Fedha za safari za JK zaibwa
MAOFISA watano wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, wamesimamishwa kazi kwa tuhuma za kuiba fedha zilizotengwa "kwa ajili ya safari za rais," MwanaHALISI limeelezwa"
........................................................................
Source: Gazeti la Mwanahalisi:
IKulu leo ama kesho itakuja na waraka kukanusha haya madai
ukisikia jambazi kapigwa roba na kibaka ndio hapo sasa.
Fedha za safari za JK zaibwa
MAOFISA watano wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, wamesimamishwa kazi kwa tuhuma za kuiba fedha zilizotengwa kwa ajili ya safari za rais, MwanaHALISI limeelezwa.
Taarifa za uhakika zilizopatikana ndani ya ikulu na wizara hiyo, zimesema kwamba maofisa hao, akiwemo Mkuu wa Itifaki, walifanikiwa kuchota Sh. 3 bilioni kutoka benki moja nchini.
........................................................................
Source: Gazeti la Mwanahalisi:
kaka kweli JF burudani tosha.. nimecheka mpaka mbavu zinataka kukatika... Jambazi kapigwa roba na kibaka.... kweli hii kali... Ngoma draw...
Sio mchezo mkuu hata wao wanaona jinsi 'VASCO DA GAMMA' anavyozichota hadi wanapata hasira.
Taarifa zinasema walisimamishwa kazi wiki mbili zilizopita, but kati ya hao waliosimamishwa kuna ambao wapo Nje ya nchi (Brazil) kikazi mpaka sasa. Kuna haja ya kujua namna transaction ya kutoa fedha za matumizi serikalini inavyofanyika coz haiwezekani Katibu wa wizara asijue dili kama hilo! Si ajabu hata TAKUKURU wamepata taarifa hizi kupitia Mwanahalisi!
ukisikia jambazi kapigwa roba na kibaka ndio hapo sasa.
Hii ni hatari wezi wameamua sasa kutafuna hicho hicho kidogo kinacho tengwa kwa ajili ya Ikulu. Sasa inabidi rais ashtuke hapa tafsiri yake ni kwamba rais ameng'atwa alikuwa amesinzia sasa inabidi aamke kukabiliana na hawa panya.