Fedha za SHIMIWI zimeenda kwenye uchaguzi?

Boramaisha

JF-Expert Member
Apr 29, 2009
820
18
Baadhi ya watumishi wa Serikali wamekuwa wakilalamika kwamba wamepoteza muda mwingi kufanya mazoezi ya kujitayarisha na mashindano ya kila mwaka ya Wizara na Idara za Serikali - SHIMIWI lakini ghafla wametangaziwa kwamba SHIMIWI haipo mwaka huu.

Je, kuna sababu gani ya kutofanyika mashindano hayo mwaka huu? Je, yawezekana fedha za kuendesha mashindano hayo hazipo kwa kuwa zimeingizwa kwenye matumizi ya Uchaguzi? Kama hivyo ndivyo watumishi hawa wa Serikali na Idara zake wategemee nini baada ya uchaguzi kwisha? Ni dhahiri kuna hatari kwamba hata mishahara wataweza kuikosa maana fedha zitakuwa zimetumika kwenye gharama za kuitafutia Serikali iliyo madarakani ushindi kwenye Uchaguzi mwezi ujao!

Wenye kujua sababu za kutokuwepo SHIMIWI mwaka huu tunaomba watueleze.
 
serikali haina fedha, zinagharamia siasa hasa kampeni ya CCM, lakini pia CCM haiitaji kura zenu wafanyikazi so hakuna haja ya SHIMIWI.
 
Serikali yenu imehofia kwamba kundi kubwa la wafanyakazi wapatao elfu tatu nchi nzima kukusanyika pamoj
a kwa wakati huu huenda wakaanzisha move mpya against serikali, wajameni wafanyakazi amkeni sasa ili
muinyime serikali hii kura mwezi ujao!
 
Wafanywa kazi wa serikali ya CCM mtakuwa mnalialia tu....maana mnapenda kudanganywa. Pesa za SHIMIWI zimeenda kwenye nyongeza za mishara yenu mliopewa kama hongo.
 
Raisi wenu wafanyakazi (JK) amekwisha watangazia nyongeza hadharani bila kupitishwa na bunge mkasema sawa! lakini hili mmeona noma kivipi au ndo mlikuwa mkijipatia fedha ya kusomeshea watoto wenu?
 
niseme moja nililojuzwa kwa mtiririko ufuatao..

Baada ya serikali kung'amua kuwa fedha yoote ya matumizi ya kawaida haipo pale hazina na walipogundua kuwa hawawezi hata kuendesha kazi za kawaida za kiutawala za serikali nzima, ikapasa waondoe shughuli walizoamini kuwa sio za msingi wala zamaanal.
SHIMIWI ikawa muhanga wa mambo hayo.
Ila nijuacho mie , baada ya barua ya siri kutumwa kwa Ndugu mmoja anaitwa Sululu, sijui nafasi yake ndani ya SHIMIWI, aliombwa akubali kwa moyo mmoja na tena kimyakimya kuwa michezo hiyo inaahirishwa kwa ukosefu wa pesa ila atangaze kuwa hali hiyo inasababishwa na mahitaji ya wafanyakazi kushiiki kampeni vituoni mwao,....ieleweke kwamba hofu ni kuwataka washiriki kampeni kwenye maeneo ya waliyo jiandikishia, ili waweze kuwa na uchaguzi sahihi hapo oct,31.
Sululu akatoa taarifa ya awali kwenda kwa katibu mkuu na mwenyekiti Tughe akiwaomba wakubali matakwa ya serikali kuu juu ya hilo, viongozi wa TUGHE WAKAWASILIANA na viongozi wa serikali, katika hali ya ajabu na Usaliti kwa TUCTA , jamaa wakatoa Ushauri kuwa huu ndio utakua wakati mzuri kwa Kikwete (Mgombea Urais) kwa tiketi ya ccm kuongea a watumishi wa umma, maana alikosa fursa hiyo pale wakati wa May Mosi. na alishauri kuwa, ni vyema akaalikwa kama mgeni rasmi either siku ya kufunga ama kufungua mashindano.
hoja ikaonekana inamashiko, lakini pesa Haziko Hazina, zimeenda wapi hapo alienijuza mkasa akasita kuendelea.
 
Labda Pesa zimeenda kwenye kampeni na nyongeza ya mishahara.
 
SHIMIWI inawapunguzia nini wafanyakazi?wao kama wanaona wamekoseshwa kitu muhimu ndio muda muafaka wa kukaa na kumfikiria kiongozi atakaye wawezesha wawe na shimiwi bila kukosa
 
Back
Top Bottom