Fatuma Karume ndiye mtu sahihi wa kuwa Rais wa TLS

Goliath mfalamagoha

JF-Expert Member
Aug 3, 2012
602
2,505
ONLY FATMA KARUME FOR TLS 2018

Katika kipindi hiki ambacho nchi yetu ipo katika mteremko mkali wa kuelekea kwenye bonde la giza hasa kwenye masuala ya haki za watu, Demokrasia na Uhuru wa watu kujieleza na kutoa maoni yao, Fatma Karume analifaa taifa kwa sasa kuvaa viatu vya Tundu Lissu hapo TLS.

Katika hili sipo tayari kumung'unya maneno, na ni kwa bahati nzuri sana, wasomi wa nchi hii hasa Mawakili na Wanasheria, hawajawahi kuelekezwa jinsi ya kupiga kura zao kwa kigezo cha kujitambua. Kila mmoja miongoni mwao anatambua faida na umuhimu wa kura yake moja kama walivyo wenzetu wa mataifa ya ng'ambo.

Nchi yetu kwa muda wa miaka mingi imekuwa na utamaduni wa sisi wanasiasa kuwatumia wapigakura kama mitaji ya kubakia madarakani huku tukiwatesa na kuwanyanyasa.

Lakini dawa ya utamaduni huu kwa miaka ya hivi karibuni imeanza kupatikana baada ya watanzania kuona wasomi wa nyanja hii ya Sheria hasa hawa Mawakili na Wanasheria wanavyopiga na kulinda kura zao kistaarabu kuwachagua Marais wao bila kuuliza vitu vya hovyo kama Chumvi, Kanga, Kofia na T-Shirt za Maisha Bora.

Nchi hii ilipofika hivi sasa, inawahitaji kwa gharama yoyote ile watu wenye karama na hulka kama ya akina Tundu Lissu Rais wa TLS, Dr.Hellen Kijo-Bisimba Mkurugenzi wa LHRC na Onesmo Olengurumwa Mkurugenzi wa THRDC na mtu huyo kwa sasa ni Wakili nguli Fatma Karume anayewania nafasi ya Urais wa TLS baada ya Tundu Lissu tarehe 14, April 2018.

Binafsi sitaki kuwazungumzia hao wagombea wengine watatu maana historia ya mtu ni Hakimu tosha anayejitosheleza. Mapambano na harakati za Wakili Fatma Karume katika kuipigania haki ndani ya Nchi hii ya wavuja jasho zinafahamika na ziko wazi, sio mtu wa kupepesa macho wala sio mtu wa kumung'unya maneno na kutafuna vijiti wakati akilisimamia jambo la haki.

Sina shaka nanyi Mawakili ama Wanasheria ambao kimsingi ninyi ndio wapigakura kwenye uchaguzi huu wa 14, April 2018 juu ya weledi wenu katika kufanya maamuzi ya kura ili kumpata mtu sahihi na jasiri anayeweza kusimama kwa niaba yenu. Kwa unyenyekevu mkubwa sana, naomba nimuombee kura zenu zote Bi.Fatuma Karume.

Natamani kuiona tena TLS imara chini ya Fatma Karume baada ya Tundu Lissu, natamani kumuona Fatma Karume akiungana na wapigania haki wengine walio mstari wa mbele katika kuhakikisha kuwa demokrasia na haki za watu katika kujieleza na kutoa maoni yao zinaendelea kupiganiwa na kutetewa wakati wote kama wafanyavyo Dr.Hellen Kijo-Bisimba wa LHRC na Onesmo Olengurumwa wa THRDC.

Wanasheria na Mawakili wangu, hivi sasa kinachofanywa na wenye mabavu ni kuwanyamazisha watu ili wafanye watakayo gizani, hivyo basi, lengo na kusudio lao kubwa ni kumpata mtu kwenye taasisi hii ambaye wataweza kumuelekeza nini afanye dhidi yetu na ninyi nyote.

Aidha, furaha kubwa na ndelemo kwa wenye mabavu, ni kumpata mtu bubu asiyesema au kukemea chochote badala yake abaki kupokea maagizo na maelekezo kutoka juu kama tunavyoona katika mihimili na taasisi nyingi tu hapa nchini.

Ikitokea nafasi hii ya Urais wa TLS akaipata mtu mkimya asiyesema wala kukemea lolote lifanywalo na wenye nguvu dhidi yenu au sisi wananchi wa kawaida, basi mjue moja kwa moja nje ya baadhi ya vyama vya siasa, kama taifa tutakuwa tumebakiwa na watetezi wawili tu wa haki ambao ni LHRC na THRC ukituachilia mbali sisi Wanaharakati 28 wa Haki na Demokrasia.

Fatma Karume for TLS 2018
 
Aidha, furaha kubwa na ndelemo kwa wenye mabavu, ni kumpata mtu bubu asiyesema au kukemea chochote badala yake abaki kupokea maagizo na maelekezo kutoka juu kama tunavyoona katika mihimili na taasisi nyingi tu hapa nchini.
Na NDICHO KINACHOTAKIWA. Ntu Bubu!Na ili hili lifanikiwe, mikwara itaanza kama walivyomfanyia TLS mwaka jana.Mwaka huu wanaweza kujaribu hivi:
1. Kwa kuwa chama cha Wanasheria ni TANGANYIKA Law Society, basi MZANZIBARI haruhusiwi kuwa Raisi wake.
2. Ntu yeyote ambaye ni Mtoto au Mjukuu wa ALIYEWAHI kuwa Raisi wa Inji (Tanzania au Zanzibari), haruhusiwi kugombea Uraisi wa TLS.
3. Ntu yeyote ALIWAHI KUISHTAKI Serkali kwenye Mahakama YOYOTE, basi si Ruhsa kugombea/kuchaguliwa kuwa Raisi wa TLS.
4. Uraisi wa TLS ni MAPOKEZANO kati ya Mawakili Binafsi na Wale wa Serkali.
Na akishapita Wakili wa Serkali, basi uchaguzi wa TLS utafanyika baada ya MIAKA SABA!
Tusubirie VIKWAZO Kwa Fatma.....
 
FB_IMG_1522087473507.jpeg
huyu anafaa sana ni jasiri
 
Kura zote kwa dada yetu Fatma TLS members please!
Kama tunataka kazi ngumu ikamilishwe kwa kipindi hiki mpeni huyu jembe!
Smart, strong and professional
Let's ChangeTanzania

Nina sababu maana huyu ataendeleza gurudumu la kuyasema mambo muhimu,

Pia ni zamu ya wanawake

Pia ni zamu ya Zanzibar

Swali dogo tu linanichanganya TLS si Tanganyika lawyers Society, je fatuma ameingia vipi?

FB_IMG_1522128188656.jpg
 
Kwa historia fupi tu ni kuwa Babu yake Fatma ni Rais wa kwanza wa Zanzibar na muasisi wa Muungano huu wa leo. Na Baba yake Fatma ni Rais mstaafu wa Zanzibar na ni CCM mpaka leo. Lakini Mtoto huyo wa Rais anapingana uongozi wa Rais Magufuli na chama cha Baba yake mzazi kutokana na ukiukwaji wa Katiba unaofanya na awamu hii. kama humjui Babu yake hebu toa mia mbili hapo utamuona. Iweje wewe ambae mtu wa vijijini uwe mzalendo wa kusifia maovu bila ya aibu wakati watoto waliozaliwa Ikulu wanakemea??
IMG-20180327-WA0056.jpg
 
Back
Top Bottom