Fedha za kutatua tatizo la umeme zitapatikana kwa njia hii...

Maxence Melo

JF Founder
Feb 10, 2006
4,230
13,415
yav_logo.gif

Tatizo la uhaba wa umeme linasukuma kushuka kwa uzalishaji wa ndani na kusababisha upotevu wa ajira. Hali hii inaweza kusababisha machafuko ya kijamii kama haitapatiwa ufumbuzi wa haraka. Wakati ikijitahidi kupunguza matumizi yasiyo ya lazima na kutafuta njia mbadala ya kutenga bajeti yake kwa ajili ya kushughulikia matatizo ya umeme yanayoendelea, Sikika inatoa pendekezo kwa kufafanua ni jinsi gani malengo yanaweza kufanikiwa kwa pamoja.

Serikali kwa mara nyingi imekuwa inakiri kuwepo kwa matumizi yasiyo ya lazima na kuahidi kuyapunguza.

"Serikali itaendelea na jitihada zake za kudhibiti matumizi kwa kuahirisha ununuzi wa kila aina ya magari [...]; kupunguza malipo ya posho mbalimbali, kukata gharama za mafuta kwa magari ya serikali, kupunguza idadi ya safari za ndani na nje, [...] na kuendelea kuhakikisha kwamba semina na warsha zinaondolewa na kama ni za muhimu basi ni lazima ziidhinishwe na Ofisi ya Waziri Mkuu, "alisema Waziri wa Fedha, Mheshimiwa M. Mkulo, tarehe 8 Juni 2011

Leo hii, jumla ya makadirio ya matumizi ya vitu visivyo vya lazima ni shilingi za kitanzania bilioni 568 ingawa wadau wa ndani na wahisani wamekuwa wakionyeshawasiwasi wao kuhusu kuendelea kwa tatizo la matumizi yasiyo ya lazima.

Kwa hisani ya SIKIKA

Zaidi download attachment hii ndogo yenye mapendekezo ya wapi papunguzwe fedha, kiasi gani n.k
 
Attachments

  • Swahili version.pdf
    335.2 KB · Views: 166
These guys are not serious

Kwanza wangeleta mchanganuo mzima wa matumizi yaso ya lazima ya kila wizara then wangeleta figures sio kutuletea namba bila kueleza nini na nini kinapunguzwa.

That said, sikubaliani nao kwenye kuwaondolea AFYA, ELIMU na huduma za jamii ili hali wao wanaendelea kupeta na VX

pia ningependa kujua IKULU iweje wakawa na bajeti ndogo hivyo wakati kila kukicha Bosi yuko nje ya nchi?
 
Serikali ilivyo sikivu haitayazingatia mapendekezo haya mazuri ya sikika. Serikali ni sikivu kwa wajinga na si welevu kama sikika na haki elimu.
 
Mie sina Muda wa kuwasikiliza Magamba na timu yao ya uongo, nasubiria Maandamano ya kumtoa Fisadi Papa Kikwete ndio nitashiriki na hata kama kujitoa muhanga kwa ajili ya Kizazi kijao itafanya hivyo.

Invisible umegonga LIKE kwa Bosi wako sio?
 
Mkuu Maxence kwahiyo nikishagonga hiyo link halafu nikasoma hiyo habari natakiwa kurudi tena hapa kutoa maoni au inakuwaje hii?
 
Mkuu haya matumizi yasikuwa ya lazima ni yapi tena. Matumizi ambayo si ya lazima kwa nini yawepo kwenye budget?
 
Mie sina Muda wa kuwasikiliza Magamba na timu yao ya uongo, nasubiria Maandamano ya kumtoa Fisadi Papa Kikwete ndio nitashiriki na hata kama kujitoa muhanga kwa ajili ya Kizazi kijao itafanya hivyo.

Invisible umegonga LIKE kwa Bosi wako sio?

Mkuu kujitoa muhanga ni kazi!!!
 
mbona kamgongea Muhosini hapo juu, hujaona?
 
Mkuu kujitoa muhanga ni kazi!!!
hasa hasa waarabu ndio wanaweza hii kitu.. hakuan mmbongo anayeweza.. si unakumbuka mnaijeria pamoja na malecture yote aliyopata hadi alipelekwa YEMEN lakini siku ya siku akaona miyeyusho kujilipua .. akaone aendelee kula bata duniani tu.
 
Sikika ndio kina nani?

NGO, wapiganaji. Nadani watu wanachangia bila hata kuelewa wanachochangia, hawa wanatoa mapendekezo wapi kuna fedha zilizowekwa kwenye bajeti ambazo si matumizi ya lazima kuwa yanaweza kupunguzwa kwa ajili ya matumizi ya urgent kama Umeme.

Sasa sijui kama tatizo la umeme ni la gent kwa serikali hii au la!
 
wana uhakika watasikilizwa? ujue kwenye hii serikali yetu mara nyingi huwa tunampigiaga mbuzi gitaa.i hope itakuwa sio kupiga gitaa
 
NGO, wapiganaji. Nadani watu wanachangia bila hata kuelewa wanachochangia, hawa wanatoa mapendekezo wapi kuna fedha zilizowekwa kwenye bajeti ambazo si matumizi ya lazima kuwa yanaweza kupunguzwa kwa ajili ya matumizi ya urgent kama Umeme.

Sasa sijui kama tatizo la umeme ni la gent kwa serikali hii au la!

Sasa mkuu hayo matumizi yasiyo ya lazima ambayo yamewekwa kwenye budget ni yepi? Manake mimi naona figure tu bila kuonyesha kwamba hayo matumizi ni kama yapi. Kwa mfano Vote 99 kuna 6.7 billion ambazo ni pesa za matumizi yasiyo ya lazima sasa mimi sijaelewa hayo ni matumizi gani kwa mfano. Kwa maana nyingine wangetusaidia kwa kuweka mchanganuo wa matumizi yasiyo ya lazima na si kubandika tu figures.
 
Mkuu Kimbunga, naona kwenye website yao kupitia hiyo link hapo juu kuna doc ya Kiingereza inajibu maswali yako. Bofya Hapa please http://www.sikika.or.tz/yavworks/Analytical works/Cutting Down Unneccessary Expenditures.pdf Inaonekana wamekusanya posho, safari, semina, n.k
 
wakuu naona mnataka kunilaza njaa mimi biashara yangu ni vifaa vya umeme wa jua na majenereta
 
Sasa mkuu hayo matumizi yasiyo ya lazima ambayo yamewekwa kwenye budget ni yepi? Manake mimi naona figure tu bila kuonyesha kwamba hayo matumizi ni kama yapi. Kwa mfano Vote 99 kuna 6.7 billion ambazo ni pesa za matumizi yasiyo ya lazima sasa mimi sijaelewa hayo ni matumizi gani kwa mfano. Kwa maana nyingine wangetusaidia kwa kuweka mchanganuo wa matumizi yasiyo ya lazima na si kubandika tu figures.

Mi sijui kwanini watu hampendi kusoma na badala yake mnatafu majibu marahisi kila sehemu na kila wakati, Max ameweka hiyo taarifa hapo kuisoma hamtaki ila kuijadili ndio mnataka hii tabia itatuathiri sana Watanzani.

Hiyo proposal ipo wazi kabisa wamesema wanashauri matumizi yasiyo ya lazima yapunguzwe kutoka katika fedha zilizoainishwa kwa ajili ya: -
  1. Posho
  2. Usafiri
  3. Mafunzo
  4. Mafuta na Vilainishi
  5. Ukarimu na Manunuzi ya magari mapya
Ilizitumike kufanya agency procurement ya kutatua tatizo la Umeme, na wameonyesha kiasi cha fedha kinachoweza kupatikana kwa kukata kutoka katika hayo matumizi katika Bajeti hii inayosomwa sasa Bungeni.

Sasa kusoma hamtaki mnataka mtu wakuwasomea na kuwapa hadithi!
 
Back
Top Bottom