peno hasegawa
JF-Expert Member
- Feb 24, 2016
- 12,818
- 21,419
Mbunge wa Jimbo la Hai, unaulizwa Fedha Za mfuko wa jimbo kwa Jimbo la Hai zimeweza kusaidia shughuli gani tangu 2020 hadi 2022?
Kuna kila dalili fedha hizo wanalamba asali wachache.
Miaka ya 2015-2020 fedha hizo zilioneka jimboni na Kufanya shughuli muhimu ila kwa sasa mbunge anajengea nyumba yake ya kuishi.
CCM ni janga la kitaifa.
######
Mbunge atoa ufafanuzi kuhusu madai hayo[/B]
Akijibu taarifa hizo, Mbunge wa Jimbo la Hai, Saashisha Mafuwe amekanusha uwepo wa madai hayo ya matumizi mabaya ya Fedha za Mfuko wa Jimbo akieleza hakuna ukweli katika suala hilo.
Anasema “Fedha hizo zipo kwa mujibu wa Sheria, haziingii kwenye akaunti ya Mbunge kama wengi wanavyodhani, zinaingia katika akaunti ya Mkurugenzi wa Halmashauri.
"Zikiingia Mkurugenzi anamtaarifu Mbunge kama Mwenyekiti wa Mfuko wa Jimbo ambaye anaitisha kikao kwa ajili ya maelekezo, fedha hizo zinaenda kwenye miradi ya Serikali.
“Mimi huwa huwa ninaita Madiwani tunajadili kuhusu miradi na kuidhinisha, lakini wanaonunua, wanaosambaza, wanaosimamia ni Halmashauri na siyo mimi Mbunge.”
Amesema Mkurugenzi wa Halmashauri anaweza elezea zaidi kuhusu fedha hizo kwa kuwa ndiye anayezipokea kupita akaunti yake.
Ametaja Wajumbe wa Mfuko wa Jimbo kuwa ni:
1. Saashisha E Mafuwe (Mb)- Mwenyekiti
2. Leonard Luhwavi - Mkuu wa Idara ya Mipango, Takwimu na uratibu -Katibu.
3. Judica J. Munisi - Diwani wa Machane Kaskazin -Mjumbe
4. Zanika A. Mushi Diwani V/Maalum-Mjumbe.
5. Hellen J. Munuo- Mtendaji Kata ya Muungano-Mjumbe.
6. Andrew E. Msuya - Mtendaji Kata ya Masama Mashar - Mjumbe.
7. Asifiwe James Malya - Mwakilishi kutoka NGO