#COVID19 Fedha za kupambana na UVIKO19: Tenda ya Sept 29 na mwisho wa maombi Sept 30?

Mapema leo Rais Samia akiwaapisha viongozi mbalimbali ameeleza wazi kuwa hatovumilia viongozi wala RUSHWA. Hata Siku ya Jumapili wakati akizindua mpango wa Serikali wa kuinua uchumi na kukabiliana na UVIKO19 alisisitiza matumizi sahihi ya fedha za hizo huku akiwataka wasimamizi kuzingatia sheria na kanuni zote za matumizi.

Habari mbaya ni kwamba, inawezekana Wizara ya Afya ikawa wameshayakoroga maji mapema kabisa katika kutangaza tenda kwani ni dhahiri kuna watu wamekula "dili" wakapeana tenda juu kwa juu na barua ya tenda imetolewa tu kama ushahidi. Kwa mujibu wa barua hiyo (Iko hapo chini), wizara ya afya imetangaza tenda tarehe 29/09/2021. Lakini sharti la 7 inawataka waombaji wote kuwasilisha nyaraka zao halisi tarehe 30/09/2021 kabla ya saa nane mchana. Kwa lugha rahisi mwombaji anatakiwa kujaza nyaraka na kuzifikisha Dodoma katika muda chini ya masaa 24. Hii ni wazi kuna watu wamepeana dili hapa na Rais Samia anapaswa kuanza kushughulika na hawa watu mapema iwezekanavyo

View attachment 1971345

Soma ufafanuzi wa Wizara: #COVID19 - Serikali yakana kuwepo upendeleo au rushwa kwenye kampeni ya kuhamasisha chanjo
Swala si kupeana dili swala ni je watakaokuwa wamepata wataweza kuonesha ufanisi? Na hii ndio single source atakeyewahi na ana uwezo ndio hiyo atapata.
 
Swala si kupeana dili swala ni je watakaokuwa wamepata wataweza kuonesha ufanisi? Na hii ndio single source atakeyewahi na ana uwezo ndio hiyo atapata.
Kwanza ni suala sio swala, alafu unaposema kupeana dili sio suala unakiuka kanuni, sheria na taratibu za tenda na zabuni, rudi kasome tena
 
Back
Top Bottom