ACT Wazalendo
JF-Expert Member
- May 5, 2014
- 609
- 1,540
Chama cha ACT Wazalendo kimepokea kwa faraja hatua ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwanusuru Watanzania walioko nchini Ukraine nchi ambayo iko vitani na Urusi.
Taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imesema Serikali inachukua hatua za haraka kunusuru maisha ya Watanzania wapatao 300 pamoja na wanafunzi waliopo Ukraine.
Inakumbukwa kwamba likuwa ni ACT WAZALENDO iliyoibua hadharani haja na umuhimu wa Serikali kuchukua uongozi katika suala hilo la kuwachukua watanzania waliopo nchini Ukraine kwa kupitia nchi jirani.
Taarifa ya Naibu Msemaji Kivuli wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Ndugu Dahlia Majid iliyotolewa tarehe 25,Februari/ 2022 iliitaka Serikali ivae wajibu wake wa kulinda usalama wa raia wake kwa kuwaokoa Watanzania hao kwa sababu wajibu mkuu na wa kwanza kwa Serikali yoyote ni kulinda raia wake na mali zao popote walipo.
Baada ya Juhudi kubwa za Chama cha ACT Wazalendo kupitia Msemaji Wa Kisekta wa Mambo ya Nje, kuitaka Serikali ichukue hatua za makusudi kuwasaidia Watanzania Walioko Ukraine, Serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Nje imetoa taarifa na Muongozo wa namna unavyo shughulikia jambo Hilo!
Kuna taarifa kwamba kutakuwa na ndege ya ATCL itakayo kwenda kuwachukua watanzania wenzetu nchi ya Poland ,Romania na nchi zingine zinazopakana na Ukraine ambazo watanzania wapo Siku ya Tarehe 03.03. 2022.Na kuna mawasiliano yametolewa na Shirika la Ndege la Tanzania kupitia namba 0800110045 kwa mawasiliano zaidi ,hii kwetu sisi ni hatua njema.
Ila kuna changamoto ambayo ipo na tunaitaka Serikali kupitia Wizara ya mambo ya nje na Ubalozi wa Tanzania wa Poland uliopo Berlin kuchukua hatua za haraka ili kutatua changamoto hii.
Nchi ya Poland sasa inapokea watu wengi sana kutoka Ukraine,uwezo wao wa kuhudumia wote ni mgumu sana ingawa wanajitahidi sana .Na kwa kurahisisha hili ndio maana yeyoye anayeingia Poland anaulizwa mpakani kama ana ndugu wa kumpokea na atakayemsaidia na kumpa hifadhi na mahitaji.
Jambo la kuumiza watanzania wenzetu wanaoingia Poland na Romania mpakani hakuna utaratibu wowote uliowekwa na serikali yetu ya Tanzania ili kuwapokea hawa ndugu zetu aidha kuwapakia katika usafiri na kuwapa sehemu ya hifadhi na mahitaji yote hakuna utaratibu, watanzania wenzetu wanaoingia mpakani wanateseka hakuna utaratibu wowote uliowekwa.
Hivyo basi,tunashauri serikali ya Tanzania kupitia wizara ya mambo ya nje na Ubalozi wa Tanzania Poland uliopo Berlin iweke utaratibu wa haraka wa kuwapokea watanzania wanaoingia Poland na nchi zingine kama Romania ili kuwapa usafiri, hifadhi ya malazi,chakula na mahitaji ya msingi katika kipindi hiki ambacho serikali inajiandaa kwenda kuwachukua.
Lakini pia serikali iwasiliane na nchi za Afrika Mashariki na nchi kadhaa za Afrika ambazo nazo zinapokea watu wao ili pia wawapokee Watanzania popote wawaonapo na kuwapa hifadhi watanzania watakaopokelewa hapo mpakani kabla ya kuchukuliwa na kuletwa Tanzania.
ACT Wazalendo itaendelea kuwa sauti mbadala kwa kuwasema Watanzania katika masuala mbali mbali ya kisiasa, kijamii na kiuchumi
Fatma Fereji
Msemaji wa Kisekta wa Mambo wa Nje.
+255 777 424 390
28/03/2022