Fatuma Karume kumfananisha Rais na kinyago ni sahihi?

YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
36,909
51,904
Akizunguzma na waandishi wa wahabari mahakamani Kisutu, Fatuma Karume kasema kuna msemo wa kiswahili unaosema kuwa " kinyago ulichochonga mwenyewe hakitakiwi kukusumbua"

AKAENDELEA kusema kuwa Rais MAGUFULI sisi ndio tuliomchagua na kumuweka.

Kwa hiyo anamfananisha Rais na kinyago cha kuchonga kuwa wananchi ndio waliochonga hicho kinyago?

Huyu MZANZIBARI kwenye hicho alichoongea inabidi achukuliwe hatua sio sawa.

Ushahidi huo hapo

 
Akizunguzma na waandishi wa wahabari mahakamani kisutu fatuma karume kasema kuna msemo wa kiswahili unaosema kuwa " kinyago ulichochonga mwenyewe hakitakiwi kukusumbua" AKAENDELEA kusema kuwa Raisi MAGUFULI sisi ndio tuliomchagua na kumuweka.Kwa hiyo anamfananisha raisi na kinyago cha kuchonga kuwa wananchi ndio waliochonga hicho kinyago?

hUYU MZANZIBARI kwenye hicho alichoongea inabidi achukuliwe hatua sio sawa

ushahidi huo hapo


That is what we call silent language
 
..Fatuma karume kasema kuna msemo wa kiswahili unaosema kuwa " kinyago ulichochonga mwenyewe hakitakiwi kukusumbua"

Mbunge yule standard 7 B aliwahi kutamka maneno hayahaya, akimaanisha kwamba Magufuli kawekwa pale na wanaCCM na hapaswi sasa kuanza kuwatisha/au wanachama kumuogopa. Hayana shida haya maneno, ndio maana Msukuma hakuitwa ili apimwe mkojo.
 
Hakuna tatizo lolote hapo.
Huo ni msemo wa wahenga wa kiswahili, na wahenga waliutunga kwa manufaa yetu sote, hivyo tuutumie tu kila inapobidi.
Ni msemo mzuri sana, tena ukizingatia rais wetu anapenda lugha ya kiswahili kuliko lugha za kigeni, hata yeye anaupenda.
 
Akizunguzma na waandishi wa wahabari mahakamani kisutu fatuma karume kasema kuna msemo wa kiswahili unaosema kuwa " kinyago ulichochonga mwenyewe hakitakiwi kukusumbua" AKAENDELEA kusema kuwa Raisi MAGUFULI sisi ndio tuliomchagua na kumuweka.Kwa hiyo anamfananisha raisi na kinyago cha kuchonga kuwa wananchi ndio waliochonga hicho kinyago?

hUYU MZANZIBARI kwenye hicho alichoongea inabidi achukuliwe hatua sio sawa

ushahidi huo hapo


Ukikataza wananchi kumsema rais kwa bezo na kejeli (Fatma Karume hata hajafika huko, katumia tafsida tu), umewaruhusu wampige risasi huyo rais na kumpindua katika mapinduzi ya kijeshi.

It is as simple as that.

The probability of a military revolution in any country is inversely proportional to the freedom to satirize the head of state.

The more you have freedom to satirize the president,the less you have the probability of a military revolution.

Chukua Marekani na Burundi kama mifano utaona hilo.

Watu wastaarabu huwa hatupinduani kwa kupigana risasi katika mapinduzi ya kijeshi.

Huwa tunapinduana kwa vijembe, kejeli, utani, misemo.

Nimempenda bure Fatma Karume.
 
Lugha ya picha tu hiyo, don't get sore..
Ila wakili naona angestick kwenye technicalities za kesi zaidi, kama mahakama au polisi wamemuoneaje mteja wake.

mambo ya Magufuli aachane nayo, maana mambo yalivyo nae tutashangaa amekamatwa kesho kwa kumkashifu rais
Hana lolote huyu wakili. Ana mihemuko sana na kwa hivyo anapoteza weledi. Afadhali angehojiwa Kibatala.
 
Back
Top Bottom