Fatma Karume Kumrithi Tundu Lissu?

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Apr 29, 2016
20,744
25,445
karumeee.jpg
WAKILI wa kujitegemea, Fatma Karume, amejitosa kumrithi Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu kwa kugombea urais wa Chama cha Mawakili wa Tanganyika (TLS), utakaofanyika Aprili 14, mwaka huu.

Lissu aliteuliwa kugombea nafasi hiyo lakini ameshindwa kukidhi matakwa ya kamati kutokana na fomu ya uteuzi iliyowasilishwa kwa sekretarieti hiyo kwani kwa mujibu wa sheria mpya, kifungu cha nane cha sheria hiyo, kinamzuia mtu ambaye ni kiongozi wa chama chochote cha siasa, kuongoza chama hicho.

Fatma atachuana na Godwin Mwapongo, Godfrey Wasonga na Godwin Ngwilimi, nafasi ya makamu wa rais atagombea Rugemeleza Nshalla pekee na mgombea wa nafasi ya Mweka Hazina atakuwa ni Sadock Magai.

Mwenyekiti wa Kamati ya Uteuzi wa chama hicho, Dkt. Kibuta Ongwamuhana amesema uchaguzi wa rais utatanguliwa na viongozi wa kanda utakaofanyika kila mkoa kuanzia Machi 27, mwaka huu.

Wakizungumzia uchaguzi huo baadhi ya mawakili wamesema wanamtabiria Fatma ushindi wa kishindo kutokana na kuwa na kaliba inayofanana na Lissu.
 
Tunamuombe Sana
Karume maana ndiye mwanaharakati pekee ambaye yupo hapo kama mtetezi Wa haki za wananchi wanyonge, najua shida IPO sana lakini naamini kule ni wasomi na wenye akili wote, sio Wa kuhongwa pesa ni watu Wa maamuzi naipenda sana hii sehemu maana mdipo haki ilipo
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom