Fastjet wazuiwa kuingiza ndege mpya. Wanyimwa vibali, watakiwa kuondoka

  • Thread starter Return Of Undertaker
  • Start date

Return Of Undertaker

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Joined
Jun 12, 2012
Messages
3,631
Points
2,000
Return Of Undertaker

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Joined Jun 12, 2012
3,631 2,000
Leo katika amka na BBC mmiliki wa ndege za Fastjet Masha ambaye ni kada wa CCM kwa sasa amelia na mamlaka za anga Tanzania kwa kunyimwa vibali vya kuingiza ndege mpya.

Pamoja na katazo hilo kapewa makavu live kuwa wafungashe kwa sasa ATCL ndio shirika pekee litakalopewa safari zilizokuwa zikifanywa na Fastjet.

_—------------_------------

Mwenyekiti mtendaji wa Shirika la Ndege la Fastjet Tanzania, Lawrance Masha amesema Serikali imemzuia kuingiza ndege za shirika hilo nchini humo.

Waziri huyo wa zamani wa Mambo ya Ndani ametoa kauli hiyo leo Jumatano Desemba 26, 2018 wakati akizungumza na Mwananchi, kubainisha kuwa ana matumaini kuwa baada ya kumalizika kwa sikukuu ya Krismasi huenda mambo yakawa mazuri.

Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Hamza Johari amesema kesho atazungumza na waandishi wa habari ili kufafanua yote yanayoendelea baina ya mamlaka hiyo na Fastjet.

Katika maelezo yake Masha amesema Serikali haimpi ushirikiano wa kutosha katika mkakati wake wa kulifufua Shirika la Fastjet.

Amesema wamemzuia kuingiza ndege aina ya Boeing 737-500 baada ya iliyokuwepo kuzuiliwa kuruka kwa madai kuwa inapata hitilafu mara kwa mara na shirika halina meneja mwajibikaji.

Desemba 19, 2018 akizungumza katika kipindi cha 360 kinachorushwa na televisheni ya Clouds, Masha alisema ndege hiyo ingewasili Tanzania Jumamosi iliyopita Desemba 22, 2018 lakini hadi leo saa sita mchana ndege hiyo ilikuwa haijafika.

Leo amebainisha kuwa ikiwa ataruhusiwa ndege hiyo itafika Tanzania ndani ya muda mfupi kwa maelezo kuwa kila kitu kipo tayari, “safari kutoka Afrika Kusini ilipo hiyo ndege hadi Tanzania ni mwendo wa masaa matatu tu.”

Amesema ndege iliyozuiwa ilikuwa imelipiwa tayari kwa kuruka ikiwa na wafanyakazi wote, hivyo kitendo cha kuizuia ni hasara.
“TCAA inasema ili niweze kuingiza ndege hiyo nimalize kwanza madeni yote, baadhi ya madeni tayari yamelipwa na Fastjet Plc mengine Fastjet Tanzania,” amesema.

“Tayari tumemaliza lakini fedha imeisha, kwa kuwa tayari fedha nyingine tulizitumia kutimiza matakwa yao, wangeniruhusu nifanye kazi ili nipate fedha ya kulipa yaliyobaki.”

Mawazo yangu:

1. Tunasema wawekezaji kwa mpango huu hata waliopo wanapata picha gani?

2. Mnasema kujiajiri kwa hali hii nani atajiajiri?

3. Hivi mnapouwa ushindani na kutengeneza monopoly ndio kukuza uchumi?

4. Ni biashara ngapi mmeziuwa kisiasa kufurahishana nyie na sio taifa?
 
Nyani Ngabu

Nyani Ngabu

Platinum Member
Joined
May 15, 2006
Messages
82,379
Points
2,000
Age
29
Nyani Ngabu

Nyani Ngabu

Platinum Member
Joined May 15, 2006
82,379 2,000
Ningependa pia kusikia taarifa za upande wa pili!

Ila kama anachofanyiwa huyo Masha na hiyo Fastjet yake ni hila za ki biashara, basi si vizuri hata kidogo.

Uhodhi katika biashara ni jambo baya sana.

Sasa hivi tayari athari za huo uhodhi zimeshaanza kuonekana.

Bei za tiketi za ATCL zipo juu mno kuliko kawaida.

Wasipojiangalia hao ATCL wataishia kufanya vibaya mno kwenye hiyo biashara ya usafiri wa anga!

Nani atalipa laki 4 kwa safari moja ya ndege wakati kuna mabasi ya elfu 50!!??

Serikali ingeachana kabisa na haya mambo ya kufanya biashara.

Yenyewe ingejikita tu katika kutengeneza mazingira mazuri ya kufanyia biashara na yanayovutia wawekezaji zaidi.

Bado ningependa kusikia na upande wa pili kuhusu hili suala.
 
rikiboy

rikiboy

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2017
Messages
8,198
Points
2,000
Age
41
rikiboy

rikiboy

JF-Expert Member
Joined Feb 19, 2017
8,198 2,000
Toka siku ilee Tamko limetoka nikajua kabisa Hii ni Hujumaaa na Fitina za wazi dhidi ya Fastjet.. Lakini ATCL kwa hiyo tamaa waliyoonyesha wakidhani kuwafukuza Fastjet watapata wateja inaweza kuwa Ndo downfall ya ATCL na hizo faida za Bil 28 sijui danganya toto tu wanatuona sisi mafala sijui...

ATCL HAITABAKI SALAMAAA...
 
Mshana Jr

Mshana Jr

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Messages
110,223
Points
2,000
Mshana Jr

Mshana Jr

JF-Expert Member
Joined Aug 19, 2012
110,223 2,000
Leo katika amka na BBC mmiliki wa ndege za fast jet Masha ambaye ni kada wa ccm kwa sasa amelia na mamlaka za anga Tanzania kwa kunyimwa vibali vya kuingiza ndege mpya.

Pamoja na katazo hilo kapewa makavu live kuwa wafungashe kwa sasa ATCL ndio shirika pekee litakalopewa safari zilizokuwa zikifanywa na fast jet.

Mawazo yangu.

1. Tunasema wawekezaji kwa mpango huu hata waliopo wanapata picha gani?

2. Mnasema kujiajiri kwa hali hii nani atajiajiri?

3. Hivi mnapouwa ushindani na kutengeneza monopoly ndio kukuza uchumi?

4. Ni biashara ngapi mmeziuwa kisiasa kufurahishana nyie na sio taifa?
Let Masha learn it a hard way... Inajulikana wazi yupo kwenye siasa kimaslahi halafu wamekutana sasa....
 
Nyasirori

Nyasirori

JF-Expert Member
Joined
May 3, 2009
Messages
264
Points
500
Nyasirori

Nyasirori

JF-Expert Member
Joined May 3, 2009
264 500
Leo katika amka na BBC mmiliki wa ndege za fast jet Masha ambaye ni kada wa ccm kwa sasa amelia na mamlaka za anga Tanzania kwa kunyimwa vibali vya kuingiza ndege mpya.

Pamoja na katazo hilo kapewa makavu live kuwa wafungashe kwa sasa ATCL ndio shirika pekee litakalopewa safari zilizokuwa zikifanywa na fast jet.

Mawazo yangu.

1. Tunasema wawekezaji kwa mpango huu hata waliopo wanapata picha gani?

2. Mnasema kujiajiri kwa hali hii nani atajiajiri?

3. Hivi mnapouwa ushindani na kutengeneza monopoly ndio kukuza uchumi?

4. Ni biashara ngapi mmeziuwa kisiasa kufurahishana nyie na sio taifa?
Ukiachana na ushindani, tunahitaji kodi. Tutapataje kodi kama tunaondoa wawekezaji? Tungeacha siasa kwa masilahi binafsi na tukajenga nchi yetu.
 
Nyani Ngabu

Nyani Ngabu

Platinum Member
Joined
May 15, 2006
Messages
82,379
Points
2,000
Age
29
Nyani Ngabu

Nyani Ngabu

Platinum Member
Joined May 15, 2006
82,379 2,000
Oneni hii one-way ticket price ya ATCL...

3b00ded7-7784-43f9-8210-85d49cd3463d-png.977480


How this is going to be sustainable long term is beyond me!!!

One-way ticket for over 300K!!??

Maybe I’m out of touch here....but it sure looks like it’s too much money.
 
M

Mkirindi

JF-Expert Member
Joined
Mar 2, 2011
Messages
4,815
Points
2,000
M

Mkirindi

JF-Expert Member
Joined Mar 2, 2011
4,815 2,000
IKIWA HIZI HABARI ZINA UKWELI WOWOTE, THIS IS NOT ACCEPTABLE AT ALL, NI DHULMA NA UHASIDI. UWANJA WA BIASHARA LAZIMA UWE WAZI, WATU WASHINDANE NA WATANZANIA WAPATE HUDUMA SAFI NA RAHISI.

HII INAMAANISHA SEREKALI IMEAMUA KULIFUFUA SHIRIKA LA NDEGE NA IMENUNUA HIZO NDEGE, WAKIZINGATIA KUWAFUNGIA BIASHARA WASHINDANI, TUSIJIDANGANYE, TUTARUDIA PALEPALE ENZI YA NYERERE, ALIFANYA HIVYO NA AKIFELI VIBAYA SANA, HATA HAYATI MWENYEWE ALIKIRI.

UJAMAA UMESHINDWA KUFANYA KAZI ULIMWENGUNI, UMESHINDWA CHINA, SOVIET UNION, EASTER EUROPE, ASIA, SOUTH AMERICA.

SIJUI PENGINE HUYU MHESHIMIWA RAISI WETU KAJA NA MAZINGAUMBWE MENGINE.
 

Forum statistics

Threads 1,293,776
Members 497,735
Posts 31,153,158
Top