Fastjet yaamriwa kumlipa abiria fidia ya milioni 30 kwa kuahirisha safari bila kumtaarifu

barafu

JF-Expert Member
Apr 28, 2013
6,739
32,866
image.jpeg



Dar es Salaam. Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeiamuru Kampuni ya Ndege ya Fastjet kumlipa abiria wake, John Mhozya fidia ya Sh30 milioni baada ya kushindwa kumtaarifu kuhusu kuahirishwa kwa safari yake.

Mbali na fidia hiyo ya hasara ya jumla aliyoipata abiria huyo kutokana na safari hiyo kufutwa, pia Mahakama hiyo imeiamuru kampuni hiyo kumrejeshea abiria huyo nauli yake ya Sh43,000 alizokuwa ameshalipa na Sh339,000 alizozitumia kwa nauli baada ya kutafuta usafiri mbadala kutoka shirika jingine la ndege.

Uamuzi huo ulitolewa juzi na Hakimu Mkazi Mkuu Kisutu, Respicius Mwijage baada ya kuridhishwa na madai ya abiria huyo katika kesi aliyoifungua mahakamani hapo ya kampuni hiyo kuvunja mkataba.

Katika kesi hiyo ya madai namba 4 ya mwaka 2013, Mhozya ambaye pia ni wakili wa kujitegemea wa Mahakama Kuu, alikuwa akiiomba Mahakama iiamuru Fastjet imlipe Sh50,000,000, ikiwa ni hasara ya jumla aliyoipata pia imrejeshee fedha zake za nauli alizokuwa ameshalipa kwa mdaiwa pamoja na nauli aliyotumia kwa usafiri mbadala.

Katika hukumu hiyo, Hakimu Mwijage alisema baada ya kupitia ushahidi wa pande zote, hakuna shaka kwamba mdai na mdaiwa waliingia mkataba baada mdai kununua tiketi ambayo iliwasilishwa mahakamani kama kielelezo.

Alisema kwa mujibu wa mkataba huo, mdai alipaswa kusafiri kutoka Dar es Salaam kwenda Mwanza na kurudi na kwamba kwa mujibu wa tiketi hiyo, mdaiwa alikuwa na wajibu wa kuwasiliana na mdai saa tatu kabla kuhusu kufutwa kwa safari.

Katika utetezi wake, mdaiwa kupitia kwa Ofisa Uhusiano na Ofisa Mtendaji, Lucy Mbogoro alidai kuwa baada ya kufuta safari walimtafuta mdai lakini simu yake ilikuwa haipatikani.

Hata hivyo, Hakimu Mwijage katika hukumu yake alisema hakuna ushahidi wowote uliowasilishwa mahakamani kuonyesha kuwa baada ya kufuta safari walimtaarifu mdai kwa wakati kama inavyotakiwa kwenye tiketi.

“Mdaiwa hakujaribu hata kumleta shahidi kutoka kampuni ya huduma za simu za mikononi kuthibitisha madai yake kwamba siku hiyo mdai alipigiwa simu lakini hakupatikana,” alisema Hakimu Mwijage.

Licha ya mdai kueleza kuwa kufutwa kwa safari hiyo kulisababisha usumbufu katika kuhudhuria kesi za wateja wake na vikao muhimu, Mahakama ilisema fidia ya Sh50 milioni aliyoomba ni kubwa.

Chanzo: MWANANCHI
 
Kuna likampuni linaitwa precision niliapa kutopanda ndege zao labda km naumwa napandishwa sijielewi. Walinicost laki 4 ya ziada coz two consecutive days nafika airport wanghair safari. Sijui kwa nn sikupata hii akili
 
na mashirika ya nje je naweza kufungua kesi? maana hawa Ethiopan airline kama mara 3 walishakatisha safari zangu bila sababu na bila kunitaarifu,
 
HII NIMEIPENDA

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeiamuru Kampuni ya Ndege ya Fastjet kumlipa abiria wake, John Mhozya fidia ya Sh30 milioni baada ya kushindwa kumtaarifu kuhusu kuahirishwa kwa safari yake.

Mbali na fidia hiyo ya hasara ya jumla aliyoipata abiria huyo kutokana na safari hiyo kufutwa, pia Mahakama hiyo imeiamuru kampuni hiyo kumrejeshea abiria huyo nauli yake ya Sh43,000 alizokuwa ameshalipa na Sh339,000 alizozitumia kwa nauli baada ya kutafuta usafiri mbadala kutoka shirika jingine la ndege

Chanzo : Mwananchi
 
ndo maana siku hizi hata kukiwa na mabadiliko ya time hata ile nusu saa wanakupigia kumbe washapewa somo
 
Watanzania wa leo si wale mwaka 47 watu wanatambua haki zao na ule woga wa kudai haki unazidi kupungua...
 
Si jambo jema kukejel maoni ya mwenzako tena kwa matusi tuwe wastaarabu jamani.
 
HII NIMEIPENDA

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeiamuru Kampuni ya Ndege ya Fastjet kumlipa abiria wake, John Mhozya fidia ya Sh30 milioni baada ya kushindwa kumtaarifu kuhusu kuahirishwa kwa safari yake.

Mbali na fidia hiyo ya hasara ya jumla aliyoipata abiria huyo kutokana na safari hiyo kufutwa, pia Mahakama hiyo imeiamuru kampuni hiyo kumrejeshea abiria huyo nauli yake ya Sh43,000 alizokuwa ameshalipa na Sh339,000 alizozitumia kwa nauli baada ya kutafuta usafiri mbadala kutoka shirika jingine la ndege

Chanzo : Mwananchi
Hivi hicho kiwango cha fidia kinafikiwaje na mahakama na justification ya hasara aliyopata huyo abiria inafanyikaje?
 
Hongera sana wakili wangu Mhozya, haya mashirika yamekuwa yakifanya kazi kienyeji mno. I hope wafanyakazi watajifunza kuwajibika.
 
Aise amenifumbua macho. Precision Air is the worse. Mwanza- Bukoba safari inaweza ikaahirishwa hata kwa siku tatu. Mwaka 2013 nilisafiri kwa basi kutoka Morogoro hadi Arusha kwa basi nikawahi Ndege ya precision iliyokuwa isafiri kutokea Dar Arusha ( departure time saa saba mchana.) Ndege ilifika saa 6 usiku.
Namuunga mkono huyo wakili. Suala la huduma kwa wateja bado ni tatizo sana.
 
Safi sana.... Hawa jamaa wa Fastjet pamoja na mazuri yao, wana tatizo la kutotoa taarifa ya kuahirisha safari......wakati wewe ukichelewa tu kucheckin wanafunga kupokea wasafiri 40 Min kabla ya kuanza safari!!!!
 
Back
Top Bottom