Fatuma Karume kuhusu wimbo wa taifa asema ‘Hii sio haki’

5525

JF-Expert Member
Apr 6, 2014
5,412
6,273
KANDA (1).jpg

Wakili wa kujitegemea na rais wa chama cha wanasheria Tanganyika (TLS), Fatuma Karume amelalamikia kitendo cha serikali kutoa masharti kuhusu kuimba wimbo wa taifa.

Katika ukurasa wake wa kijamii wa Twitter, Fatuma Karume ameonyesha kusikitishwa na kitendo hicho, ambapo amesema kupiga marufuku kuimbwa wimbo huo si haki.

Amendika kuwa, “Mpaka nyimbo ya taifa hatuwezi kuiimba bila ya kibali, hawa watu hawako makini, sijui hata wametoka wapi,”ameandika Fatuma Karume

Aidha, siku za hivi karibuni Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia, iliwaandikia barua wakuu wa vyuo vya ualimu, vyuo vya ufundi na maendeleo ya jamii, vyuo vikuu na vishiriki na taasisi zilizo chini ya wizara hiyo kuhusu matumizi sahihi ya rangi ya bendera na wimbo wa Taifa.

Barua hiyo iliyoandikwa Novemba 23 mwaka huu ikiwa na kumbukumbu namba CHA-56/193/02/16, ilisema wizara hiyo imepokea barua ya maelekezo kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, kuhusu matumizi sahihi ya bendera na Nembo ya Taifa, na Wimbo wa Taifa.

“Wizara ya Mambo ya Ndani inaelekeza kuwa wimbo wa Taifa utapigwa kwenye dhifa za kitaifa na endapo hadhi ya sherehe haitambuliki, taasisi italazimika kuomba kibali kwa waziri mwenye dhamana,” imeeleza sehemu ya barua hiyo,”
 
View attachment 967818

Wakili wa kujitegemea na rais wa chama cha wanasheria Tanganyika (TLS), Fatuma Karume amelalamikia kitendo cha serikali kutoa masharti kuhusu kuimba wimbo wa taifa.

Katika ukurasa wake wa kijamii wa Twitter, Fatuma Karume ameonyesha kusikitishwa na kitendo hicho, ambapo amesema kupiga marufuku kuimbwa wimbo huo si haki.

Amendika kuwa, “Mpaka nyimbo ya taifa hatuwezi kuiimba bila ya kibali, hawa watu hawako makini, sijui hata wametoka wapi,”ameandika Fatuma Karume

Aidha, siku za hivi karibuni Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia, iliwaandikia barua wakuu wa vyuo vya ualimu, vyuo vya ufundi na maendeleo ya jamii, vyuo vikuu na vishiriki na taasisi zilizo chini ya wizara hiyo kuhusu matumizi sahihi ya rangi ya bendera na wimbo wa Taifa.

Barua hiyo iliyoandikwa Novemba 23 mwaka huu ikiwa na kumbukumbu namba CHA-56/193/02/16, ilisema wizara hiyo imepokea barua ya maelekezo kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, kuhusu matumizi sahihi ya bendera na Nembo ya Taifa, na Wimbo wa Taifa.

“Wizara ya Mambo ya Ndani inaelekeza kuwa wimbo wa Taifa utapigwa kwenye dhifa za kitaifa na endapo hadhi ya sherehe haitambuliki, taasisi italazimika kuomba kibali kwa waziri mwenye dhamana,” imeeleza sehemu ya barua hiyo,”[/Q Alerts UOTE]

Naona kuna shida mahala au kuna jambo tusilolifahamu na liko njiani.
Utaifa hujengwa na mmoja za nguzo zake ni Bendera na Wimbo. Hili la kuondoa sherehe ya Uhuru tayari ni doa na bado tunaongezea lingine. Je tuko njia kuelekea kwingine ?

Wenyewe utaalamu wa sayansi ya Siasa ebu tusaidieni.
 
Halafu tunataka watu wewe wazalendo!!
Kwani imekatazwa kupigwa au kuimbwa kiholela.?? Kila siku saa 1 asbh mfano clouds wanaipiga.. Mwisho wa siku itakuwa kawaida tu ata Mond ataitumbuiza jukwaani...! Nyimbo ile inapigwa kwa heshima na ndiyo maana lazima usisame nyimbo ikiwa inaimbwa ile! Ni utambulisho pia wa taifa
 
Mtu ata akifika kuimba wimbo wa taifa huwa amejawa na shauku ya kuipenda Tz na uzalendo wa hali ya juu, ayo mambo ya kibali ndio munapoteza uzalendo kwa watu pole pole alafu badae mtakuja kudai wazalendo wa tz wako wapi? kumbe kila kitu mumefungia kabatini
 
Yaani wewe hata siku JF imepigwa pini ulipongeza ni vile kulikua hakuna jinsi ya kuweka bandiko LA kupongeza maammuzi ya TCRA

Natamani sana members wote humu wapigwe ban waachwe wanaccm peke yao kwa muda wa wiki moja nione mujadala yenu itakuweje

I second that
 
Huyu mama tokea atetee mashoga nilimuweka katika kundi la watu wasioeleweka na wasiostahili heshima sababu ya kukosa hekima.....

Sasa huyu mama kila anachokiongea nashindwa kukipokea hata kama yupo sahihi ila najikuta siwezi pokea maoni yake sababu ni tatizo....
 
Mimi nilifikiri ni kutujenga kiuzalendo zaidi hasa kwa vijana kwa kuruhusiwa kuimba wimbo wa Taifa.
 
Kuna madhara gani watoto shuleni wakiimba huo wimbo wakati wa parade la asubuhi? Nakumbuka enzi zile za mwalimu tulikuwaa tukiimba kila Monday kabla walimu hawajapita kucheki kama kaptula imenyooka, nywele zipo safi na kucha zimekatwa. Yaani hili nalo linahitaji kibali?
 
Watoto wetu watakuwa bila kujua kuimba national anthem.

Ngoja tuone mwisho wake.

Halafu hii issue ya bendera kuwa na rangi ya gold badala ya njano ambayo tulifundishwa sisi tangu primary mpaka secondary imekaaje mbona inavuruga akili zetu wahenga.
 
Back
Top Bottom