FEEDBACK: Baada ya Maoni na Mtazamo wa Wananchi Kuhusu Ajali ya Meli Nungwi PEMBA

GHOST RYDER

JF-Expert Member
Jun 10, 2011
1,025
475
Halikuwa kusudio letu kumchonganisha yeyote na lolote katika thread nyingi zilizoandikwa hapa jana juu ya fikara za hatua gani ingekuwa ya busara zaidi katika kushughulikia maafa haya badala ya kulaumiana kama alivyohadharisha hapa Mzee Mwanakijiji katika post ya mapema kwenye thread ya slidingRoof.

Watanzania wengi jana waliitikia wito na licha ya maandalizi mazuri ya Tamasha la VODACOM Miss Tanzania, tunaarifiwa lililazimika kucheleweshwa kuanza kutokana na idadi ndogo ya wahudhuriaji kutokana na wenye mapenzi mema na wenzao waliotangulia mbele ya haki kususia kwenda huko licha ya kuwa Ticket zote ziliuzwa na kwisha jana saa 5 asubuhi katika vituo vya kuuza Ticket.

Matukio mengi sasa ni dhahiri yanafuata baada ya kukosa umakini na maamuzi ya Haraka ya watendaji katika kada mbalimbali na kuendelea kuendekeza mcjezo ule ule wa nani amfunge paka kengele
  • VODACOM Wamebip wamepigiwa rasmi na watanzania wasiopenda dhihaka - Dhambi na Mzimu huu utawaandama kwa Muda, ni dhahiri sasa Bundi anatweta VODA.
  • Mjadala wa TANZANIA WE WANT Nao waahirishwa na hautafanyika tena katika Ukumbi wa MOVEN Pick kama ilivyotangazwa. Nimezungumza na mmoja wa waandaaji kanihakikishia kuwa wamekwishapeleka ujumbe kwa wahusika Star TV ili kuutangazia Umma kuwa wamefikia uamuzi huo kwa kuwa sehemu ya wazungumzaji walikuwa na kutoka Zanzibar na haitakuwa Busara kujadili Muungano huku wenzetu wanakabiliwa na msiba Mkubwa kama huo.
  • Bado tutayasikia mengi baada ya kadhia hii, hebu tuambie huko ulipo Nini hasa kinajiri.

ADIOS
 
0 Reactions
Reply
Top Bottom