Fatma Karume asimamishwa kufanya kazi za Uwakili Tanzania Bara kwa kosa la kuishambulia ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali(AG)

Papaa Mobimba

JF-Expert Member
Jan 27, 2018
752
3,092
Wakili Fatma Karume amesimamishwa kufanya kazi za Uwakili Tanzania Bara, Maamuzi hayo yametolewa na Jaji Feleshi kwenye kesi iliyofunguliwa na mwanaJF Ado Shaibu akipinga uteuzi wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali(AG). Fatuma Karume amesema kuwa maamuzi hayo yametolewa bila yeye kusikilizwa.

Mahakama Kuu imeamuru Fatma apelekwe kamati ya maadili ya Mawakili kwa madai ya kushambulia ofisi ya Mwanasheria Mkuu.

Akihabarisha katika ukurusa wake wa Twitter, MwanaJF Ado Shaibu ambaye ndiye aliyefungua kesi hiyo amesema kwamba...

1. Kesi yangu dhidi ya Rais Magufuli imeondolewa "struck out" kwa kumjumuisha Mh. "John Pombe Magufuli". Wakili wangu Fatma Karume atafafanua.

2. Wakili Fatma Karume amesimamishwa (suspended) uwakili kwa maneno yake kwenye "submission" ya kutetea kesi yangu.


Pia, mwanaharakati na mwanaJF Suphian Juma amenena haya kuhusu Fatma Karume kusimamishwa Uwakili

''Kitendo cha Fatma Karume kusimamishwa uwakili kisa tu anaisimamia kesi ya Kikatiba ya
Ado Shaibu dhidi ya Rais Magufuli kumteua AG kimakosa, ni ishara kwamba muhimili wa Mahakama unazidi kugeuzwa kuwa tawi la Serikali. Na hii ni kutulaghai kwamba Rais yupo juu ya Sheria, #Ushamba''



Karume.PNG

Pia soma
tapatalk_1569137348166.jpeg
tapatalk_1569137351630.jpeg
tapatalk_1569137354595.jpeg
tapatalk_1569137572175.jpeg
 
😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂

Huu mchezo hautaki hasira. Atanyooka tu, after suspension & her advocacy will be terminated indefinitely..!! 🏃🏃 Na hatupokei msamaha ng'oo 😂😂 Asiyesikia la mkuu huvunjika guu msikilize baba yake mdogo Balozi Karume akimkanya Fatma hapa kwenye You Tube, muda tu alimkanya, hakusikia

 
Nikiwa huku kijijini nimepata habari kuwa Fatma Karume amesimamishwa Uwakili kwa muda usiojulikana.

Siku hizi za miaka ya mitandao ya kijamii inakuwa ni vigumu kujua ipi ni habari ya kweli au uongo!

Nimeona nilete hii habari hapa Jamiiforums kwa sababu ni sehemu ambayo habari za kweli hupatikana!

Naomba mwenye ukweli anipe!
ni kweli kasimamishwa furahi sasa
 
Back
Top Bottom