Fedha zilimwagwa kumng'oa Askofu Malasusa KKKT................... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Fedha zilimwagwa kumng'oa Askofu Malasusa KKKT...................

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Rutashubanyuma, Dec 9, 2010.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Dec 9, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,305
  Likes Received: 418,551
  Trophy Points: 280
  Fedha zilimwagwa kumng'oa Askofu Malasusa KKKT
  Wednesday, 08 December 2010 20:21 0diggsdigg

  Mwandishi Wetu
  MBINU chafu za kutumia fedha kurubuni wajumbe ili wafanye mapinduzi zimeelezwa kuwa zilitumika bila mafanikio kwenye mkutano mkuu wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani (DMP)ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) ili kumng'oa Askofu Alex Malasusa.

  Fedha hizo zinadaiwa kutolewa na wanasiasa wenye fedha ambao mipango yao ni kujenga mitandao kwa ajili ya uchaguzi mkuu 2015.

  Hata hivyo, Askofu Malasusa, ambaye pia ni mkuu wa KKKT nchini, alifanikiwa kuendelea kuongoza dayosisi hiyo baada ya kushinda kwa kishindo kwenye kura ya maoni iliyopigwa mwanzoni mwa mkutano huo wa DMP.
  Viongozi wa DMP hawakutaka jana kuzungumzia suala hilo wala tofauti zilizoibuka kwenye mkutano huo unaomalizika leo mjini Bagamoyo, lakini Katibu Mkuu wa dayosisi hiyo anayeshughulikia utawala na utumishi, Ernest William alisema kikundi kidogo cha watu kilitaka kuvuruga dayosisi hiyo na ndio maana kilitoa habari hizo wakati wa kuelekea mkutano mkuu.

  Lakini akabainisha kuwa idadi kubwa ya kura iliyotaka Askofu Malasusa aendelea kuiongoza DMP ni uthibitisho tosha kuwa kiongozi huyo amefanya kazi kubwa na inayokubalika.
  “Mtu ukisemwa vibaya ujue ndio unafanya vizuri. Kwanza maneno haya yameibuka wakati tunaelekea katika uchaguzi, hii inaonyesha wazi kuwa ni uvumi tu ulioibuliwa na watu fulani,” alisema mchungaji William.

  Baadhi ya watu walio kwenye mkutano huo waliiambia Mwananchi kuwa kuna fedha nyingi zilimwagwa kwa ajili ya kufanya mapinduzi hayo, lakini njama hizo ziligundulika mapema ndipo wajumbe walipolazimisha kufanyika kwa mabadiliko ya ratiba ili ajenda ya kupiga kura ya imani kwa Askofu Malasusa iendeshwe mwanzoni.

  Awali hoja hiyo ilipingwa na ikatakiwa mkutano uendeshwe kama ulivyopangwa hadi mjumbe mmoja alipoibuka na hoja kuwa kupiga kura ni muhimu ili kuondoa wasiwasi kwa mwenyekiti, ambaye ni Askofu Malasusa na wajumbe baada ya barua kusambazwa kwenye sharika zote kumsafisha kiongozi huyo Jumapili iliyopita.

  "Hali ilikuwa ngumu na kama uchaguzi ungefanyika mwishoni, watu wangeweza kubadilishwa kabisa msimamo," alisema mmoja wa wajumbe wa mkutano huo.
  Habari zinadai kuwa baada ya kuafikiana kupiga kura ya maoni mwanzoni mwa mkutano juzi, karatasi za kura zilianza kuandaliwa lakini mjumbe mwingine akaibuka na kutoa hoja kwamba upigaji kura usiwe wa siri.

  "Sisi ni Wakristo na mambo yetu tunaendesha kwenye nuru, kwa hiyo hakuna sababu ya kupiga kura za siri," mjumbe huyo alimnukuu mtoaji hoja ambaye alishangiliwa na kupitishwa uamuzi huo uliomfanya Askofu Malasusa athibitishwe kwa asilimia 96.6 ya kura kuendelea kuiongoza dayosisi hiyo hadi atakapostaafu utumishi wa kanisa.

  Habari za kufukuta kwa mgogoro huo ziliwekwa bayana wakati msaidizi wa askofu wa DMP, Mchungaji George Fupe alipowaeleza waandishi Novemba 23 kuwa kuna kikundi cha watu wanaojiita waumini wa kanisa hilo ambao alidai kuwa walikuwa wakifanya njama za kuhujumu mkutano huo kwa kutumia magazeti.
  Mchungaji Fupe alieleza, hata hivyo, kuwa kanisa halijatikiswa na njama hizo na kwamba litaendelea na mkutano wake kama ulivyopangwa.
   
 2. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #2
  Dec 9, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Yaani mpaka kwa kanisa wanaanza kutumia rushwa kheri RC ambao jina linatoka ROME
   
 3. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #3
  Dec 9, 2010
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Sitashangaa kama Jina la Mluteri Edward L halijajitokeza katika sakata hili.
  Tamaa ya pesa na madaraka inapompofua mtu hata uwezo wa Mungu hauoni.
   
 4. L

  Lorah JF-Expert Member

  #4
  Dec 9, 2010
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 1,193
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0


  ni kwamba shetani yuko kila mahali na anataka kuitawala dunia ole wenu mtakaomruhusu awatumie katika tamaa zenu
   
 5. WiseLady

  WiseLady JF-Expert Member

  #5
  Dec 9, 2010
  Joined: Jan 22, 2010
  Messages: 3,248
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Yezebel at work!
   
 6. N

  Ndinani JF-Expert Member

  #6
  Dec 9, 2010
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 5,413
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Inawezekana Lowassa na kundi lake hawafurahi Askofu Malasusa anapokemea ufisadi nchini; ndio maana wameanza kuja na mbinu za kutaka kuyachafua madhehebu yenye ushawishi mkubwa katika jamii!!
   
 7. Young Tanzanian

  Young Tanzanian JF-Expert Member

  #7
  Nov 15, 2013
  Joined: Mar 10, 2012
  Messages: 1,740
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  mtasema sana mungu mkubwa malasusa na lowasa ni marafki wakubwa ata mbnu za kumhujumu aliyezizuia ni mtandao wa lowasa
   
 8. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #8
  Nov 15, 2013
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,434
  Likes Received: 19,774
  Trophy Points: 280
 9. amu

  amu JF-Expert Member

  #9
  Nov 15, 2013
  Joined: Aug 8, 2012
  Messages: 7,979
  Likes Received: 157
  Trophy Points: 160
  mashujaa band
   
 10. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #10
  Nov 15, 2013
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,520
  Likes Received: 1,691
  Trophy Points: 280
  Kwa nini hii thread imerudishwa tena hapa jamvini leo?
   
 11. muhomakilo jr

  muhomakilo jr JF-Expert Member

  #11
  Nov 15, 2013
  Joined: Jul 28, 2013
  Messages: 10,130
  Likes Received: 3,233
  Trophy Points: 280
  Huyu jamaa Lowasa yupo kila angle duu,kama mchezaji wa mpira ni midfied kisheti, lakini watanzania hatudanganyiki.
   
 12. mzaramo

  mzaramo JF-Expert Member

  #12
  Nov 15, 2013
  Joined: Sep 4, 2006
  Messages: 6,273
  Likes Received: 4,278
  Trophy Points: 280
  dini mmegeuza biashara
   
 13. 1000 digits

  1000 digits JF-Expert Member

  #13
  Nov 16, 2013
  Joined: Oct 16, 2012
  Messages: 2,751
  Likes Received: 1,293
  Trophy Points: 280
  Hilo tukio mbona ni la muda mrefu. Na kwanini kila jambo baya anahusishwa lowasa ! Itafikia mahali hata mtu akinyimwa unyumba na mke wake atasema kuna mkono wa lowasa!
   
Loading...