Fedheha iliyonikuta ukweni nafikiria kutokanyaga tena

Naona watu wanahangaika kumsimanga kubwa jinga mzee wa pumba wanasahau kulielewa jina lake na avatar yake
 
Kweli.. wewe kubwa jinga... wasaidie na kuzika.. teh teh teh
 
Ikubali hali yako wajibika msibani kama kwenu usiweke mawazo upon ukweni.Usiache kufika hapo hata kama hali kiuchumi itakuwa mbaya kiasi gani.Fanya shughuli zako kwa bidii zote huku ukimwomba Sana Mola wetu mlezi akubariki.
 
shida ni pale mnapokataa kukubali uhalisia wa maisha
taka usitake mwenye maisha ya juu ndie anae angaliwa hasa kwa familia zetu za kibongo

nijuavyo wala usinung'unike manake Mungu yupo na anaona na maisha ni folen siku zote.
wa kwanza atakuwa wa mwisho
 
Pole sana mkuu. Hiyo kweli ni fedhea.

Learn to let go. Japo ni process ngumu na inayochukua mda,ila jitahidi kupotezea tu.

Or unaweza ukaongea na mkeo kuhusu ilo swala just kuclear air.
 
wanajukwaa

leo hii mpaka naandika ujumbe huu nina huzuni na kitu kinachoma kama mkuki moyoni mwangu,
Hapa nilipo nipo kwenye msibwa takribani siku ya tano upande wa mke wangu yaani ukweni

Hapa nyumbani mke wangu ni mkubwa ana wadogo zake wawili mmoja ameolewa na mmoja anasoma chuo

Sasa balaa ni ile siku ya msiba tulipanda gari kuelekea msibani mimi na mke wangu kwakua kipato si kizuri niliona sina budi kuwahi mapema

Nilipofika pale msibani kama dakika tano yule mdogo wake na mke wangu wakaingia yeye na mume wake na gari nzuri ya kisasa dah mapokezi yao kama wafalme kiasi kulikuwa na mzee alimpisha kwenye kiti yule bwana ili hali mimi nilichukua mwenyewe mkeka

Baada ya pale mwenzangu alianza kuitwa kila kona chemba,niliwasikia wazee wakimuta baba njoo tupange mipango,baada ya hapo niliambiwa nichukue toroli nikakodi majamvi na maturubai na shemeji zangu

baada ya hapo shughuli zimeendelea leo ndio nimemalizwa kuambiwa nikafuate kuni nisaidiane na wapishi,

Yule bwana mdogo yupo na amezunguukwa na wazee na watoto wa mwenzangu wapo mapajani kwa bibi nahisi mke wangu pia amehisi kitu

Kila nikivuta picha kuna siku mama mkwe alikuja kumwangalia mke wangu alikua amejifungua akajamba mbele yangu nikaondoka kwa kujua ni kibinadamu ushuzi ulimponnyoka tu

Lakini leo nimeprove ule ushuzi ulikuwa na maana gani
kumbe leo nimeamini si lolote si chochote mimi ni ushuzi tu

uamuzi niliofikia nisikanyage tena pale ukweni kwa fedheha iliyonikuta aibu

ushauri wenye kujenga la kakini dah kama nimepigwa mkuki moyoni

assanteni
mmmmmmmmmh hii imetungwa hapa hapa.
 
nimechekea kama mazuri lkn si kitu cha kucheka. Kweli ni fedheha! Hizo hasira uzitumie kujiongezea kipato.
 
Pambana,ikiwa una lalamika tuu haisaidi,jitume trust me ukiwa busy na kutafuta pesa hutoona hivi vijimambo sababu utakua busy na kuangalia mambo yako...........
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom