Fatuma Karume: Mwambieni Ndugai Kanuni za Bunge si Sheria za Nchi, hazituhusu sisi

Shujaa Mwendazake

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
3,735
6,291
Swali kwa Job:

Kwani Wanahabari ni Wabunge mpaka uwapeleke kwenye Kamati ya Maadili ya Bunge?

Ushauri wangu ni:
Job soma kanuni ya 2 ya Kanuni za Bunge. Kanuni zenu zinatumika kuendesha Bunge na si NCHI. Hazituhusu sisi. Si SHERIA za Nchi.

Bunge si Mahakama. Halina MAMLAKA la kumuhukumu mtu yeyote. Job anataka kuingilia MAMLAKA ya Mahakama. Kama wanahabari wamevunja SHERIA awapeleka Mahakamani. Kanuni za Maadili za Bunge hawezi kuzitumia kuwahukumu wanahabari. Bunge si MAHAKAMA!"

Wakili msomi Fatma Karume

E4vDRXeWYAEbU1_.jpg
 
Kama kwenye maswala madogo hivi hayafuatwi kisheria, basi kuna kanuni pia zinakiukwa sana hasa bunge lile lilopita lenye wapinzani
 
Katika watu wa hovyo wasiostahili nafasi ya uongozi popote, huyu Ndugai ndiye namba moja.

Huko bungeni inafaa waanze kumshughulikia na kumtoa kwenye nafasi hiyo. Kinga aliyokuwa akiitegemea sasa haipo, ya nini kuendelea kuaibisha bunge letu na mtu asiyekuwa na sifa za uongozi kama huyo abaki kuwa spika wake?

Bado anatishia watu na vyombo vya habari na vikamati vyake utadhani na yeye ana mabunduki ya kwenda kuwatishia hao anaowalaumu kwa kumpa ukweli juu ya udhaifu wake mkubwa kiuongozi.
 
Paschal Mayala aliwahi kuitwa kwenye kamati kwani alikua Mbunge?

CAG aliwahi kuitwa kwenye kamati, kwani yeye alikua mbunge?

Fatuma aache kujibu hoja kimipasho, ajibu kama mtaalamu wa sheria, je kisheria bunge linaweza kumuita nani na nani kwenye makati ama hawaruhusiwi kumuita mtu yoyote asie mbunge kwenye kamati.

Sasa kumwambia Ndugai asome kifungu gani inatusaidia nini sisi tusieolewa sheria?
 
Amekuwekea attachment isome vizuri
 
Zilikuwa enzi za jiwe na job ulikuwa ni mmoja wa mikono miovu ya jiwe.

Back
Top Bottom