FC Barcelona (Barça or Blaugrana) | Special Thread

Screenshot_2017-08-18-08-06-39-1.png

Management they must do something kuna tofauti kubwa sana ya composition ya team enzi hizi na zile ambazo tulianza kuipenda Barca
Wachezaji wengi sasa hivi ni liability sio asset kabisa ,mfano juzi Suarez aliumia akawa anashindwa hata kutoka kwa sababu ni replacement -best
 
  • Thanks
Reactions: PNC
Liver tuachane nao, mtu ameshawaambia sitaki kuendelea na ninyi wanamzuia wa nini, wawe wastaarabu Kama Barca, Neymar aliposema tu anataka kuondoka Barca wakampa ruhusa ya kutofanya mazoezi ili ashughulikie future yake
 
2786881873684c9353b238e6f9fc16f5.jpg

2cc53714975fd8b9416fbe792ce495df.jpg

Kiukweli naona kuna shida kwenye management ya Barca. Hiyo habari ya Messi wanasema Messi kutosaini mkataba mpya ni kwa sababu anataka kutumia pressure hiyo kama njia ya kumfanya Rais wa klabu ajiuzuru coz inaonekana Messi hamkubali Rais wa timu.
Nadhani kwa sasa Barca inashida sio tu uwanjani bali hata nje ya uwanja
 
KUSHUKA KWA LA MASIA NDIYO ANGUKO KUBWA LA UFALME WA BARCELONA.

Lilikuwa jambo lenye maono makubwa sana kwa Josep Nunez kutumia muda mwingi ofisini kwake kusoma karatasi za Johan Cruyff.

Karatasi zilizokuwa na mawazo yenye thamani kubwa kuliko thamani ya madhari ya ofisi ya Josep Nunez kwa wakati ule.

Karatasi ambazo zilikuwa na umbo zima la utamaduni wa Barcelona utakavyokuwa.

Utamaduni ambao ulikuja kuzalisha matunda mengi ya Barcelona ndani ya muongo mmoja uliopita.

Alichokiona Johan Cruyff 1979 kwenye akili yake ndicho hicho ambacho kilikuja kuishi kwenye mafanikio ya Barcelona.

Wafalme wengi walikuwa wanatengenezwa na kupewa nafasi ya kuongoza falme ya Barcelona.

Imani ilijengwa katika kituo cha La Masia. Vijana wengi walipikwa kuwa wachezaji bora na siyo wachezaji imara peke yake.

Sylabus ya chuo cha La Masia ilikuwa tofauti na vyuo vingine. Kwenye kila somo ambalo lilikuwa lunafundishwa pale La Masia, lazima mada ya kuifia Barcelona ilikuwepo.
Vijana walifundishwa kuipenda na kuipigania Barcelona baada ya Mpira.

Kwao Barcelona ndiyo ilikuwa dunia yao ambayo waliagizwa kuitunza na kuipigania zaidi.

Vipaji vingi vilitoka pale La Masia mpaka tukashuhudia mchezaji wa kwanza kutoka La Masia kuchua tunzo ya Ballon D'or mwaka 2010.

Matunda ya chuo hiki yalidhihirika wazi pindi pale Barcelona ilipochukua kombe la klabu bingwa ulaya (UEFA) wakiwa na wachezaji saba kutoka La Masia.

Hiki ndicho alichokuwa anakiona Johan Cruyff kipindi kile anampelekea Josep Nunez karatasi za mapendekezo yake.

Wazo la Masia kuanzishwa lilikuwa kuwatumia vijana wanaotoka kwenye chuo hicho ili waweze kuibeba Barcelona.

Ulifikiria sababu ya Johan Cruyff kupendekeza Pep Guardiola kuwa kocha wa Barcelona??

Hii yote ilikuwa kuanzisha tamaduni ya Barcelona kuwa kwenye mikono mtu anayeijua vizuri timu.

Mtu ambaye atadumisha tamaduni ya kuwapandisha wachezaji wa La Masia mpaka kwenye timu ya wakubwa.

Waliaminishwa tangia chuoni kuwa wao ni wachezaji bora, wao ni bora kuzidi mchezaji yoyote duniani na wanacheza kwenye timu ambayo ni bora kuzidi timu yoyote duniani.

Jeuri ya kucheza mpira bora ndipo ilipoanzia hapo.

Mpira waliufanya kama wamezaliwa nao, wanakula nao, wanaoga nao, wanalala nao, kwa kifupi mpira uliishi na wao na wenyewe wakauishi mpira.

Chini ya Pep na wachezaji wake kutoka La Masia kila kitu kilienda kama watakavyo.

Walichukua kila kombe watakalo, walifunga kila aina ya goli watakalo, walishinda kila ushindi watakao na hii ni kwa sababu walitukuza vipaji kutoka La Masia na vipaji vikawatukuza wao na mwisho wa siku mpira ukawatukuza zaidi.

Mafanikio yakawa kitu cha kawaida chao, mafanikio ambayo yalileta ufalme imara kwenye mpira.

Hakuna aliyefikiria kwa Barcelona kama itaanguka tena kwa sababu La Masia ilikuwepo. La Masia ndiyo ilikuwa kuburi cha Barcelona.

Waliamini mrithi wa Iniesta atapatikana La Masia pekee, ilikuwa ngumu kuamini kuna mchezaji atasajiliwa kwa ajili ya kuziba pengo la Xavi.

Kwao wao waliamini warithi wa kizazi cha dhahabu watatokea La Masia ndiyo utamaduni waliouweka.

Utamaduni ambao ulisababisha wachezaji watatu kutoka La Masia ( Iniesta, Xavi na Messi) kuwepo kwenye orodha ya wachezaji watatu bora waliokuwa wamebaki kuwania tunzo ya Ballon D'or.
Mafanikio haya yalijenga imani kuwa La Masia ni uti wa mgongo wa Barcelona.

Utamaduni huu ulianza kuondoka taratibu baada ya Luiz Enrique kuwa kocha.

Alikuwa siyo mtu wa kuiamini La Masia, hata alipokumbushwa kuwa mwaka 2012 Barcelona ilicheza mechi na Levante ikiwa na kikosi chote cha wachezaji waliotoka La Masia.

Kwake yeye hakuwa muumini na hiki chuo, hata Josep Maria hakumkemea kwa kuamini kocha ndiye mwenye maamuzi ya mwisho kwenye kujenga timu kwa aina ya wachezaji anaotaka.

Kuanza kusajili wachezaji nje ya La Masia kulisababisha kupata watu ambao hawana damu ya kuipenda Barcelona baada ya mpira.

Wachezaji ambao mwisho wa siku wamewakimbia, wachezaji ambao kwa kiasi kikubwa hawakuwa na uwezo na vipaji vikubwa kama vile vilivyotoka La Masia.
Mzigo kaachiwa Ernesto, kaachiwa watu ambao walitoka La Masia lakini umri na viwango vyao vinawatupa.

Muda umeenda kwake yeye kupata mafanikio ya muda mfupi kupitia La Masia.

Ndicho kipindi cha mpito kwake na timu kwa ujumla, hana budi kusajili wachezaji wanaonekana kukomaa huku akipandisha watu wengine tena kutoka La Masia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
We jamaa Barcelona unaijua sawa sawa, ukiachana na hayo, soka pia unalijua, na hoja zako ziko sawa. Kuna mashabiki wa Barcelona viazi kishenzi, yaani hata yanayotokea Barcelona sidhani kama wana upeo mzuri wa kuona which is which, wamebakia tu na umbeya oooh countinho tayarrr bado kupima mkojo, mara tena dembele hataki kujisaidia chooni mwa viwanja vya Dortmund, anataka akajisaidie chooni kule nou camp. Halafu hao mashabiki viazi wakishajua ni umbeya hawakiri, wanabaki mgt ya Barcelona kuna shida. Nawashauri waende Zimbabwe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Liver tuachane nao, mtu ameshawaambia sitaki kuendelea na ninyi wanamzuia wa nini, wawe wastaarabu Kama Barca, Neymar aliposema tu anataka kuondoka Barca wakampa ruhusa ya kutofanya mazoezi ili ashughulikie future yake
Neymar alikuwa na release clause so timu ikilipa hakuna wa kumzuia,Coutinho hana release clause so kumsajili lazima ufanye mazungumzo na klabu yake
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom