Fedha za DHAMANA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Fedha za DHAMANA

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mambo Jambo, Dec 1, 2008.

 1. Mambo Jambo

  Mambo Jambo JF-Expert Member

  #1
  Dec 1, 2008
  Joined: Jul 11, 2008
  Messages: 1,100
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  Heshima mbele wakuu na vigogo.

  Nina swali limekuwa lininiumiza kichwa na kunitia hofu kwa siku kadhaa sasa, wakati serikali ikiwa katika mshike-mshike huu wakuwapekeka watuhumiwa wa matosa ya fedha za akaunti za nje EPA, usimamizi mbovu wa mikataba(on progress) na utumiaji mbovu wa madaraka na n.k. Nakutozwa kiasi kikubwa cha fedha taslimu (cash) kama dhamana.

  Swali langu linakuja hivi:-

  1. Je fedha hizo zinawekwa wapi kwenye account gani?.
  2. Kwa kuwa watuhumiwa hawa wamekuwa wakitozwa kiasi kukubwa cha fedha za dhamana je hii haiwezi kupunguza kiasi cha fedha kwenye mzunguko na soko la fedha na hapo kuiweka nchi katika hali mbaya kiuchumi na kupanda kwa hali ya maisha.  MJ
   
 2. Ochu

  Ochu JF-Expert Member

  #2
  Dec 1, 2008
  Joined: May 13, 2008
  Messages: 972
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  anatoa bond ndugu na si cash kama unavyodhani.... suala la cash lilikuwa kwenye kesi ya kina mramba tu na mahakama kuu imekubali bond!!!!
   
 3. Mambo Jambo

  Mambo Jambo JF-Expert Member

  #3
  Dec 1, 2008
  Joined: Jul 11, 2008
  Messages: 1,100
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  Mkulu you mean there is no cash arrangements, unamaana ni BONDS kwenda mbele...kama ni hivyo itakuwa vizuri, lakini kama ni CASH arrangments then swali langu bado liko pale pale.
   
 4. Domo Kaya

  Domo Kaya JF-Expert Member

  #4
  Dec 1, 2008
  Joined: May 29, 2007
  Messages: 530
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Huwa wanaweka bond yenye thamani sawa ana kiasi cha fedha zilizotajwa na si fenda taslim, nadhani Kina Mramba waliamua kuwakomoa ndio wakataka cash.
   
 5. Njilembera

  Njilembera JF-Expert Member

  #5
  Dec 1, 2008
  Joined: May 10, 2008
  Messages: 1,423
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  Mkullu, ni kweli dhamana iliyodaiwa na mahakama ya Kisutu ni CASH, kesi 1162 ya kina Maranda na wafanyakaz wa BOT walidaiwa Milioni in Cash 104, na fedha hizi huwekwa kwenye account Domestic Bank ya BOT. Hakimu aliyesimamia kesi hii alitumia discreation yake kudai dhamana ya fedha taslimu na sio vinginevyo. Ni hakimu huyo huyo aliyeamua kesi ya kina Mramba, anaitwa Mwakenja au hivi
   
 6. Mambo Jambo

  Mambo Jambo JF-Expert Member

  #6
  Dec 1, 2008
  Joined: Jul 11, 2008
  Messages: 1,100
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  Hivi ndivyo sheria inavyosema au ni kila hakimu na maamuzi yake, kwa kuwa hawa walidaiwa cash before na vilevile wale wa BOT walidaiwa Cash as well, sasa kama utaratibu utakuwa wa cash badala ya bond swali langu bado liko palepale..
   
 7. K

  Kichakoro JF-Expert Member

  #7
  Dec 1, 2008
  Joined: Sep 10, 2008
  Messages: 1,548
  Likes Received: 1,307
  Trophy Points: 280

  Mkuu ni swali zuri sana

  Hizo hela zinawekwa kwenye account ya Mahakama (sina hakika mahaka kuu ama vinginevyo ambapo serikali ndio msimamizi wa hiyo hela kupitia hazina).

  Kuhusu kupunguza mzunguko wa fedha sio kweli maana zikiwa bank ni kama umeweka fixed deposit so mzunguko bado uko pale pale. Sijui interest earned inakuwa na nani????

  Mchezo ninaouona hapa ni kwamba serikali inaweza kuwa inakusanya hela kutoka vyanzo kama hivi ili kuja kuonesha kwa wananchi ni hela za EPA zilizorudi, chache zinaenda kwa wananchi(wakulima) nyingine zinazopelekwa TIB then zinazopelekwa TIB serikali inaikopa TIB tena inawarudishia kina Mramba et al pesa zao pale kesi yao inapokuwa imemalizika, Je hili haliwekani???????????
   
 8. Watu

  Watu JF-Expert Member

  #8
  Dec 1, 2008
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 3,054
  Likes Received: 427
  Trophy Points: 180
  Aliye toa cash ni Mama Komu 2, wengine wameacha hati za viwanja!
   
 9. FDR.Jr

  FDR.Jr JF-Expert Member

  #9
  Dec 1, 2008
  Joined: Jun 17, 2008
  Messages: 1,335
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  Sheria inaruhusu cash au thamani sawa na cash, ila ktk hili la maranda na mramba walikumbana na mahafidhina mahakamani. Yeye ni mkomoaji daima ila baadaye huanza kuweweseka pale anapoona alichoamuru ni ukatili zaidi kuliko sheria.

  Nadhani mramba na yonah waitumie fursa hiyo hiyo kumkataa ktk kesi maana uamuzi ule wa mahakama kuu umeonyesha kuwa kwa makusudi alipindisha sheria ili tu kuwakomoa.

  Mramba aliligundua hilo na ndio maana alimuamuru mkewe ampe ndala baada tu ya kupewa masharti licha ya kuwa mawakili na mama walitaka wamuombe hakimu palepale kuwa masharti hayo ni magumu kwao, mzee akawaambia waache na waheshimu maamuzi yake kwani yeye yuko tayari kwenda huko alikopangiwa aende, na ndivyo ilivyokuwa. Kibaya zaidi ijumaa hakimu huyo alinda b'gamoyo kwenye semina na pale alipohitajika kuhusiana na maamuzi ya mahakama kuu alizima simu yake mpaka usiku.

  Hiyo ndiyo game ya kisutu na mramba.
   
 10. A

  August JF-Expert Member

  #10
  Dec 1, 2008
  Joined: Jun 18, 2007
  Messages: 4,505
  Likes Received: 723
  Trophy Points: 280
  ukitoa bond ni sawa na cash iliyopo bank, kwani wenye kutoa hiyo bond ni bank zilipo fedha zako, alternatively ukitoa cash ndio hiyo hiyo inapelekwa bank.kwa hiyo at the end of the day fedha hizo zinakuwa bank.
   
 11. Mambo Jambo

  Mambo Jambo JF-Expert Member

  #11
  Dec 1, 2008
  Joined: Jul 11, 2008
  Messages: 1,100
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  Kwa hiyo hapa inategemea ni nani mtakaye mkuta mahakamani siku hiyo, ukimkuta mkomoaji anakukomoa, kwa hiyo kwa kifupi ni kwamba sheria juu ya BOND/CASH haipo ni zali(bahati) lako tuu...mama KOMU alitoa CASH wenzake BOND...na juzi tumeona bila mahakama kuu kutengua maamuzi nakuwapa jamaa masharti mepesi, CASH wangeitoa, hapo ndipo lilipo swali langu.
  Endapo tutawapata hawa watoa maamuzi ya CASH ONLY.
   
 12. Eeka Mangi

  Eeka Mangi JF-Expert Member

  #12
  Dec 1, 2008
  Joined: Jul 27, 2008
  Messages: 3,182
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  At the end of the day lazima fedha hizo zitawekwa benki. Mahakama ni institution kama zilivyo institution nyingine na zinafuata procedures amabazo zinagovern taasisi zote za kiserikali. Kuhusu kuwapata hawa wenye maamuzi ya CASH ONLY, ni kuwa sheria ni pana sana na mahakimu wana wigo mpna sana wa kucheza na sheria zilizopo. Hivyo akitoa maamuzi anakuwa na kipengele cha sheria kinachomlinda. Kama tulivyo wengi hatujui sheria za nchi hii, hivyo ni rahisi kwake kugonga nyundo and its done. Ukienda mahakama za juu wanasema kipengele fulani cha mwaka fulani kinaondoa nguvu ya kipengele alichotumia hakimu huyu katika shtaka hili, hata kesi za huko majuu zitatolewa mfano hapa.
   
 13. FDR.Jr

  FDR.Jr JF-Expert Member

  #13
  Dec 1, 2008
  Joined: Jun 17, 2008
  Messages: 1,335
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  Originally Posted by Mambo Jambo
  Kwa hiyo hapa inategemea ni nani mtakaye mkuta mahakamani siku hiyo, ukimkuta mkomoaji anakukomoa, kwa hiyo kwa kifupi ni kwamba sheria juu ya BOND/CASH haipo ni zali(bahati) lako tuu...mama KOMU alitoa CASH wenzake BOND...na juzi tumeona bila mahakama kuu kutengua maamuzi nakuwapa jamaa masharti mepesi, CASH wangeitoa, hapo ndipo lilipo swali langu.
  Endapo tutawapata hawa watoa maamuzi ya CASH ONLY.


  MKUU MIMI NINASISITIZA KUWA LICHA YA UWIGO HUO WALIONAO MAHAKIMU BADO WANATAKIWA KUSOMA HUKUMU MBALIMBALI ZINAZOFANANA NA KESI ILIYOPO MBELE YAKE, ANATAKIWA KUTAFAKARI BEYOND DOUBTS JUU YA KILE ATAKACHOKIAMUA, NA MENGI WA KADHAA KTK KADHIA YA NAMNA HII, MH.MWANKENJA YUKO LAW SCHOOL SASA BAADA YA KUPATA DEGREE YA SHERIA SIKU ZA USONI, KIUMRI NI HAKIMU WA SIKU NYINGI, MZOEFU NA MAJANGA YA KISHERIA TANGU ZAMA ZA KAMBARAGE, UAMUZI WAKE KTK KESI HIZI ZA EPA NA MRAMBA UNAMFANYA AONEKANE NI MKOMOAJI NA SI MSIMAMIZI NA MTAFSIRI SHERIA, SHERIA INASHAWISHI KABISA KUWA NI LAZIMA KUFANYIKE KILA LINALOWEZEKANA ILI HAKI ITENDEKE KWA PANDE ZOTE ZILIZOPO MBELE YA MAHAKAMA.

  KITENDO CHA KUWEKA MASHARTI KWA MAKUSUDI HALAFU UAMUZI WAKO UNATENGULIWA/USAHIHISHWA NA SENIOR WAKO NI UZEMBE AMBAO NDIO TUNAOUKEMEA HAPA JF, NI KUJIDHARIRISHA KUSIKO NA MAANA KWA MLINZI WA SHERIA.

  UAMUZI WA JAJI MWAIKUGILE UPO PIA KTK ILE SHERIA YA MWAKA 2002 YA DHAMANA YA MWAKA 2002 AMBAYO YEYE MWANKENJA ALICHAGUA UBETI MMOJA NA KUTUIMBISHA HUO NA KUDAI NDIO WIMBO KAMILI.

  JAJI KAMTAKA AIMBISHE NA CHORUS ILI WIMBO UKAMILIKE.

  KUNA YULE MZEE WA EPA ANASOTA MPAKA LEO, YUKO BAGA KIUCHUMI NA KAMA ALILAMBA SASA WANAMLAMBA KULE, SASA MASHARTI YA MWANKENJA YANAMSURUBU NA KUMJUTISHA HUKO ALIKO.
   
 14. Mambo Jambo

  Mambo Jambo JF-Expert Member

  #14
  Dec 1, 2008
  Joined: Jul 11, 2008
  Messages: 1,100
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  [/I]

  Mpita Njia katueleza wamerudishwa ndani na jamaa huyu huyu...removal older aliyotoa ni ya tarehe 2 Dec ya tarehe 1 Dec katoa nani...wamerudi keko.
   
 15. M

  Mwikimbi JF-Expert Member

  #15
  Dec 1, 2008
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,745
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  hakimu mwankenja tayari keshawahukumu washtakiwa hawa, nilikuwa mmoja wa watu walioenda kushughukia dhamna ya wale wafanyakazi wa bot, yeye anasema leteni hard cash pale mahakamani 104m, hata tulipokwisha kumuonya kuhusu hatari ya kutembea na 104m cash, tukamwomba tupeleke bankers draft ambayo ni sawa na cash, alikataa na kudai kuwa nyie mmezoea kubeba mabilioni mnawezaje kuogopa 104m? alipotakiwa kuandika removal order ili washtakiwa waletwe mahakamani siku ya ijumaa, (ilikuwa alhamisi tulipoomba), alikubali lakini badaye akasaini kuwa waletwe jumatatu.

  leo kama ameandika removoa order ya akinamramba iwe jumanne sishangai, ni mzee tunayemfahamu anayejifanya kuokoka huku akimaamini majungu au kuhukume watu kwa hisia tu

  ni vema watuhumiwa walio na kesi mbeke yake wajiandae kwenda jela kwa kuwa huyu anayo hukumu yao tayari

  yetu ni macho mtasikia
   
 16. K

  Kichakoro JF-Expert Member

  #16
  Dec 1, 2008
  Joined: Sep 10, 2008
  Messages: 1,548
  Likes Received: 1,307
  Trophy Points: 280

  Mwikimbi na wengine naona mnakosea

  Kwa nini mhalifu ajipangie siku wakati mahakama zina taratibu zake???????

  Unaelewa kuna kesi nyingi za kusikiliza mahakani hivyo Hakimu anayohaki ya kuangalia ni muda gani muafaka kwake na sio sisi watazamaji.

  Je na wengine ambao walikua jela kabla ya kina mramba kwa kukosa zamana nao wao wanahaki ya kuskilizwa. First In First OUt so hakuna sababu ya kumlaum huyu Hakimu BRAVO MWAKENJA KWA KUWA STRICT.
   
 17. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #17
  Dec 1, 2008
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  FdrJr na Mwikimbi,
  Sheria inauma kote.
  Hakimu anayo haki yake na mshitakiwa anayo haki yake. Nakubaliana na hukumu ya Mwankenja maana siku zote hukumu utoa uchaguzi kati ya mambo kadhaa wa kadha. Na ni uchaguzi wa hakimu mwenyewe lipi achukue na lipi aache.
  Hata Majaji si kwamba wao ndio wako right sana kisheria kuzidi mahakimu wa chini yao, maana huwa tunaona hata hukumu zao zinatenguliwa na mahakama za juu yao. Yawezeka yule jaji kawapa favour tu kwa kuwahurumia. Watu hawa wamepoteza pesa yetu nyingi wakifurahia na familia zao na baba yangu akikosa dawa hospital kwa ajili ya ujinga wao tu.
  Kwa kweli hata ningekuwa mimi ni hakimu hawa wakina Mramba, Yona, hawa watu wa EPA, watu waRichmond, Meremeta, Deepgreen nk, lazima wangesota rumande na kisha ningewalambisha miaka tu. Hasa huyu aliyekuwa anatutaka tule majani! huku kwa hakika akiiba! Lazima ningemlambisha miaka. Bahati tu mimi nilichelewa na shule ya sheria sikwenda na nikaishia kuwa mkulima wa karanga huko kwetu baada ya kumaliza form 10. Hiyo ndiyo bahati yao tu!!!!!!
   
 18. FDR.Jr

  FDR.Jr JF-Expert Member

  #18
  Dec 2, 2008
  Joined: Jun 17, 2008
  Messages: 1,335
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  anachosema mwakimbi ni 100%, mzee ni mtu aliyechanganyikiwa. Matendo yake na matamshi yake vina tofauti kubwa sana, judiciary inagawanyika kimamlaka ila mgawanyiko huo haundoi wajibu na haki za uhuru ktk maamuzi ya kisheria, mimi nilichosisitiza ni style ya u-radical wake hata pale sheria inapotoa fursa kwa mshitakiwa, mtenda haki ni lazima awe tayari kusikiliza pande zote bila kuruhusu utashi wake binafsi ktk kusikiliza na kuamua, alipowakomoa wale jamaa wa epa baadae akataka kubadilisha masharti kama alivyosema mwakimbi lakini wenzake wakamuonya kuwa hiyo hatari na kuidharirisha mahakama maana walimwambia tayari kuna watu wametoa cash kama ulivyotaka sasa huruma hii inatoka wapi sasa!! Akanywea na ndio maana yule mzee akaenda mahakama kuu, hii ya mramba na yona alipotoka tu mahakamani kama kawaida yake hutaka ku seek opinion za wenzake wote wakawa cool, akaona tayari kesharikologa akataka kubadili masharti kabla wale wazee hawajaondoka kuna mama mtu mzima pale akamuonya kuwa asithubutu maana tayari keshaipa public walichotaka na isingelikuwa salama kwake na mahakama, kwahiyo huyu si mtu makini bali ametawaliwa emotional things ktk maamuzi yake, kitendo cha jana hakikuwa cha kistaarabu kwa mahakama yenyewe, yeye ijumaa aliingia mitini na kuzima simu yake, walio juu yake wakamsurubu na kutoa maelekezo alichopaswa ni ku comply na remove order ile ile ya mahakama kuu na ku note kuwa shauri hili la zamana lilipata sura tofauti ijumaa na kwa udhuru wake siku hiyo yeye kama hakimu ameamua kuendelea na kile kilichofanyika ijumaa, lakini akaweka msimamo wa kihuni eti aonekane ni mtu thabiti ktk maamuzi yake kitu ambacho si kweli maana tayari mahakama kuu wamemtoa dosari kwa kutengua baadhi ya masharti na maamuzi yake.

  Ilitosha kwake kuanza kuonyesha kuwa naye ni mnyenyekevu na mwenye kukubali kukosolewa ktk utendaji.

  Ni hatari sana ktk sheria unapokuwa na mtu asiye makini kama huyu mzee wetu.
   
 19. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #19
  Dec 2, 2008
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,523
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  Kiutaratibu amefanya insurboordination kwa kutotii maelekezo ya seniors wake. Kinachoonekana hapa sio maamuzi ya hakimu mwenye busara bali ni uhuni, double standards na kujitafutia umaarufu from nonsense. Kama sio roho mbaya kwa nini azime simu? Dhamana ni haki ya mtu hadi hapo atakapothibishwa ana makosa .
   
 20. kinepi_nepi

  kinepi_nepi JF-Expert Member

  #20
  Dec 3, 2008
  Joined: Aug 16, 2007
  Messages: 870
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  kweli mtumishi wa umma anaweza kukusanya mali zenye thamani ya zaidi ya billion tatu????? kwa miaka arobaini???? Tanzania????
  tumeibiwa vya kutosha , Daniel ndhira Yona Umetuibia mno.
   
Loading...