Fatuma Karume muombe radhi Prof. Abdirazak Gurnar kwa niaba ya Mzee Karume

Ni mwanaharakati lazima azungumzie na hayo yaliyofanywa na baby yake
Mtoto haukumiwi kwa kosa Baba ,na Baba pia la mtoto. Huwezi kufanyia kosa wewe radhi nikaomba Mimi ,radhi haina niaba isipokuwa uwe mmoja wa watenda kosa uombe radhi kwa kuwakilisha na wenzako pia
 
Ndugu zangu,

Huu ni wito kwa "mwanaharakati" na "mtetezi wa haki za binadamu" kupaza sauti na kumuomba radhi Prof. Abdirazak Gurnar na wengine ambao waligeuka wakimbizi kutokana na siasa za Mzee Karume.

Uungwana ni vitendo, upendo huanzia nyumbani. Fatuma Karume aka shangazi kwenye hili umekuwa kimya sana. Toa tamko la kuomba radhi.
Baba zake Fatma bado wapo hivyo mjukuu hawezi kufanya jambo la kifamilia wakati mababa wapo, hivyo licha ya kuwa hoja yako haina mashiko hata hivyo hilo kiafrika haliwezekani.
 
Yaani Fatuma Karume aombe radhi kwa mambo aliyofanya babu yake akiwa Rais... kwani Fatuma ni Rais?
 
Yeye ni mwanaharakati wa haki za binadamu angelaani ya babu na Baba kwanza
Baba zake Fatma bado wapo hivyo mjukuu hawezi kufanya jambo la kifamilia wakati mababa wapo, hivyo licha ya kuwa hoja yako haina mashiko hata hivyo hilo kiafrika haliwezekani.
 
Ndugu zangu,

Huu ni wito kwa "mwanaharakati" na "mtetezi wa haki za binadamu" kupaza sauti na kumuomba radhi Prof. Abdirazak Gurnar na wengine ambao waligeuka wakimbizi kutokana na siasa za Mzee Karume.

Uungwana ni vitendo, upendo huanzia nyumbani. Fatuma Karume aka shangazi kwenye hili umekuwa kimya sana. Toa tamko la kuomba radhi.
Wa kuomba radhi hasa ni Tanganyika iliyomweka Karume Rais kwani iliivamia Zanzibar tokea wakati huo na kila uchafuzi unaoitwa uchaguzi huletewa askari wa kuja kutumwagia marisasi , kututandika viboko , lengo lenu ni kutulazimisha tuwe watanganyika kwa jina la Tanzania .
 
Hii comment aione Lissu kisha awashukuru wasiojulikana
Huyo jamaa Kama asingekimbia na kwenda huko UK asingekuwa Prof na asingeshinda hiyo tuzo.

Yeye ndio anatakiwa ashukuru, kuna jamaa nawafahamu walikimbia Zanzibar 2001 wakahamia UK wanashukuru Sana kwani maisha yao yapo safi sana wangekuwa Zanzibar wangekuwa wala urojo tu
 
..Prof.Abdulrazak anatakiwa kuombwa radhi ya Serikali ya Mapinduzi Znz / SMZ.

..unyama uliomfanya Abdulrazak na wengine waikimbie Znz ulifanywa na vyombo vya DOLA vya serikali ya mapinduzi.

Hivi jeshi na polisi na uhamiaji havimo kwenye huu Uvamizi unaoitwa Muungano ??

By the way hivi nani aliwaleta Zanzibar wale wanajeshi wa Burundi kwenye uchaguzi wa Oct. 2020 ?? na wale wanajeshi waliozingira Hoteli ya Bwawani 2015 na kumlazimisha Jecha kufuta uchaguzi / Uchafuzi??
 
Basi yawapasa CCM watambae kabisa kuomba msamaha,pia Dr Mwinyi naye afanye hivyo hivyo maana naye ni mnufaika Wa huo udhalimu!
Mwinyi , kijana wa Mkuranga huyu yumo kazini kuendeleza uvamizi , hana jipya
 
Basi yawapasa CCM watambae kabisa kuomba msamaha,pia Dr Mwinyi naye afanye hivyo hivyo maana naye ni mnufaika Wa huo udhalimu!
Dr. Mwinyi is one of them. Hajawahi kuwakana. Fatuma Karume ni mnufaika wa udhalimu ambaye leo anataka kujifanya mtu mwema.
 
Dr. Mwinyi is one of them. Hajawahi kuwakana. Fatuma Karume ni mnufaika wa udhalimu ambaye leo anataka kujifanya mtu mwema.
Ni MTU mwema ndiyo kwasababu hakushiriki udhalimu huo!Ni upuuzi kumuhukumu kwa makosa ya Babu yake na viongozi wa CCM!
Juzi tu hapa Mzee Amani amehojiwa kuhusu Fatma kuwa kinyume na serikali ya CCM,Mzee akasema huwezi kuingilia maamuzi ya Fatma kwani ni mtu mzima na anayo haki ya kufanya atakacho!
Sasa kumtwisha zigo si sawa,ni sawa leo tuanze kutafuta watoto Wa JPM na tuwahukumu kwa vitendo viovu vya baba yao,si sawa!
 
Ndugu zangu,

Huu ni wito kwa "mwanaharakati" na "mtetezi wa haki za binadamu" kupaza sauti na kumuomba radhi Prof. Abdirazak Gurnar na wengine ambao waligeuka wakimbizi kutokana na siasa za Mzee Karume.

Uungwana ni vitendo, upendo huanzia nyumbani. Fatuma Karume aka shangazi kwenye hili umekuwa kimya sana. Toa tamko la kuomba radhi.
Mkuu Wakudadavuwa, usimbebeshe mtoto wa watu mizigo isiyo ya kwake, hakuna mtu yoyote aliyefukuzwa Zanzibar, kila aliyeikimbia Zanzibar baada ya yale Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, aliondoka kwa hiyari yake, hivyo wala hakuna hitaji lolote, la kuombwa msamaha kwa mkimbizi yoyote.

P
 
Back
Top Bottom