Phillipo Bukililo
JF-Expert Member
- Dec 29, 2015
- 18,487
- 13,612
Biblia inafundisha kwamba kifo cha Nabii Issa (Yesu), kilitokana na Yuda Iskariote ambaye alikuwa ni mmoja wa mitume 12, kuamua kumuuza kwa watu waliotaka kumuua. Vipande 30 vya fedha vikatumika kama malipo ya kazi kwa Yuda, ambaye alitumia mbinu ya kumbusu kiongozi wake ili wale wenye nia ya kutaka kumkamata na kumuua waweze kumtambua. Mafundisho ya Biblia yanatuambia kuwa Yuda alijinyonga baada ya nafsi yake kumsuta.
Wenye kujua kuyachambua maandiko matakatifu husema kuwa hayazeeki wala kupoteza maana. Sisi tuliohai leo hii tutakufa lakini ujumbe wa maandiko hata siku moja hauwezi kufa.
Wakati wa kampeni kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka jana, kina Yuda Iskariote walikuwa kazini, wakitumia kila aina ya muanya ili waweze kutengeneza fedha. Uchaguzi ukamalizika lakini kwa sababu kwa miaka mingi tumeshindwa kuukwepa ushawishi wa fedha, tumebakia kuabudu njia haramu za utafutaji wa mapato.
Imekuwa ni kama haki kabisa kwa mnyonge kuonewa na yule muoneaji anazidi kutafuta njia za yeye kubaki muoneaji mwenye fedha. Tunaambiwa kuwa matajiri wanaoushikilia uchumi wa nchi hawazidi kumi. Lakini wameweza kuwaweka chini ya himaya yao kina Yuda Iskariote wengi sana. Hawa wasaliti walio tayari kufanya lolote kwa faida ya wale wenye vipande 30 vya fedha, hawawezi kuiacha serikali ya awamu ya tano ipate usingizi wa amani.
Kina Yuda Iskariote wala hawalipwi fedha nyingi, ila madhara ya matendo yao huacha laana zinazodumu kwa vizazi na vizazi. Kumpigania mnyonge ni kukubali kwamba katika unyonge wake kuna kila aina ya uwezekano wa Yuda Iskariote kutafuta njia za kumbakiza milele kwenye unyonge unaomuumiza, kwa ajili tu ya ustawi wa matajiri wachache.
Serikali ya awamu ya tano mmekubali kumpigania mnyonge, mmekubali kupambana na kina Yuda Iskariote walio wengi sana, wenye kufanya kazi kwa ajili ya matajiri wachache sana. Ipo kazi nzito katika kuitambulisha jamii kwamba fulani na fulani ndio kina Yuda Iskariote.