Februari 25, 2020 rufani ya Lissu kupata kibali dhidi ya Spika kumvua ubunge

bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
21,274
24,141
February 24, 2020

Mahakama Kuu ya Tanzania siku ya Jumanne Februari 25 mwaka huu itasikiliza maombi ya aliyekua mbunge wa Singida Mashariki,Tundu Lissu anayetaka apate kibali cha kuukatia rufaa uamuzi wa Spika wa Bunge,Job Ndugai kumvua ubunge.

Wakili Alute Mughwai ambaye ni kaka yake Lissu akizungumza na Mwananchi nyumbani kwake jijini hapa amesema maombi hayo ni kupinga uamuzi wa Jaji Silius Matupa wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam uliotolewa September 2019.

Source: MCL Digital
 
Njaa haina baunsa, sasa ukoo mzima unalilia kiinua mgongo chetu.

No, you don’t get our money!
 
Majaji watakaoitwa icc au takukukuru mwaka 2025 ni pamoja na huyu matupa
Umewasahau UVCCM ambao wanadiriki kusema kwenye vyombo vya habari wangemuua Zitto, na yule mchumia tumbo la utapia-mlo kule bungeni aliosema Zitto auliwe (ushahidi wa kumfunga ni rekodi za hansard).

Na kuna mwingine alidiriki kuingia Clouds FM na mitutu ya bunduki za moto kama vile nchi ipo vitani.
 
Sijui kama atakuwepo maana nimeonana naye kwenye wodi fulani hapa karibu na Central Police, taasisi yangu inafadhili mradi fulani pale.
Mungu hadhihakiwi. Unaweza kuwa na nguvu za ajabu za kuwaua na kuwatesa unaodhani hawana uwezo wa kupambana nawe LAKINI na wewe unaweza kufa au kuteseka kwa namna nyingine. Mwisho wa yote ukateseka kama unavyotesa, na ukafa kama unavyokuwa ukiua.

Tuishi kwa hekima ya Mungu, hekima ya upendo.
 
Mahakama Kuu ya Tanzania siku ya Jumanne Februari 25 mwaka huu 2020 itasikiliza maombi ya aliyekua mbunge wa Singida Mashariki,Tundu Lissu anayetaka apate kibali cha kuukatia rufaa uamuzi wa Spika wa Bunge,Job Ndugai kumvua ubunge.
 
Sijui kama atakuwepo maana nimeonana naye kwenye wodi fulani hapa karibu na Central Police, taasisi yangu inafadhili mradi fulani pale.
Acha kujimwambafai. Uwe na taasisi halafu uje kushinda huku JF? Eti "taasisi yangu", ipi?
Nakukumbusha tu kuwa Mtikila alisema maneno kama hayo kuhusu Lowassa, na unajua nani aliyetangulia.
Wewe siyo Mungu, si ajabu akawepo na wewe ukaondoka kabla yake. Tubu, na uwe na unyenyekevu kuhusu maisha, acha kutabiria wengine mabaya.
 
Hako kadada bwana! Eti tasisi yangu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom