Fedha za misaada za wanasiasa ni rushwa majimboni-hupumbaza wapiga kura hazina maana

Mkwawa

JF-Expert Member
Jun 8, 2011
1,334
1,464
Huu utaratibu wa Wanasiasa , wabunge ,mawaziri, madiwani kugawa vitu majimboni kama kusaidia jimbo kweli utatusaidia kuendelea. Kwanini badala ya wao kugeuka kuwa waitisha haramebee, wasisimamie kodi zetu ipasavyo ambazo ndizo zinatakiwa kutuo huduma bora za barabara, maji, elimu, afya, nk?

Je si kazi zao kama viongozi kuwa wabunifu wa vyanzo vya mapato, ajira, na huduma bora za jamii? Kweli kwa kutoa michango ya milioni moja, au mbili bila mikakati ya ukweli ya maendeleo si rushwa tu hizi?

Tukiwapima kwa michango yao binafsi tutajimaliza wenyewe. Ndio maana leo wanasiasa wenye fedha hawasumbuki wanasubiria sikukuu wanunulie watu soda, wachinje ng'ombe watu wale ukifika uchaguzi anawakumbusha soda na nyama mnasahau mambo muhimu. Sioni umuhimu wa wanasiasa kuchangisha fedha zao na kusema wanasaidia maendeleo ya jimbo. Kazi yao kubwa ni kuhakikisha vyanzo vya fedha na ajira na kodi vinapatikana na matumizi ya kodi na mipango ya maendeleo inatimizwa. Usimamizi mzuri wa bajeti na kuwafahamisha wananchi ni kiasi gani jimbo, kata inapata na itafanya nini.
Michango ya rejareja ni rushwa na upofu.
 
Back
Top Bottom