Fathers day inakaribia... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Fathers day inakaribia...

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Kwame Nkrumah, May 23, 2009.

 1. K

  Kwame Nkrumah JF-Expert Member

  #1
  May 23, 2009
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 887
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45
  Siku ya akina Mama imepita na sasa siku ya akina Baba inakuja. Tukumbushane mambo mazuri uliyotendewa na mzee that made you such a lady/gentleman that you are today.
  Tukumbushane pia nicknames na majina tunayowaita wazee wetu, Dad, Baba, Mshua, Dingi ,Mkurugenzi, Jerumani [ jirani yetu walikuwa wanamuita baba yao hivyo kwa sababu alikuwa mkali sana ] n.k . Baba yako mlikuwa mnamuitaje?
  Wengi wetu pia ni akina baba, Nini experience yako ya ubaba? Kipi hukutegemea katika ubaba? Kwa mlio ughaibuni mtoto wako ameishaanza kukurebisha kiingereza ? Ha haa haa... "dad it's not hOt,it's hAt"...
  Sitasahau pia stori za Dingi kwamba " Nilikuwa nakuwa wa kwanza kila mwaka darasani" au " nilikuwa na akili sana nilirushwa sana madarasa" pia "nilikuwa mwanamichezo bora sana".
  Ni wasaa pia tuwakumbuke akina baba wote waliotutangalia kwa mwaka uliopita na kuwashukuru kwa malezi mema na kuwaombea wapumzike kwa amani.
   
  Last edited: May 23, 2009
 2. Kapinga

  Kapinga JF-Expert Member

  #2
  May 23, 2009
  Joined: Nov 20, 2007
  Messages: 728
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  mimi nayokumbuka ni pale nilikuwa secondary unaomba hela ya raba mpya...unapewa story eti alikuwa anatembea peku peku kuanzia darasa la saba mpaka form 6! yani hawa wazee wetu...
   
 3. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #3
  May 23, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Sorry my Dad,

  Uliitwa mara nyingi sana shuleni kwaajili ya kuja

  kuniadhibu.

  Uliacha kazi zako just because of me....

  Iam grown up now....I did you wrong!
   
 4. K

  Kwame Nkrumah JF-Expert Member

  #4
  May 23, 2009
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 887
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45
  Du, nilifikiri nilikuwa peke yangu, mbaya zaidi ukipata suspension, unaanza kufikiria utasema nini nyumbani.
   
 5. K

  Kwame Nkrumah JF-Expert Member

  #5
  Jun 16, 2009
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 887
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45
  Sikukuu njema ya akina baba kwa akina baba wote.
   
 6. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #6
  Jun 16, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,916
  Likes Received: 216
  Trophy Points: 160
  Nakumbuka kuna siku tulikosa usafiri tukiwa na mzee wetu hivyo ikatubidi tutembee kwa miguu, sasa baada ya kutembea kamwendo fulani tukaanza kulalamika kuchoka, basi mzee akaanza kutuponda kuwa tuko legelege sana na kutupa stori walivyokuwa wadogo jinsi walivyotembea umbali mrefu tena na mizigo vichwani (si mnajua milima ya kule kwetu uchagani?) Basi baada ya kaka yangu kuona madogo yamezidi, akamwambia mzee kuwa, hata sisi tungekuwepo wakati huo tungeishi maisha hayo mliyoishi ila sasa dunia imeshabadilika na hakuna haja ya kujizoesha shida eti kwa kuwa ulishawahi kuipata. Kwa kuwa mzee naye alikuwa msanii aliishia kucheka na hapo hapo akaanzisha mada nyingine..

  Ninachokumbuka kwa Mzee wangu hajawahi kushika fimbo kunichapa and still i grew up na tabia njema kabisa. Nilichojifunza kwake ni kuwa ukali hauna masaada wowote katika malezi ya mtoto bali kumsikiliza na kumweshimu mwanao ndiyo njia pekee.

  Alikuwa anapenda kweli siasa na alikubali kukosolewa hata na sisi wanaye pindi akiteleza pia alitushirikisha kufanya maamuzi ya kifamilia tangu tupo wadogo sana na aliheshimu mtazamo wa kila mtu. Above all, hakuwa mtu wa jazba wala kukasirika, tulitaniana na mara zote tulicheka pamoja.
   
  Last edited: Jun 17, 2009
 7. M

  Mtu wa Kawaida JF-Expert Member

  #7
  Jun 16, 2009
  Joined: May 2, 2008
  Messages: 217
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Mie namkumbuka baba yangu kwa muda wake wote aliutoa kwa kipindi nilichokuwa mdogo pamoja na ndugu zangu. Manake mzee alikuwa na utaratibu wa kufatilia mambo yote ya masomo kwa watoto wake wote na mama yeye alifatilia mambo mengine katika makuzi ya watoto.

  KWani kila siku madaftari yalikaguliwa sasa kama haujaandika kitu chochote itabidi huseme kulikoni. Na alikuwa anataka afahamu ratiba yako ya masomo ya kila siku. Ukidanganya tu umekwisha manake alikuwa na mahusiano ya karibu na walimu katika shule tulizokuwa tunasoma.

  Kingine ambacho nitaendelea kumkumbuka mzee ni uwezo wake wa kucheza mpira wa mguu hijapokuwa hakuna hata mtoto wake mmoja aliyeweza kuwa mahahiri katika nyanja ya mchezo wowote kama yeye.
   
 8. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #8
  Jun 16, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Akina baba, dont miss out kwenye makuzi ya watoto wenu.Wengi waliofanikiwa ni wale baba zao waliowafuatailia kwa karibu maendeleo yao na hata kutumia kichocheo hasi au chanya kusukuma mambo yaende.

  HONGERENI WABABA WOTE (hivi wingi wa baba ni wababa? LOL).... JIVUNIENI SIKU YENU HII.
  WoS!
   
  Last edited: Jun 16, 2009
 9. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #9
  Jun 16, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Thank you thank you....

  I've got my first father-daughter dance coming up and I'm really looking forward to it...I can't wait
   
 10. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #10
  Jun 16, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  She will have unforgetable memories believe you me!
   
 11. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #11
  Jun 16, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  I'm sure she will and so will I.....
   
 12. BelindaJacob

  BelindaJacob JF-Expert Member

  #12
  Jun 16, 2009
  Joined: Nov 24, 2008
  Messages: 6,060
  Likes Received: 475
  Trophy Points: 180
  Happy Father's Day to all JF Dadies!
   
Loading...