Fedha ya matumizi ya kawaida kuwa kubwa kuliko ya matumizi ya maendeleo ina maana gani?

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,315
33,111
WIZARA YA FEDHA TANZANIA.jpg

BAJETI ina matumizi mengi ya kawaida kuliko Matumizi ya maendeleo ya nchi?

Hivyo kweli tutaendelea
nchi yetu kiuchumi? Bajeti aliyotoa Waziri wa Fedha na Mipango Dkt Mwigulu ili ipitishwe na Wabunge ni bajeti mbaya haifai kupitishwa Wabunge.

Tunamuomba Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Mwigulu atueleze Shilingi Trilioni 11.93 zitatumika kwa ajili ya Matumizi yapi ya kawaida? Wakati pesa aliyoweka ya Maendeleo ni ndogo sana Shilingi Trilioni 1.02.

Maendeleo gani yatakayoweza kuifanikisha Tanzania kwa Pesa ya Shilingi Trilioni 1.02.? Hebu atufafanulie zaidi Mheshimiwa Waziri wa Fedha na Mipango Dkt Mwigulu.
 
kwa Pesa ya Shilingi Trilioni 1.02. kutakuwa na Maendeleo kweli? Tutamkumbuka Mzee Wetu Hayati Magu Mungu amuweke mahali pema amin.
Bunge aliloliingiza kwa nguvu kubwa na mabavu makubwa ndio linapitisha hiyo bajeti, hakuna objection wala mtu wa kuhoji, kuna umuhimu wa bunge kuwa na wawakilishi kutoka vyama vyote la sivyo kila litakalopitishwa basi watasema ndio kwa sababu ni watoto wa baba mmoja

Lawama zote kwa Jonh
 
Hakuna maendeleo hapo kwa bajeti Pesa ya Shilingi Trilioni 1.02 Watapitisha Wabunge wa CCM kwa sababu wapo wote bungeni hakuna upinzani hapo. Bunge linaloongozwa na chama kimoja kwa asilimia 99.
 
Hiyo ni bajeti ya Wizara ya fedha siyo bajeti ya taifa!
Wewe unajuwa Bajeti ya Taifa Pesa zake zinatoka wapi? Kama sio Wizara ya Fedha? Na kama Bajeti ya Wizara ya fedha imeidhinisha pesa ndogo za Maendeleo ya nchi Pesa ya Shilingi Trilioni 1.02. Bajeti ya Taifa itakuwa imo humo humo ndani yake. Kwani Bajeti ya Taifa ipo chini ya Wizara ya Fedha.
 
Fedha za maendeleo zimetawanywa kwa kila wizara!
 
Madeni ni mengi ndiyo maana wanataka kulipa wakandarasi wa ndani, mwendazake alikuwa halipi
 
Akili kweli mali, Wizara umeomba hizo fedha kwa mafungu yake 7, kila wizaea zinapitisha bajeti zake sasa mtu mzima unashindwa kuelewa kuwa hiyo ni bajeti ya Wizara afya. Ujinga ni mzigo
 
Back
Top Bottom