa imekubali kumpeleka msukiwa a mauaji ya kimbari nchini Rwanda Felicein kabuga kushitakiwa nchini Tanzania. Bwana kabuga alikamatawa nyumbani kwake nje ya mji wa Paris baada ya miaka 26 kama mtoro.

Takriban watu 800,000 waliauwa nchini Rwanda katika mauaji ya kimbari ya 1994. Bwana kabuga anadaiwa kupitisha fedha katika makundi ya waasi akiwa mwenyekiti wa hazina ya ulinzi ya kitaifa.

Amekana madai yote hayo. Wakati wa kusikilizwa kwa kesi yake mwezi Mei, alielezea madai hayo kama ya uwongo.

Je Filicien Kabuga ni nani?
Ndiye aliyekuwa mtu tajiri zaidi nchini Rwanda kabla ya mauaji ya 1994.

Akijipatia utajiri wake kupita biashara ya majani ya chai mwaka 1970 na alifanya biashara katika sekta chungu nzima, nyumbani na katika mataifa ya kigeni.

Alikuwa mshirika wa karibu wa chama tawala cha MRND – na alikuwa na uhusiano na rais wa zamani Juvenal Habyarimana ambaye alifariki 1994.

Akituhumiwa kwa kuwa mfadhili mkuu wa mauaji hayo na kutumia biashara yake na uwezo wake kupanga na kufadhili mauaji.
Mmiliki wa kituo cha redio ya kibinafsi RTLM alishutumiwa kwa kuwachochea watu wa kabila la Hutu kuwaua Watutsi.

Mwaka 2006, jopo la kimataifa la Rwanda lililokuwa likichunguza mauaji hayo lilisema lina ushahidi kwamba bwana Kabuga alizuru nchini Kenya ama hata kuishi nchini humo, ambapo alikuwa akisimamia maslahi yake ya kibishara.

Miaka mitatu baadaye, Bwana Stephen Rapp, ambaye alikuwa balozi wa Marekani aliishutumu serikali ya Kenya kwa kukataa kumtoa bwana Kabuga.

Kulikuwa na ushahidi kwamba bwana Kabuga alihudhuria hafla zilizoshirikisha watu maarufu, alisema madai ambayo Kenya imekana.
Ni wazi kwamba familia ya bwana Kabuga ilikuwa ikimiliki mali nchini Kenya baada ya mali moja kuzongwa na kesi 2015 wakati mkewe, Josephine Mukazitoni , ambaye alikuwa mmiliki mwenza , alipojaribu kumiliki. (BBC)

1601478495338.png
 
Hiyo inazihirisha Magufuli anavyokubarika duniani
Utakuwa una kichaa ila bahati mbaya hujui kuwa ni kichaa, Kuja kushtakiwa Tanzania ambako ndio mahakama ya kimbari ilipokuwepo kabla ya kufungwa rasmi 2015 na mamlaka yake kuchukuliwa na Mahakama za kimataifa za jinai MICT kwa ajili ya watuhumiwa wa mwisho.
Sasa kuna uhusiano gani na kukubalika kwa Magufuli? Unafikiri wanakuja kuwekeza hapa?
 
Yaani asilimia 80 mwafrika ana roho ya kinyama kabisa hana akili na mjinga na ndio maana mpaka leo masikini.

Yaani unafadhili mauaji ya waafrika wenzio hivihivi badala ya kutumia pesa zake kufanya maendeleo ya waafrika wenzake.
 
Kunna wengine tunao humu nchini wana wasiojulikana.

Wapo afirika pia wanaamini kuwa wengine waliumbwa bahati mbaya ndiyo maana wanawarudisha kwa Mungu aliyewaumba?
 
Yaani asilimia 80 mwafrika ana roho ya kinyama kabisa hana akili na mjinga na ndio maana mpaka leo masikini.

Yaani unafadhili mauaji ya waafrika wenzio hivihivi badala ya kutumia pesa zake kufanya maendeleo ya waafrika wenzake.
Adolph Hittler alikua mwafrika wa nchi gani?
 
Mahusiano ya magufuli na kushtakiwa Tz ,mahakama ilipo (Arusha) Kama sijakosea ni yapi? Watanzania elimu itukomboe tusiwe wanafiki,na mihemko ya kijinga
Kuna Tatizo
Yawezekana Alikuwa Hajui Vizuri Kuhusu Mahakama Ya Kimbari
 
Utakuwa una kichaa ila bahati mbaya hujui kuwa ni kichaa, Kuja kushtakiwa Tanzania ambako ndio mahakama ya kimbari ilipokuwepo kabla ya kufungwa rasmi 2015 na mamlaka yake kuchukuliwa na Mahakama za kimataifa za jinai MICT kwa ajili ya watuhumiwa wa mwisho.
Sasa kuna uhusiano gani na kukubalika kwa Magufuli? Unafikiri wanakuja kuwekeza hapa?
Aisee kama itakuwa hajaelewa bs aende tu mirembe moja kwa moja
 
mngeachana na hizo biashara mnapoteza muda waliokufa walishakufa gangeni yajayo ...
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom