FC Barcelona katikati ya upepo mkali wa uhuru wa jimbo la Catalunya

Aaron Arsenal

JF-Expert Member
Jul 24, 2014
24,504
28,695
.
Pengine unaweza ukahisi sio stori kubwa sana ila ni kitu kikubwa sana klabu ya Barcelona imeamuwa kufanya kuelekea harakati za uhuru wa Jimbo la Catalunya, kaskazini Mashariki mwa nchi ya Hispania.
.
Mwanzoni mwa wiki hii maandamano yalifanyika jijini Barcelona kupinga hukumu iliotolewa na serikali ya Hispania (Madrid) kuwahukumu kifungo cha miaka 9-13 wanaharati 9.
.
Barca kupitia account yao ya Twitter walitweet kuwa wanasiasa hao waachiwe huru, taharuki kubwa ikapelekea mpaka mchezo wao dhidi ya Real Madrid kuhisiwa kutumika kama sehemu ya kufanya maandamo
.
Barcelona inakuwa sehemu muhimu kwenye harakati haswa ikizingatiwa kuwa wana msemo wao 'Mes que un club' tafsiri kuwa wao ni zaidi ya klabu, maana ni kama timu ya taifa la watu huru wa Catalunya.
.
Wachezaji mashuhuri kama Gerrard Pique na Sergio Roberto pamoja na Pep Guardiola na Xavi Hernandez ni watu ambao mara nyingi hutoa kauli mbalimbali
.
Kupitia soka hili bado watu wa Catalunya wanaamini La Liga haiwapi wao nafasi ya kuongoza kwakuwa hata Rais wa sasa Javier Tebas ni shabiki mkubwa wa Real Madrid na ni mtu wa jimbo la Madrid, ndie yeye aliyetoa tamko la Barcelona wacheze bila mashabiki ndani ya Nou Camp 2017 siku ya upigaji kura na ndie yeye aliamuru Las Palmas wacheze mechi huku jezi zao zikiwa na nembo ya taifa la Hispania kuonesha mshikamano.
.
Bado rangi za jezi ni rangi ya bendera yao wakipendelea kuimba wimbo wao wa taifa, hao ndio wakatalunya na Barcelona yao.
.
Tatizo kubwa ni masuala ya kiuchumi tangu zama za General Franco, Catalunya haikuwa huru na utamaduni wao kila kitu chao kuanzia lugha ilikuwa haramu, hii vita wanayopambana ni ya zaidi ya miaka 1000.
.
Catalunya ina watu 16% ya Hispania nzima, inasafirisha bidhaa nje (exports) kwa 25.6% ya nchi nzima na uwekezaji wa kigeni upo kwa 20.7% ndani ya Jimbo hilo.
.
Wakati unastaajabu la Catalunya kuna lingine la Basque region kule wanapotoka mafundi kama Ander Herrera, Inaki Williams huko nako wanakuwaga na fujo zao, nyumbani kwa Athletic Club Bilbao.
.
jr_farhanjr-20191027-0002.jpeg
 
Hivi maana ya uhuru ni nini?.Huwa naona hilo neno sometimes linatumika isivyotakiwa.

Kwani Zanzibar wakijitenga na Tanganyika watakuwa wamepata uhuru?

Kama ni ndio, kumbe sasa hivi Zanzibar ni koloni?
 
Back
Top Bottom