Fatuma Karume: Zanzibar inaidai Tanzania bara 4.6 trillion

USSR

JF-Expert Member
Jul 15, 2015
9,886
22,633
Fatuma Karume amesema Serikali ya Mapinduzi Zanzibar inaidai Serikali ya Jamhuri ya Muungano kiasi cha pesa cha trilioni 4.6 kutokana na kupokonywa kutoka kwa wadau mbalimbali wa maendeleo

Fatuma Karume ambaye mara kwa mara hujimwambafai kukulia Ikulu ya Zanzibar na hivyo kuwa anafahamu siri nyingi ameandika kupitia ukurasa wake wa Twitter kuwa Serikali ya Muungano imekuwa na kasumba ya kuipora pesa Zanzibar ambazo zipo Kikatiba na Kisheria juu ya Muungano

My take : Hawa Wazanzibar hawaridhiki kila siku wanaibuka na kero mpya ifike pahali tuunde Serikali moja including Zanzibar iwe kimkoa tu tutumie nguvu tu

USSR
IMG-20210429-WA0073.jpg
 
Huu ndiyo ukweli wenyewe mchungu. Zanzibar ni nchi mojawapo iliyo sehemu ya nchi mbili huru ziundazo JMT. Kwa hiyo stahiki zake zote zitokanazo na mambo yaliyoanishwa ndani ya muungano ni halali yake.
 
Mwanasheria alipokonywa hadhi ya uwakili na ndugu wa rais wa Aman karume Fatuma karume aisema serkali ya Zanzibar SMZ inaidai serkali ya SMT kiasi cha pesa cha trillion 4.6 kutokana na kupokonywa kutoka kwa wadau mbalimbali wa maendeleo

Fatuma karume ambaye Mara kwa mara hujimwambafai kukulia ikulu ya Zanzibar na hivyo kuwa anafahamu siri nyingi ameandika kupitia ukurasa wake wa Twitter kuwa serkali ya muungano imekuwa na kasumba ya kuipora pesa Zanzibar ambazo zipo kikatiba na kisheria juu ya muungano

My take : hawa wazanzibar hawaridhiki kila siku wanaibuka na kero mpya ifike pahali tuunde serkali moja including Zanzibar iwe kimkoa tu .tutumie nguvu tu

USSRView attachment 1768148
Huyu kuna kitu anakitafuta atakipata
 
Mmeanza msio na haya!
Deni la TANESCO mmelipa?
Halafu hela ya msaada mnataka mgawo, kaombeni na nyie mtupatie!
 
Akili nyingi huondoa maarifa,Hapa kwenye huu Muungano Nyerere alitumia akili badala ya Maarifa ndio matatizo tunayokumbana nayo hadi Leo.Walipo ungana tu ilitakiwa iwe Serikali moja kwa sasa haitakuja kutokea tena kuwa Serikali 1.

Hakuna lisilowezekana
Ngoja twende na Samia kwanza🙏
 
images (26).jpeg

Hivi Nyerere na Karume walivyochanganya ule udongo wa bara na visiwani kwenye kile chungu waliweka agano gani?

Na baada ya kuuchanganya waliupeleka wapi?

Atakayejua kile chungu kilipo na udongo wake na yale maneno anaweza vunja Muungano.... na sasa sababu hauvunjiki tuunde Serikali moja malalamiko yaishe
 
Mwambieni aweke pia Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania inaidai Zanzibar kiasi gani?! Na wanavyoijaza dunia ndg zetu hawa bila hizi fursa za ubwete ubwete upande wa pili kuanzia ajira,fursa za kibiashara ardhi tena yenye rutuba sijui wangekuwa wageni wa nani.Tanganyika haiitaji Zanzibar kama Zanzibar inavyoihitaji Tanganyika.Iko wazi,hawa wenye uwezo wasiwahadae wenzao wanaojikongoja.
 
Back
Top Bottom