Fedha yote ya Tanzania yetu ni mali ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Barbarosa

JF-Expert Member
Apr 16, 2015
22,584
27,811
Kama ilivyo ardhi yetu pia fedha yetu yote ni mali ya Tanzania chini ya usimamizi wa Rais wa JMTZ, na hapa namaanisha fedha yote ambayo Serikali inayo, na hakuna mwenye uwezo wa kuhoji wala kuzuia jinsi ambavyo Rais wa JMTZ anaamua kuitumia ni kama vile ardhi yetu, Rais wa JMTZ ana uwezo wa kuifanyia chochote na hakuna mwenye uwezo wa kuzuia, Rais wa JMTZ ana uwezo kinadharia wa kuigeuza Dar yetu yote kuwa Zoo na wakazi wote kuhamishwa ...
 
Kwenye nchi makini hata hayo mawazo kama yako hawana, mfano wa karibu kilicho mpata Rais Zuma. Chochote anachofanya Rais kinacho husisha pesa waliofanya ni wananchi, mafano yale magari waliyokabidhiwa wabunge ni kodi walizokatwa wafanyakazi, wafanyabiashara, ni pesa za mikopo ya ndani au nchi wahisani.
 
Itakuwa hajaligundua hilo bado,au hajakiona iko kipengele.akikiona tu kweli tena tunahamishwa dar unakuwa mji wa barabara na madaraja tu.anapenda miundombinu kuliko watu.
 
Gombea na wewe Uwe Rais
pia ungeongezea kuwa haya yoote hutokea kwa Muda wa Miaka 10 Pekee
 
Kwenye nchi makini hata hayo mawazo kama yako hawana, mfano wa karibu kilicho mpata Rais Zuma. Chochote anachofanya Rais kinacho husisha pesa waliofanya ni wananchi, mafano yale magari waliyokabidhiwa wabunge ni kodi walizokatwa wafanyakazi, wafanyabiashara, ni pesa za mikopo ya ndani au nchi wahisani.

Unachanganya mambo, AK siyo Tanzania, hivyo kumlinganisha Zuma na Raisi wa JMTZ ni kupotosha, haukusikiliza darasa la Waziri wetu wa Sheria Bungeni?
 
Unachanganya mambo, AK siyo Tanzania, hivyo kumlinganisha Zuma na Raisi wa JMTZ ni kupotosha, haukusikiliza darasa la Waziri wetu wa Sheria Bungeni?
Nikweli. Lakini Tanzania tunatabia moja ya kujisifu tunapofanya jambo na kufanikiwa, utasikia "katika afrika ya kati na kusini Tanzania tumekuwa wakwanza kwenye hili jambo" Je hatuwezi na sisi kuangalia huko na kujifunza ya kwamba hakuna binadamu ambaye anaweza kuwa juu ya hazina ya Taifa na kuitumia atakavyo nje ya utaratibu?.
 
Mubashara,ila kuna nyumbu makapuku ambao hawlijui hlo watapinga mpka kufa kwao
 
Nikweli. Lakini Tanzania tunatabia moja ya kujisifu tunapofanya jambo na kufanikiwa, utasikia "katika afrika ya kati na kusini Tanzania tumekuwa wakwanza kwenye hili jambo" Je hatuwezi na sisi kuangalia huko na kujifunza ya kwamba hakuna binadamu ambaye anaweza kuwa juu ya hazina ya Taifa na kuitumia atakavyo nje ya utaratibu?.

Hilo ni swala lingine, mimi naongelea hali ilivyo sasa hivi, usisahahu AK iko jinsi ilivyo kulingana na mazingira na Historia yao, siyo kila kitu kinafaa kuigwa 1-1, mambo yanayowezekan AK huwezi kuyaleta JMTZ na kinyume chake!
 
Ardhi ya mungu.pesa za wananchi.bila sisi kutoa kodi hakuna hela serikalini.

Raisi wa JMTZ anamuwakilisha Mungu, imeandikwa hata kwenye Biblia, hivyo Mungu anatawala Tanzania kupitia Raisi wa JMTZ ndiyo maana yake, na ndiyo maana Maaskofu wa Ulaya zamani walikuwa wana nguvu za Kisiasa na walikuwa wana teuliwa na Papa moja kwa moja ktk Roma, na ndiyo neno Jimbo lilipoanzia!

Wimbo wetu wa Taifa unasema Mungu Iabariki Tanzania lkn umebadilishwa tu ulikuwa unasema Mungu Mbariki Mfalme/Malkia (Uingereza) ambaye ni muwakilishi wa Mungu kwa Binadamu!
 
Back
Top Bottom