Fedha ya matumizi ya kawaida kuwa kubwa kuliko ya matumizi ya maendeleo ina maana gani?

mbwe

JF-Expert Member
Feb 23, 2018
582
1,000
Tujue kwanza hayo mambo ya kawaida ni yapi
Ukishajua utafanya Nini sasa, hujui lolote kuhusu uchumi unavyoendeshwa so kaa kimya,waza kesho watoto wako watakula Nini maana hili swala lipo juu sana kwa uwezo wako finyu wa kufikiria maana hata ukipewa mchanganuo ni matumaini yangu utatoka patupu
 

RAISI AJAYE

JF-Expert Member
Oct 29, 2019
2,454
2,000
Baada ya maumivu makali ya kiuchumi na kuzeesha watu!kama Raisi lazima niwafariji watu wangu ili warudishe Tabasamu jipya usoni!!!
 

kitowowoti

JF-Expert Member
Feb 25, 2016
377
250
kwa Pesa ya Shilingi Trilioni 1.02. kutakuwa na Maendeleo kweli? Tutamkumbuka Mzee Wetu Hayati Magu Mungu amuweke mahali pema amin.
Unajua lakini hujui, rahisi iko hivi, nchi inavyokuwa na mapato kidogo ndivyo uwiano wa matumizi ya kawaida yatakuwa. makubwa kuliko ya maendeleo. sababu matumizi ya kawaida ndani yake kuna matumizi yasiypbadilka(fixed)kuendana wingi wa Mapato.mfano kwa halmashauri Tanzania bara iwe kubwa au ndogo ni ilipe mshahara ikiwemo mishahara ya wakurugenzi na wakuu wa idara ambao mishahara na idadi inafanana bila ya kujali ukubwa au udogo.hivyo hivyo kwa vikao vya madiwani, umeme na kadhalika.

Chukulia fixed expenditure kwa council ni tshs 900,000,000/=linganisha mfano Kama ileje itakusanya tsh 1000,000,000/=hiyo ni 90%ya mapato yake hivyo 10%tu itakuwa ya miradi linganisha na mbozi mfano chukulia inakusanya 10,000,000,000/=na matumizi 900,000,000/=hiyo ni9%ya mapato yake hivyo hi itaweza peleka 90%ya mapato yake kwenye miradi ya maendeleo. unaweza kukuta Kenya ikatenga70%yabajeti miradi ukakuta taifa lingine likitenga kiwango cha chini zaidi. mapato zaidi miradi zaidi.
 

GwaB

JF-Expert Member
Mar 19, 2014
2,210
2,000
Wewe pimbi Kati ya Magu wa miaka 5 na Kikwete wa miaka 10 nani kakopa pesa nyingi? Usiwe mkiruukaji muwe mnasoma kabla ya kuharisha.

Magu kaacha deni la Taifa 71 trillion kutoka 35 tirion
Jifunze kwanza ustaarabu katika kuwasiliana na watu, unaweza ukaeleweka vizuri tu bila hata kutumia lugha za mtaani.🥸
 

Nikupa

JF-Expert Member
Mar 15, 2018
304
500
Kuna siku niliona ili jambo wakat wizara ya tamisemi inawasilisha bajet yake nilishangaa et matumiz yao ni fedha nyng kulko ya maendeleo ,nafikir hii ipo kila wizara kiukwel inafikilisha
 

skiiiwalker92

Member
Dec 30, 2016
28
75
Hii ni abajeti ya mwaka 2020/21

, Wizara ya Fedha na Mipango inaomba kuidhinishiwa jumla ya shilingi trilioni 12.39 kwa mafungu yote saba (7) kwa ajili ya matumizi ya kawaida na maendeleo. Kati ya kiasi hicho, shilingi trilioni 11.73 ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida na shilingi bilioni 659 kwa ajili ya matumizi ya maendeleo. Kati ya matumizi ya kawaida, shilingi trilioni 10.48 kwa ajili ya deni la Serikali, shilingi bilioni 750.29 matumizi mengineyo na shilingi bilioni 510 kwa ajili ya mishahara na marekebisho ya mishahara. Aidha, matumizi ya maendeleo yanajumuisha shilingi bilioni 624.7 fedha za ndani na shilingi bilioni 34.61 fedha za nje.
 

Blac kid

JF-Expert Member
Apr 1, 2012
6,425
2,000
kwa Pesa ya Shilingi Trilioni 1.02. kutakuwa na Maendeleo kweli? Tutamkumbuka Mzee Wetu Hayati Magu Mungu amuweke mahali pema amin.
Bajeti ya samia na ya mwendakuzimu haina tofauti acheni propaganda nyie wazee wa ligasi.
 

Tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
43,543
2,000
kwa Pesa ya Shilingi Trilioni 1.02. kutakuwa na Maendeleo kweli? Tutamkumbuka Mzee Wetu Hayati Magu Mungu amuweke mahali pema amin.

Utamkumbuka kwa lipi, kaingia madarakani kakuta deni la taifa ni 39t+, sasa deni limepaa mpaka 71t chini ya utawala wake, na hakuna maendeleo yanayoendana na hiyo hela. Au ni mmoja ya wale aliofanikiwa kuwabrainwash kwa propaganda zake?
 

MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
40,604
2,000
Utamkumbuka kwa lipi, kaingia madarakani kakuta deni la taifa ni 39t+, sasa deni limepaa mpaka 71t chini ya utawala wake, na hakuna maendeleo yanayoendana na hiyo hela. Au ni mmoja ya wale aliofanikiwa kuwabrainwash kwa propaganda zake?
Wwe Mungu amekuupa macho möawili huoni, amekupa masikio mawili husikii sasa nitakwambia kitu gani mpaka uniamini? Hilo deni la taifa ni 39t+ ulitaka alimalize kwa muda miaka 5? Inawekana kweli? Hawakuwea kulipa utawala uliopita hilo la deni la taifa ni 39t+ ataweza kulipa Marehemu Magufuli kwa muda wa miaka 5? Kama huna macho ya kuona aliyoyafanya Hayati Dr.Magufuli nyamaza kimya.
 

Blac kid

JF-Expert Member
Apr 1, 2012
6,425
2,000
Wewe unajuwa Bajeti ya Taifa Pesa zake zinatoka wapi? Kama sio Wizara ya Fedha? Na kama Bajeti ya Wizara ya fedha imeidhinisha pesa ndogo za Maendeleo ya nchi Pesa ya Shilingi Trilioni 1.02. Bajeti ya Taifa itakuwa imo humo humo ndani yake. Kwani Bajeti ya Taifa ipo chini ya Wizara ya Fedha.
Mzee tuwekee bajeti ya wizara ya fedha ya mwaka wowote ktk utawala wa mwendakuzimu tukompee na kukontrast hapa jamvini.
 

Joh Doe

JF-Expert Member
Sep 23, 2019
576
1,000
Kinachoamua uwiano wa bajeti iegemee wapi zaidi ni mapato yanayokusanywa nchini kwako kwanza. Mara nyingi matumizi ya kawaida kama kulipa madeni (ya ndani na nje), mishahara, posho, ununuzi wa magari, mafuta, ruzuku, n.k huwa vinakuwa na ongezeko ambalo haliendani na kasi ya ukusanyaji mapato, hivyo hupelekea kiasi kikubwa kutumika ktk upande huo na kiasi kidogo kinachosalia huenda ktk maendeleo. (Revenue-driven budget)

Kwa sehemu kubwa ya deni la taifa hukopwa ili kuongeza kiwango cha bajeti ya maendeleo na kiasi kingine huwa tunachangiwa na wahisani. Ila njia ya kutoboa kupitia bajeti ndogo ni kuhakikisa tunakuwa na miradi michache ila inapata uwekezaji mkubwa na kupunguza miradi isiyo na tija sana na yenye uchocheo mdogo ktk uchumi. Pia, serikali ijikite ktk kutoa huduma zaidi haya mashirika ya kibiashara kama ATCL ingetafutwa namna tuyamiliki kwa asilimia 25 tu, ili tupunguze gharama za uendeshaji. Mengi yanaendeshwa kwa pesa za umma.
 

Noti bandia

JF-Expert Member
May 3, 2020
889
1,000
Ukishajua utafanya Nini sasa, hujui lolote kuhusu uchumi unavyoendeshwa so kaa kimya,waza kesho watoto wako watakula Nini maana hili swala lipo juu sana kwa uwezo wako finyu wa kufikiria maana hata ukipewa mchanganuo ni matumaini yangu utatoka patupu
No. Muuliza swali anahoja nzuri tu sema wewe umekataa kujua hayo matumizi mengine ni yapi? Hv nikuulize swali, unawatumishi kadhaa wa wizara wanadai 60% ya bajeti mzima ya wizara. Je utalipa kwanza mishahara au utapotezea then uwaze hayo maendeleo inayoyawaza?. Kunamatumizi mengineyo huwezi kuyakwepa ili ukafanye maendeleo mengine
 

tajiri tumbo kubwa

JF-Expert Member
May 27, 2021
324
500
Bunge aliloliingiza kwa nguvu kubwa na mabavu makubwa ndio linapitisha hiyo bajeti, hakuna objection wala mtu wa kuhoji, kuna umuhimu wa bunge kuwa na wawakilishi kutoka vyama vyote la sivyo kila litakalopitishwa basi watasema ndio kwa sababu ni watoto wa baba mmoja

Lawama zote kwa Jonh
sielewi watu wengine kabisa, mtu hapa anamusifu dikteta magufuri aliyeiba kura mchana kweupe bunge ni 100% ccm, alafu mtu hapa anasema apumuzike pema, ndio watz wengine watabaki masikini ajabu,huyu hawezi connect the dots ajue where the problem is,and how we got here.huyu mwigulu ni ile wizara yake huko boat walijilipa mamia ya mamilioni hata wakati wa siku isio ya kazi, safari ndefu sana kwa bongo
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom