Fedheha iliyonikuta ukweni nafikiria kutokanyaga tena

Polee bt hakuna wa kumlaumu hapo cha msingi tu we tafuta hela mwenye hela sikuzote ndo mwenye thamani mbele za watu
 
Nimecheka sana ila pia ka huzuni kwa mbali. hapo sasa ubadilike akili yako iwe kubwa kutafta na cyo KUBWA JINGA
 
Kama vipi mwambie mama mkwe, Magufuli amefanya maisha yawe magumu
b03a3ebbed19354611c0422689c23782.jpg
 
Pole kaka wengi kuangalia unanini nakumbuka nilikaribishwa kwa mchumba angu mala ya kwanza Sweden aliumwa dada ake mchumba angu nilivyoenda odini kumdalimia ndugu nilitolewa balu utadhani mimi ndo mtoa roho pole sana kaka.
Duu. Pole sana Mkuu...enhe, ikawaje? Ulikomaa hadi ukaweka ndani au ulisepa mazima?
 
Maadam wewe na mkeo mwapendana achana na hao wanao kuona wewe lofa na kukudharau....uko siku watakusalimia kwa heshima....
 
Ahaaa pole sana hivi kabila gani hilo mkwe anafata kuni msibani?

Kwakweli nimeshindwa kusikitika,

ningekuwa mkeo tukimaliza kuzika tu tunaaga mtoto anaumwa.

Hivi niende na mpz au mme wangu nyumbani chochote kimtokee, yaan watajuta kuzaliwa.
 
wanajukwaa

leo hii mpaka naandika ujumbe huu nina huzuni na kitu kinachoma kama mkuki moyoni mwangu,
Hapa nilipo nipo kwenye msibwa takribani siku ya tano upande wa mke wangu yaani ukweni

Hapa nyumbani mke wangu ni mkubwa ana wadogo zake wawili mmoja ameolewa na mmoja anasoma chuo

Sasa balaa ni ile siku ya msiba tulipanda gari kuelekea msibani mimi na mke wangu kwakua kipato si kizuri niliona sina budi kuwahi mapema

Nilipofika pale msibani kama dakika tano yule mdogo wake na mke wangu wakaingia yeye na mume wake na gari nzuri ya kisasa dah mapokezi yao kama wafalme kiasi kulikuwa na mzee alimpisha kwenye kiti yule bwana ili hali mimi nilichukua mwenyewe mkeka

Baada ya pale mwenzangu alianza kuitwa kila kona chemba,niliwasikia wazee wakimuta baba njoo tupange mipango,baada ya hapo niliambiwa nichukue toroli nikakodi majamvi na maturubai na shemeji zangu

baada ya hapo shughuli zimeendelea leo ndio nimemalizwa kuambiwa nikafuate kuni nisaidiane na wapishi,

Yule bwana mdogo yupo na amezunguukwa na wazee na watoto wa mwenzangu wapo mapajani kwa bibi nahisi mke wangu pia amehisi kitu

Kila nikivuta picha kuna siku mama mkwe alikuja kumwangalia mke wangu alikua amejifungua akajamba mbele yangu nikaondoka kwa kujua ni kibinadamu ushuzi ulimponnyoka tu

Lakini leo nimeprove ule ushuzi ulikuwa na maana gani
kumbe leo nimeamini si lolote si chochote mimi ni ushuzi tu

uamuzi niliofikia nisikanyage tena pale ukweni kwa fedheha iliyonikuta aibu

ushauri wenye kujenga la kakini dah kama nimepigwa mkuki moyoni

assanteni



uamuzi mzuri sio kukimbia ukweni nikutafuta pesa tu
 
Kwahiyo ishu iliyokuuuma ni mama mkwe kujamba msibani au kuna kingine..?
Pigana kiume , mtoto wa kiume hutakiwi kuwa nyoro nyoro .
Yaani wewe umeoa na kuwa na mke wako na mji wako lakini bado hujiamini..??
aisee, mkuu , wewe lazima una shida mahala beyond stigmatization point uliyo ilelezea hapo kwa uzi wako.
 
Take it as a challenge, simama imara pigana tafuta hela na wewe! Mpaka kieleweke!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom