Fatuma Karume: Zanzibar inaidai Tanzania bara 4.6 trillion

View attachment 1768230

Hivi Nyerere na Karume walivyochanganya ule udongo wa bara na visiwani kwenye kile chungu waliweka agano gani?

Na baada ya kuuchanganya waliupeleka wapi?

Atakayejua kile chungu kilipo na udongo wake na yale maneno anaweza vunja Muungano.... na sasa sababu hauvunjiki tuunde Serikali moja malalamiko yaishe


Butiama na kuleee Zenj kumkaburi
 
Tunahitaji kuwa na serikali moja kuondoa haya malumbano
Kwa maana hiyo muundo wa Serikali tatu hauepukiki. Zanzibar ni nchi inajitegemea na ipo fully autonomous maana Ina flag, Katiba yake plus wimbo wa Taifa, Tanganyika ndio haipo🤷🤷 maana ipo Serikali ya Muungano inayoitwa SJMT lakini serikali ya Jamhuri ya watu wa Tanganyika (SJWT ) ipo wapi? .

Saa nyingine huwa nawaangaliaga wazanzibari nashindwa kuwaelewa kwamba hawaoni serikali yao ipo Ila ni kweli imemezwa na Muungano na ni jambo ambalo ni lazima mnapokuwa na Muungano, sasa mbona Tanganyika haipo??????
 
Akisema maneno hayo akiwa wapi BARA au VISIWANI?

Kama akiwa BARA kwanini asirudi VISIWANI? Sina furaha na muungano wa wao kila siku wanamanunguniko tu,wakati wanabebwa sana.
 
Waliuweka ardhini kisha wakapanda mti juu yake

Kwa hiyo mti ulimea ukatupatia upepo na hewa tukapumua😃😍
Sasa tunaweza kwenda kuuchukua ule wa bara na kuurudisha bara na wa visiwani tukaurudisha visiwani?
 
😆😆.ally kessy yu wapi?Miaka 20+ from now ,kila mtu atachukua cha kwake na kuondokana na hizi bugudha.
 
Hilo sio deni waombe wapewe kisha wazilipe... wasidhani ni pesa ya mfukoni hiyo... naona Mama kaja na style mpya nusu nusu
 
Usalama gani ?hii hoja ni dhaifu sanaaaaaaa ukweli ni kwamba Zanzibar inahitajika sana katika muungano ndio maana Mwalimu Nyerere alikuwa tayari Kuzika nchi yake ya Tanganyika kwa ajili ya muungano
Inahitajika kwa sababu za kiusalama tu hakuna la zaidi labda kama wewe unalijua lingine
 
Fatuma Karume amesema Serikali ya Mapinduzi Zanzibar inaidai Serikali ya Jamhuri ya Muungano kiasi cha pesa cha trilioni 4.6 kutokana na kupokonywa kutoka kwa wadau mbalimbali wa maendeleo
Hizo ni porojo tu za mitandaoni
Zanzibar ilikua inadaiwa Bilioni 120 za umeme,ni Magufuli aliefuta kabisa Hilo deni
Wekeni ushahidi hizo Trilioni zimetokana na nini
 
2 state solution ndio dawa /muarobaini kero za muungano . Hapa jamhuri ya Zanzibar ,n'gambo ya pili ya Zanzibar channel Jamhuri ya Tanganyika. Jamhuri mbili zinaishi kwa amani na upendo milele daima.
 
Wakate kwenye hayo matrilion chenji yao wapewe... kwanini Zanzibar wanalazimishwa kutumia umeme wa Tanesco badala ya kuwa na umeme wao? Je huo umeme wa Tanesco uko Pemba na Kojani?
Una hakika wanalazimishwa kutumia umeme wa TANESCO?
 
Tatizo lilianzia pale walipofichwa nn faida ya muungano,, kwani kila nchi ikibaki pekee yake nn kitatokea, ok kumbe ni bahari ndiyo lengo, ha kwani usalama wenu hamuwezi kujilinda na maadui mpaka Zanzibar iwe pamoja na Tanganyika,, ok ila naona nao wana Haki ya kudai maana hapa tuna serikali mbili badala ya kuwa na serikali moja,, kumbe Zanzibar ilitakiwa uwe mkoa na siyo nchi!!!!
 
Hivi Nyerere na Karume walivyochanganya ule udongo wa bara na visiwani kwenye kile chungu waliweka agano gani?

Na baada ya kuuchanganya waliupeleka wapi?

Atakayejua kile chungu kilipo na udongo wake na yale maneno anaweza vunja Muungano.... na sasa sababu hauvunjiki tuunde Serikali moja malalamiko yaishe
UNA HOJA NZITO
 
Back
Top Bottom