Fedha za safari za JK zaibwa na watendaji

Kuna magazeti ya kuamini lkn sio Mwanahalisi. Udaku mtupu.
 
Maofisa watano wa wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa wamesimamishwa kazi kwa tuhuma za kuiba fedha zilizotengwa kwa ajili ya safari za raisi.
Taarifa za uhakika kutoka ndani ya ikulu na wizara hiyo zimesema kwamba maofisa hao akiwemo mkuu wa itifaki walifanikiwa kuchota 3 bilioni kutoka bank moja nchini.

Fedha hizo zilikuwa zitumike kugharamia matumizi ya safari mbalimbali za rais. Maofisa waliotajwa katika kashfa hiyo ya ufisadi ni mkuu wa itifaki Anthony Itatiro, wengine ni Shamim khalifa, kaimu mhasibu mkuu Kassim laizer, mhasibu Deltha mafie na karani wa fedha Shaban kesi.
Wote wamesimamishwa kazi yapata wiki mbili sasa kupisha uchunguzi.

Mtoa taarifa amesema "fedha hizo zimeibiwa kwa ustadi mkubwa, walikuwa wametoa fedha zote banki, sijui ilifichukaje wakati wameshapanga jinsi ya kugawana"

Taarifa nyingine zilizopatikana zilisema katibu mkuu kiongozi Balozi Ombeni sefue ameunda tume ya kuchunguza na kuipa muda wa hadi julai 4 kukamilisha uchunguzi na kumkabidhi ripoti.

Chanzo. Mwanahalisi jumatano, juni 13 - 19 uk 6.
 
Hii ni hatari wezi wameamua sasa kutafuna hicho hicho kidogo kinacho tengwa kwa ajili ya Ikulu. Sasa inabidi rais ashtuke hapa tafsiri yake ni kwamba rais ameng'atwa alikuwa amesinzia sasa inabidi aamke kukabiliana na hawa panya.

ye kang'atwa sie tunatafunwa
 
Hizo ni ndogo sana, usishangae ni salio la safari moja tu ya Brazili, hehehe wamemvurugia rekodi yake ya safari ya 328, watu wanawivu hao.
 
Ukiiba sasa wezi wengine wakajua unaiba sana, nao wanajua mchongo, watakuibia na wewe tu.
 
lazima wakwibe maana safari zenyewe za huyo wanayemtaja nazo ni za uwizi tu...bora kupiga hela na safari zisiwepo akae afanye kazi sio kutwa kuzurura kwenye nchi za watu...safi sana maafisa wezi mliosimamishwa kazi hapo wizara ya mambo ya nje...
 
ukisikia jambazi kapigwa roba na kibaka ndio hapo sasa.

Mkuu umenivunja mbavu eeeeh!

Back to the topic: Ni kwamba mkuu wa nchi alikuwa asafiri kukawa hamna pesa. Hazina walipopata pesa wakawajulisha wahusika (mambo ya nje) kuwa "jamani eee, kuna pesa hapa njooni mchukue kabla hazijaisha". Wakati huo hakukuwa na safari in hand kwahiyo wahusika wakafanya taratibu zote wakaenda wakachota hizo pesa ili wawe nazo mkononi ili ikitokea tu safari wasipate shida ya kutafuta pesa tena. Inasemekana kwamba pesa hawajazitafuna wanazo ila walitumia njia isiyo rasmi (sahihi) kuziomba huko Hazina.
 
Back
Top Bottom