Feedback: Tatizo la Fungus sugu kwenye Nyeti, Dawa iliyonipa Relief na namna ya kulitibu kabisa.

Mar 13, 2019
64
30
Wakuu habari,

Kama mnakumbuka muda kadhaa uliopita, nilipandisha uzi hapa Jamvini kuomba ushauri wa kitabibu kuhusu tatizo la Fungus sugu kwenye Nyeti lililokua linatusumbua mimi na mke wangu kipenzi

Niwashukuru sana wote mlionipa ushauri na jinsi ya kulitatua hili tatizo. Kwa kweli sasa hivi mimi na mke wangu tunaendelea vizuri.

Nilipokea ushauri mwingi sana ila nikaamua nianze na mmoja kwanza maana ni ngumu kufuata kila ushauri kwa wakati mmoja.

Nilianza na ushauri wa ndugu American Ninja ambaye alinihakikishia kuwa, kuna dawa anayoiamini kabisa inaweza kutusaidia, nayo ni SKDERM CREAM.

Niliinunua hii dawa na tukaanza kuitumia mimi na wife. Baada ya wiki moja tukaanza kupata releaf. Na hadi sasa muwasho umepotea.

Shida moja ambayo ipo, ni baada ya kuitumia kama wiki mbili hivi, tukasema tuache kutumia tuone.. Baada ya siku mbili tu, muwasho ukaanza kurudi kwa mbaali, ila tukitumia dawa unakata.

Kuhusu usafi, tunazingatia sana usafi. Kila siku tunaweka shuka safi, nguo za ndani tunazifua na kuzianika juani na kuzipiga pasi kabla ya kuvaa.

Kwakua nimeshafika hatua hii ndugu zangu, nisaidieni tena ili niweze kulimaliza permanently hili suala na tukae bila kupaka dawa. Coz tukiacha tu dawa, linaanza kurudi tena hili suala la muwasho...

Msichoke kutupa msaada wenu.

Natanguliza shukrani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dawa ya kupaka ni nzuri tuu kama hilo tatizo haliko kwenye damu. Kama liko kwenye damu hiyo cream itakuwa ya kupooza tuu; ushauri wangu kamwone daktari ili akupe dawa ya kuondoa tatizo kwenye damu
 
Mkuu tumia limao paka maeneo yaliyoathilika asubuhi na jioni, kuna uzi uko humu kuna mtu alikua na tatizo kama lako alitumia njia akapona ila anadai mwanzoni kuna maumivu fulani ila ndani ya siku chache yanaisha.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu pole sana na tatizo lako sema hizo Dawa zina create addiction acheni kutumia tumieni mafuta ya Nazi sijui huwa yana nini yaani utapona kabisa
 
poleni sana..! tumia kitunguu swaumu kuleni punje mbili jioni kwa siku7 huku mkipaka( wewe utapakapa ilawifiyangu yeye ataponda kisha aweke kwenye kitambaa safi kidogoaweke kuko kwa usiku...within 7 days mtapona kabisa.
 
Mkuu ungepata na yakumeza utumie pamoja mfano (fluconazole)..then uendelee kupaka hiyo cream as long as possible..taratibu zitapungua na mwishoni kuisha

Kingine ni hakikisha hizo za kupaka hazina steroid,maana utaongeza shida juu ya shida..
 
Mkuu pole Sana kuna Mdau aliwahi post humu na mimi Ndio dawa ninayoitumia nipatapo fungus.chukua nusu dozi ya septrine .Visage vidonge viwe unga kabisa then changanya na Mafuta ya vaseline ya mgandoLile kopo Dogo changanya vizuri kisha paka baada ya kuoga asubuhi na Jion ndani ya siku mbili utaanza kuona mabadiliko na utapona kabisa.
 
Hii dawa kuna jamaa yangu anaitengenezaga anauza

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom