FEAR Of UNKNOWN DESTINATION | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

FEAR Of UNKNOWN DESTINATION

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Kituko, Oct 25, 2010.

 1. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #1
  Oct 25, 2010
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,367
  Likes Received: 7,008
  Trophy Points: 280
  Akijibu swali la Mwanachama mfu wa CCM (A, Lwaitama), Dr Slaa alisema, kisaikolojia hiyo ni hulka ya binadamu kuogopa asipokujua,
  lakini ni kweli watu hawakujuhi huko?

  Miongoni mwa sifa kuu za binadamu ni usahaurifu, na hiyo ndio inayompa matumaini makubwa sana binadamu ile hali ya kusahahu ikitokea basi kila kitu kinaonekana ni kawaida tu, na binadamu anaendelea kupambana na maisha yake mapya bila kumbukumbu ya yale ya zamani. sifa nyingine kuu ni hofu, na hii hofu yaweza kuwa ni yako mwenyewe (personal) ama ya kupandikizwa (kutiwa hofu)

  Swali ni wapi huko kusikojulikana?
  Asilimia karibu ya hamsini ya Watanzania wanakujua huko Dr Slaa anapopazungumzia ila wamesahau na kuona hali iliyopo ni ya kawaida tu, namaanisha wamekusahahu kule kulikokuwa na Elimu ya Bure, Matibabu ya Bure, Heshima kwa UTU wa mtu, utawala wa kuheshimu katiba, kuheshimu mali za umma pamoja na rasilimali zake, kule kulikokuwa na Miiko ya uongozi na kule kulikokuwa na Watanzania waliokuwa tayari kuitetea nchi yao (Kimichezo, sanaa na hata kijeshi) ni usahaurifu tu. lakini Dr Slaa anawakumbusha na yupo tayari kuwarudisha kule kwenye nchi ile ya Asali na Maziwa (Tanzania), keshajitoa muhanga na kisha onyesha nia na njia ya kupitia kurudi kule, hauna haja ya kupigana wala kumwaga damu ili Dr Slaa akurudishe kule, anachohitaji kwako ni wewe kuweka (√) tu kwenda kwake

  Lakini pia kuna karibu ya aslimia hamsini ya Watanzania hawakujuhi kule anapopazungamzia Dr Slaa, hawajawahi kuiona ile Tanzania, wako tayari kwenda kule lakini wanatatizo la Hofu, wanaogopa kwa sababu wametiwa uoga nafsini mwao kuwa hicho kitu akiwezekani, Dr Slaa atapata wapi Pesa? Na wameambiwa hiyo nchi anayoizungumzia Dr ni ya kufikirika tu, haipo, yaani wanaambiwa na Viongozi waliopo kwamba Utawala bora (usio wa kirafiki, Kindugu, Kikabila, Kidini) hauwezekani Tanzania, Ndugu zanguni hakuna vita itakayotokea kwa wewe kuibadilisha hii serikali iliyopo, kama una hofu na hayo waulize wale waliokuwepo kwenye nchi ile watakwambia inawezekana na wao wameshawahi kushuhudia

  Nchi ilikuwa na watu wachache na rasilimali chache na zilitumika kwa faida ya Watanzania wote, sasa nchi ina watu wengi na ina rasilimali nyingi mno lakini zinatumiwa na watu wachache,
  Dr Slaa anataka hizo rasilimali (keki) ya Taifa tugawane wote (katika uduma muhimu za kibinadamu) na kila raia awe katika hali ya kiutu
  Wakati naendelea kuandika nasikia sauti ya Nyerere ikitukumbusha it can be done-play your part
  Kwa kuweka √ kwenda kwa Dr Slaa hiyo 31 October 2010, na utakuwa umeweka historia katika nchi hii, utakuwa umeshiriki katika ukombozi wa kuirudisha Tanzania kwa Watanzania na kwa faida ya Watanzania wa sasa na wale wajao
   
 2. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #2
  Oct 25, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,767
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  nI KWELI CHUKULIA SAMAKI WAMAGUFULI TUU! MFANO MZURI WAKUWA RESOURCES HAZITUMIKI SAWASAWA!
   
 3. luvcyna

  luvcyna JF-Expert Member

  #3
  Oct 25, 2010
  Joined: Feb 24, 2009
  Messages: 1,441
  Likes Received: 1,035
  Trophy Points: 280
  naomba msaada kisheria kuprint hii na kupeleka copy za kutosha kijijini kwangu ambapo watu wengi hawafikiwi na technogy kama hii ya email inawezekana. Je ntakuwa sijavunja sheria yeyote ya nchi?
   
 4. d

  dotto JF-Expert Member

  #4
  Oct 25, 2010
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 1,720
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Dr. Slaa 68%
  Kikwete(dr) 22%
  na...
  na...
  na...
  31/10/2010
   
 5. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #5
  Oct 25, 2010
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,367
  Likes Received: 7,008
  Trophy Points: 280
  kwa faida ya Watanzania wenzangu iko huru kucopy ,na hata kutuma kwa yoyote
   
 6. k

  kijukuu kindo Member

  #6
  Oct 25, 2010
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 87
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Subject: Fwd: FW: Mipango ya kuchakachua kura 31/10

  Subject: Mipango ya kuchakachua kura 31/10  Taarifa ya Siri - Mikakati ya Kuiba Kura Inavyoendelea USALAMA WA TAIFA

  Napenda kuwajulisha mikakati michafu ya kupora na kuzuia maamuzi ya umma yanayofanywa na ccm kwa uratibu wa usalama wa taifa. Baada ya kubaini dalili za kuanguka vibaya katika uchaguzi wa mwaka huu idara ya usalama wa taifa imeandaa mikakati ya kuiba kura ili kuzuia chadema msiingie ikulu.

  Mikakati hii inaeleweka vizuri kwa tume ya taifa ya uchaguzi ambayo inashirikiana bega kwa bega na idara ya usalama wa taifa kumtengenezea jk ushindi bandia wa 80%. Wana hakika watanzania watagundua wizi huo na watakataa matokeo ndiyo maana kwanza waliwatumia viongozi wa dini waliotembelea makao makuu ya chadema wawasihi chadema wakubali matokeo yatakapotangazwa na juzi wamelitumia jeshi kutisha wananchi watakaoamua kupinga matokeo ya kupikwa yanayoandaliwa na nec/usalama wa taifa. Majid Kikula ambaye ni government security officer ndiye mratibu wa zoezi la kuiba kura, ni mtaalamu aliyebobea katika kazi za aina hii aliratibu vizuri zoezi kama hilo mwaka 2005. Pia mwaka 2007 alitumwa kenya kwenda kumsaidia kibaki kupora ushindi wa odinga.

  Kikula anatumia muda wake mwingi hivi sasa ofisi za tume ya uchaguzi kwa ajili ya uratibu wa uvurugaji daftari la kudumu la wapiga kura akiifanya kazi hiyo kwa karibu na baadhi ya watendaji wa nec na maafisa kadhaa wa usalama wa taifa kutoka kurugenzi ya IT ya idara ya usalama (DITA) ambao wako ndani ya nec kwa zaidi ya miezi sita sasa, nitawapatia majina yao. Pia kuna vijana wataalamu wa IT waliochukuliwa kutoka maeneo mbalimbali wamepewa nyumba upanga mtaa wa undali shughuli kubwa wanayofanya ni kuandaa utaratibu wa ku-access remotely daftari la kudumu la wapiga kura. Hawa wanafanya kazi chini ya Salva Rweyemamu na Mindi Kasiga kutoka kurugenzi ya mawasiliano ikulu.

  Wapo vijana kadhaa leo nawapa majina ya wawili; Maharage Chande na Edgar Masatu wanafanya kazi kwa karibu na Nzowa wa idara ya usalama ambaye ndiye aliyeratibu shambulio la kumwagiwa tindikali Kubenea. Pia kuna kundi linalojumuisha wataalamu wa printing wa kiwanda cha uchapaji cha usalama wa taifa kilichopo MALINDI ambao hivi karibuni walikuwa mjini tanga kwa semina fupi ya jinsi ya kughushi kura kupitia fake ballot paper, timu hii inaongozwa na ndg SINYAU.

  Kwa hiyo utaona kwamba imeandaliwa mikakati mingi kuufanikisha uovu huo ili mmoja ukikwama basi mwingine utatumika ila wameamua ni lazima jk ashinde kwa 80%. Ndani ya idara ya usalama wa taifa maafisa wengi wamechoshwa na uongozi mbovu wa ccm hivyo wanataka mabadiliko ya uongozi idara imechukua hatua kadhaa kuhakikisha maafisa wote wa idara wanampigia kura jk, wote wameagizwa kuwasilisha vitambulisho vyao vya kupigia kura ili vinakiliwe namba ili atakayepigia upinzani afukuzwe kazi baada ya uchaguzi. Fuatilieni kwa karibu haya niliyowaeleza nimeyapata kwa nafasi yangu ndani ya tiss. Huyu KIKULA mfuatilieni kwa karibu ni hatari. HAKIKISHENI DUNIA NA WATANZANIA WOTE WANAJUA MAPEMA HILA HIZI. Jambo la kujiuliza maafisa usalama wa taifa wanafanya nini ndani ya tume ya uchaguzi wakati huu.   
Loading...