Fedha "za ndani" zinazojenga miradi ni hizi hizi Bil. 700?

Guus

JF-Expert Member
Jul 16, 2013
1,130
823
Wakuu habarini,

Nipo najiuliza maswali mawili matatu, lakini sioni kama halmashauri ya ubongo inanipa majibu ya kueleweka. Naona ni heri niweke hapa jukwaani naweza kupata machache ya kuniongoza kupata majibu.

Ni kuwa: nilikuwa nafuatilia ripoti ya kamati ya wizara ya fedha bungeni. Katika maelezo yaliyotolewa, ilibainishwa kuwa bajeti ya mwaka unaoisha (iliyopitishwa mwaka jana) ilikuwa ni trilioni 11 bilioni 881 na ushee. Kati ya hizo, trilioni 11 bilioni 157 na ushee zilikuwa ni za matumizi ya kawaida (mfano kulipa madeni na mishahara), na inayobaki hapo (kama bilioni 700 hivi) ndizo za maendelo.

Haraka haraka, nikajiuliza hizi bilioni 700 ndizo kila wakati tunatajiwa miradi tofauti tofauti kuwa tunaitekeleza kwa fedha zetu za ndani, lakini kama haitoshi, ripoti ikaendelea kusomwa kuwa hadi mwezi wa tatu mwaka huu, wizara ya fedha ilikuwa imekwishapokea trilioni 7 bilioni 648 na ushee.

Vilevile, kati ya hizo trilioni 7 bilioni 639 na ushee ni za matumizi ya kawaida (kwa lugha nyingine, fedha za maendeleo zilizotolewa kwa mwaka huu ni bilioni 8 hivi tu). Hapa ndiyo wakanikoroga kabisa. Kuna SGR na Stiglers kwa mfano wa miradi miwili tu (tuwache manunuzi mengine tunayoyafanya) tunayoambiwa tunaitekeleza kwa fedha zetu.

Je, ni hizi bilioni 8? SGR pekee kwa "phase I" ya DSM-Morogoro inagharimu zaidi ya Trilioni 3 (sio bilioni). Sasa wakuu hizi fedha zetu za ndani zinazofanya makubwa haya ni zipi? Kuna miradi ya maji pia nilimsikia Prof. Mkumbo TBC naye akisema imetumia mabilioni ya fedha zetu za ndani? Ni hizihizi bilioni 8? Wajamani tuwekane sawa kwenye hili la fedha za ndani.
 
Huyo ndio Magufuli, nchi inapaa kiuchumi kuelekea uchumi wa kati.

Hiyo miradi ikikamilika tutapiga Hatua kubwa
 
Duh, kweli huelewi. Hata ulichoandika hakieleweki. Ndio maana mpaka sasa haujatokea msaada.
 
Ili uelewe tunayoambiwa unapaswa kutofikiri mara mbili mbili yaani wewe ni kupokea na kuanza kushangilia haswaa kama mataga.au lazima ujiwekee akili kama ya Bia yetu (joke),vinginevyo ni ngumu kuelewa na nasikia kadeni ka taifa kanazidi kuvimba na hatujui anayekavimbisha nani.
 
Back
Top Bottom