Faru wa JK wang’oa vigogo maliasili

MARA YA KWANZANZA KABISA WALIPOLETWA WATAALAM WA UHUFADHI WALIOMBWA WAPENDEKEZE NI WAPI WAWEKWE...WALIPENDEKEZA KATIKATI YA HIFADHI KWANI ITAKUWA NI VIGUMU KWA MAJANGILI KUPENYA NA KUHATARISHA MAISHA YAO..LAKINI SEREIKALI YETU ILIVO YA KINAFIKI..IKAWAPELEKA KULEE GURUMETI AMBAPO NI SEHEMU KARIBU NA VIJIJI VINGI VINAVYOZUNGUKA HIFADHI NA MIMI KAMA MHIFADHI WA ULINZI NINAJUA VIJIJI HIVO NI VIJIJI VYA MAJANGILI, CHAKUSHANGAZA NI KUWA SIJUI SERIKALI ILIKUWA INAOMBA USHAURI WA NINI MWANZONI WAKATI HAWATAKI KUFATA MAELEKEZO YA WAHIFADHI,NA HILI TUMEGUNDUA WANAPUUZA USHAURI HUKU WAKIFATA MASILAHI (INTEREST) ZA WALE MABWANA WENYE MAHOTELI MAARUFU YA KIFAHARI KULE GURUMETI..,ILI WAWAFANYIE BIASHARA ZAO KWA WATALII WAO...,KAMA MNAKUMBUKA SERIKALI ILIPUUZA USHAURI WA WATAALAM KUHUSU UJENZI WA SOPA LODGE TARANGIRE,SOPA LODGE NGORONGORO KWENYE UKUTA WA KRETA...HAYA MAMBO YAMEKUWA YAKIJITOKEZA SASA NA MADHARA YAKE NDO TUNAYAONA SASA..... HIVO MNATAKIWA MJUE KUWA SERIKALI HII HAIKO RADHI KUFATA USHAURI WA WASOMI WAKE..AMABAO WENGI WAO ILIWASOMESHA WAO ILI WAISAIDIE NCHI YAO LAKINI NDO HALI HALISI SASA ILIVO..... MWISHO WA YOTE NATAKA NITAHADHARISHE KUWA ITAKUJA KUBAKI HISTORIA TUU KWA WANYAMA WETU KWAMBA WALIKUWEPO.. (KWA KWELI SIASA NA UHIFADHI NI KAMA NYOTA NA BAHARI)kagasheki atakiwa ajue kuwa kuna hayo na ndoo aanze huko......badala ya chini[/QUOTE] Mkuu faru waliouawa sio wale walioletwa toka South Africa. Hao ni faru ambao walisalimika miaka ya nyuma wakati wa wimbi kubwa la ujangili na wako eneo linaloitwa Moru ambalo liko katikati ya hifadhi na sio Gurumet kama vyombo vya habari vinavyoeleza.
 
MARA YA KWANZANZA KABISA WALIPOLETWA WATAALAM WA UHUFADHI WALIOMBWA WAPENDEKEZE NI WAPI WAWEKWE...WALIPENDEKEZA KATIKATI YA HIFADHI KWANI ITAKUWA NI VIGUMU KWA MAJANGILI KUPENYA NA KUHATARISHA MAISHA YAO..LAKINI SEREIKALI YETU ILIVO YA KINAFIKI..IKAWAPELEKA KULEE GURUMETI AMBAPO NI SEHEMU KARIBU NA VIJIJI VINGI VINAVYOZUNGUKA HIFADHI NA MIMI KAMA MHIFADHI WA ULINZI NINAJUA VIJIJI HIVO NI VIJIJI VYA MAJANGILI, CHAKUSHANGAZA NI KUWA SIJUI SERIKALI ILIKUWA INAOMBA USHAURI WA NINI MWANZONI WAKATI HAWATAKI KUFATA MAELEKEZO YA WAHIFADHI,NA HILI TUMEGUNDUA WANAPUUZA USHAURI HUKU WAKIFATA MASILAHI (INTEREST) ZA WALE MABWANA WENYE MAHOTELI MAARUFU YA KIFAHARI KULE GURUMETI..,ILI WAWAFANYIE BIASHARA ZAO KWA WATALII WAO...,KAMA MNAKUMBUKA SERIKALI ILIPUUZA USHAURI WA WATAALAM KUHUSU UJENZI WA SOPA LODGE TARANGIRE,SOPA LODGE NGORONGORO KWENYE UKUTA WA KRETA...HAYA MAMBO YAMEKUWA YAKIJITOKEZA SASA NA MADHARA YAKE NDO TUNAYAONA SASA..... HIVO MNATAKIWA MJUE KUWA SERIKALI HII HAIKO RADHI KUFATA USHAURI WA WASOMI WAKE..AMABAO WENGI WAO ILIWASOMESHA WAO ILI WAISAIDIE NCHI YAO LAKINI NDO HALI HALISI SASA ILIVO..... MWISHO WA YOTE NATAKA NITAHADHARISHE KUWA ITAKUJA KUBAKI HISTORIA TUU KWA WANYAMA WETU KWAMBA WALIKUWEPO.. (KWA KWELI SIASA NA UHIFADHI NI KAMA NYOTA NA BAHARI)kagasheki atakiwa ajue kuwa kuna hayo na ndoo aanze huko......badala ya chini[/QUOTE]



Mkuu faru waliouawa sio wale walioletwa toka South Africa. Hao ni faru ambao walisalimika miaka ya nyuma wakati wa wimbi kubwa la ujangili na wako eneo linaloitwa Moru ambalo liko katikati ya hifadhi na sio Gurumet kama vyombo vya habari vinavyoeleza.
 
..MARA YA KWANZANZA KABISA WALIPOLETWA WATAALAM WA UHUFADHI WALIOMBWA WAPENDEKEZE NI WAPI WAWEKWE...WALIPENDEKEZA KATIKATI YA HIFADHI KWANI ITAKUWA NI VIGUMU KWA MAJANGILI KUPENYA NA KUHATARISHA MAISHA YAO..LAKINI SEREIKALI YETU ILIVO YA KINAFIKI..IKAWAPELEKA KULEE GURUMETI AMBAPO NI SEHEMU KARIBU NA VIJIJI VINGI VINAVYOZUNGUKA HIFADHI NA MIMI KAMA MHIFADHI WA ULINZI NINAJUA VIJIJI HIVO NI VIJIJI VYA MAJANGILI, CHAKUSHANGAZA NI KUWA SIJUI SERIKALI ILIKUWA INAOMBA USHAURI WA NINI MWANZONI WAKATI HAWATAKI KUFATA MAELEKEZO YA WAHIFADHI,NA HILI TUMEGUNDUA WANAPUUZA USHAURI HUKU WAKIFATA MASILAHI (INTEREST) ZA WALE MABWANA WENYE MAHOTELI MAARUFU YA KIFAHARI KULE GURUMETI..,ILI WAWAFANYIE BIASHARA ZAO KWA WATALII WAO...,KAMA MNAKUMBUKA SERIKALI ILIPUUZA USHAURI WA WATAALAM KUHUSU UJENZI WA SOPA LODGE TARANGIRE,SOPA LODGE NGORONGORO KWENYE UKUTA WA KRETA...HAYA MAMBO YAMEKUWA YAKIJITOKEZA SASA NA MADHARA YAKE NDO TUNAYAONA SASA..... HIVO MNATAKIWA MJUE KUWA SERIKALI HII HAIKO RADHI KUFATA USHAURI WA WASOMI WAKE..AMABAO WENGI WAO ILIWASOMESHA WAO ILI WAISAIDIE NCHI YAO LAKINI NDO HALI HALISI SASA ILIVO..... MWISHO WA YOTE NATAKA NITAHADHARISHE KUWA ITAKUJA KUBAKI HISTORIA TUU KWA WANYAMA WETU KWAMBA WALIKUWEPO.. (KWA KWELI SIASA NA UHIFADHI NI KAMA NYOTA NA BAHARI)kagasheki atakiwa ajue kuwa kuna hayo na ndoo aanze huko......badala ya chini

hahah,
Jana usiku niliangalia USIKU WA HABARI TBC, na mada ilikuw ani hawa FARU, na katika kusikiliza kwangu nilisikia kuwa SUNGITA GRUNEMET ni moja wa wafadhili walio dhamini changi hawa faru kuletwa nchini, Kwahiyo usishangae, MCHAGUA WIMBO, Ndiye aliyemlipa mpiga ZUMARI.
 
Mkuu faru waliouawa sio wale walioletwa toka South Africa. Hao ni faru ambao walisalimika miaka ya nyuma wakati wa wimbi kubwa la ujangili na wako eneo linaloitwa Moru ambalo liko katikati ya hifadhi na sio Gurumet kama vyombo vya habari vinavyoeleza.

Sio kweli kaka , jana TBC wamemtaja hadi jina kama sijasahau ni JOHN aliyeuwawa , na huyu ni kati ya wale watano waliotoka south africa.
 
Mkuu Maundumula sasa hao wanaoitwa game wakukamate na kakitoweo ka swala tu ndugu yangu umeisha! Kuna watu wamekula nyama ya swala ikiwa mbichi. Lakini kwa majangiri ati hawaonekani! Hawa TANAPA wana vifaa vya kisasa vya monitoring na hata ndge za patrol wanazo lakini Faru wanauawa.

Kimbunga,

Mimi naona hawa jamaa wa maliasili wamejibinafsishia hii wizara, na taasisi zake ni Bogus kabisa. Ndio maana kumbe Maige katolewa. Hawa Faru wamekufa kipindi chake nashangaa analia lia kwamba ameonewa.

Kama wanashindwa kulinda hao Faru 5 ambao rais kasema wapewe ulinzi mkali kuliko yeye mwenyewe na waziri alikuwepo na watu wake wanasikiliza je wataweza kulinda tembo 1000? JK anajitahidi sana kutengeneza hii nchi lakini watendaji wapo busy kuibomoa, pole sana rais wangu.

Nina hakika serikali ingeomba volunteers kutoka nje wa kuja kulinda hao Faru wangekuja wangefanya kazi hiyo buree bila malipo!
 
Inaaminika alikuwa anajiuliza aanzie wapi maana anaweza kufukuza wote akaishia kujifukuza yeye mwenyewe jinsi maliasili ilivyoooza
 
Ndahani,

Hivi huwezi kufuta watu wote kazi wizarani ukatangaza upya nafasi zao na wale wa zamani ukawapa ruksa kuomba?
 
Ndahani,

Hivi huwezi kufuta watu wote kazi wizarani ukatangaza upya nafasi zao na wale wa zamani ukawapa ruksa kuomba?

That is possible...tatizo lake sasa ni kwamba nafasi zinatolewa kwa interest za groups. Inamaana ukiondoa mtu group fulani linaweza kukosa ulaji. Ndo mana kuondoana kazini inakuwa ngumu sana hasa kama umewekwa kwa interest fulani fulani hivi
 
That is possible...tatizo lake sasa ni kwamba nafasi zinatolewa kwa interest za groups. Inamaana ukiondoa mtu group fulani linaweza kukosa ulaji. Ndo mana kuondoana kazini inakuwa ngumu sana hasa kama umewekwa kwa interest fulani fulani hivi

Ndahani,

Nadhani rais anayefuata itabidi aliangalie hili, watumisi wa umma ni sehemu muhimu ya maendeleo yetu. Bora wa restructure utumishi wote vyeo visivyo na mpango viondolewe. Wale wachapa kazi warudishwe na wale wachovu waondoke for good. Mbona kuna vijana wengi hawana kazi wapo wapo tu na wengine wapo kwenye private sector wachapa kazi wanaweza kuchukua hata hizo nafasi za ma principal officers na wakurugenzi.
 
Waziri kaamua kuunda tume ya kubainisha ukweli juu ya suala hili. tuombe tume iwe makini na taarifa ije ikatolewa. Tume nyingi zimekuwa zikiundwa nchi hii lakini hakuna taarifa inayowekwa wazi. Ujangili upo na utaendelea kuwepo kwa kuwa kuna soko la vipusa. Muhimu ni kweli maofisa na watumishi wamehujumu nchi? Je ni kweli ujambazi ukifanyika hata katika mabenk, askari polisi (wakuu) husimamishwa kazi?
 
Waziri kaamua kuunda tume ya kubainisha ukweli juu ya suala hili. tuombe tume iwe makini na taarifa ije ikatolewa. Tume nyingi zimekuwa zikiundwa nchi hii lakini hakuna taarifa inayowekwa wazi. Ujangili upo na utaendelea kuwepo kwa kuwa kuna soko la vipusa. Muhimu ni kweli maofisa na watumishi wamehujumu nchi? Je ni kweli ujambazi ukifanyika hata katika mabenk, askari polisi (wakuu) husimamishwa kazi?

Kihorohonjo,

Tatizo kubwa la hao waheshimiwa ni kuficha ukweli. Wamekaa kimya hadi magazeti yalipoanza ku report habari hizo na waziri mpya kuanza kuulizia ndio wakakubali kwamba Faru wamekufa. Inaonesha wizara ya maliasili chini ya Maige ilikuwa inaenda kwa utaratibu huu wa kuwaficha wananchi na kutoa tu taarifa ambao wao wanaona ni nzuri kwao.

Kujibu swali lako hata Polisi ikithibitika kama wanaficha uhalifu fulani lazima wachukuliwe hatua kama alivyosota Zombe kwa kutuambia kwamba wameua majambazi wakati ni raia wema.
 
Nimesikitishwa na taarifa za kusimamishwa kwa askari na wakurugenzi wa idara ya wanyamapori kwa sababu ya kuuawa kwa faru serengeti. Kilichonisikitisha ni kwamba alitekuwa Mratibu wa Mradi wa Faru, Nyamakumbati Mafuru alihamishwa kati ya Januari na Februari akitokea KINAPA. katika habari iliyoandikwa na NIPASHE kuhusu uharibifu katika mlima Kilimanjaro ambako yeye alikuwa MHIFADHI MKUU alimjibu mwandishi kwamba 'KILA MTANZANIA ANAWAJIBU WA KULINDA MLIMA IKIWEMO KUKAMATA WANAOPASUA MBAO' pamoja na hayo majibu ya 'kunya' aliyotoa aliishia tu kuhamishwa kutoka KILIMANJARO kwenda KINAPA. kulindana huku hakulisaidii taifa letu!!

[h=2]Uhalifu wa kutisha mlima Kilimanjaro[/h]


By Restuta James



16th January 2012





Jeuri na hujuma zinazofanywa na askari wanaolinda Mlima Kilimanjaro zinahatarisha maliasili hiyo kutokana na uhalifu mkubwa wa upasuaji wa mbao na ukataji wa miti unaofanyika ndani ya hifadhi ya msitu wa mlima huo.
Uchunguzi wa NIPASHE uliofanywa kwa wiki moja kuanzia Januari 3, mwaka huu umebaini kwamba upasuaji huo wa mbao unafanyika mchana na usiku; kilometa chache kutoka kwenye geti la askari wa Mamlaka ya Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro (Kinapa), katika kila njia rasmi zinazoingia mlimani.

Mbali ya upasuaji wa mbao, wananchi wa vijiji vya karibu wanachunga mifugo yao ndani ya hifadhi, wakiwamo ng'ombe na mbuzi ambao hula hata miti midogo inayoanza kuchipua.

NIPASHE ilishuhudia sehemu kubwa ya msitu wa hifadhi hiyo ukiwa umebaki vichaka na maeneo ya wazi badala ya miti kama ilivyokuwa imezoeleka miaka ya nyuma.

Pia NIPASHE ambayo iliingia kwenye hifadhi hiyo, ilishuhudia ukataji wa miti na upasuaji wa mbao ukifanywa nyakati hizo; na katika maeneo mengine, wahalifu hao walikimbia walipohisi kuona watu wasiowafahamu.

Baadhi ya wananchi wanaoishi katika vijiji vinavyopakana na msitu ambao walizungumza na NIPASHE walieleza kwamba wahalifu wanaovuna miti na kupasua mbao katikati ya hifadhi wanafahamika, lakini wanalindwa na askari wanaolinda hifadhi hiyo.

Mkazi wa Kijiji cha Kifuni, Kata ya Kibosho Magharibi, Wilaya ya Moshi Vijijini, ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazetini, aliliambia NIPASHE kwamba, baadhi ya watuhumiwa ni viongozi wa kijiji ambao ni marafiki wa karibu wa askari hao.

Alisema wananchi wamekuwa wakitoa taarifa za uhalifu huo kwa askari, lakini watuhumiwa hawachukuliwi hatua zozote.

Alisema hali hiyo imesababisha uharibifu mkubwa wa vyanzo vya maji na kusababisha mito mingi kukauka hivyo kuathiri shughuli za kiuchumi kijijini hapo.

Januari 3, mwaka huu, NIPASHE ilifika kwenye geti la kuingia katika mlima huo la Umbwe saa 6.00 mchana baada ya kufanya uchunguzi ndani ya hifadhi.

Ilikutana na askari wawili ambao walikanusha kuwapo uharibifu huo na kuwazuia waandishi kuingia kwenye hifadhi hadi watakapopata kibali cha Kinapa.

“Hatusemi kwamba kuna upasuaji unaofanyika. Huo ni uvumi tu, watu wanawaletea. Lakini kama mnataka kuingia msituni inabidi mpate kibali cha Kinapa na wao ndio wanaweza kusema kama kweli kuna kitu kama hicho hapa,” alisema askari aliyetambulika kama mkuu wa kituo hicho bila kutaja jina lake.

Askari huyo alimtaka mwandishi wa habari hizi awasiliane na Kinapa ama Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (Tanapa) kwa ufafanuzi zaidi.

Kutokana na hali hiyo, NIPASHE ililazimika kwenda kwa Diwani wa Kata ya Kibosho Magharibi (CCM), Claud Olomi, ambaye alithibitisha kuwapo uharibifu huo, lakini akaeleza kwamba Kinapa ilishafunga msitu huo siku nyingi.

“Wiki kama mbili hivi zilizopita Kinapa walifanya msako na kukamata mbao na mabanzi katika nyumba kadhaa katika kijiji cha jirani hapo Kiwei. Upasuaji mnaousikia unafanyika usiku na sio mchana,” alisema.

Kauli ya diwani huyo ni tofauti na hali, ambayo NIPASHE ilishuhudia kwa kuwa upasuaji ulikuwa unafanyika mchana wa siku hiyo.

Hata hivyo, alisema kumekuwa na jitihada kubwa za upandaji wa miti ndani na nje ya msitu wa hifadhi kwa lengo la kuokoa mazingira.

“Tulikuwa na mito minne na mifereji isiyo na hesabu lakini yote imekauka, mto Umbwe ambao ni mkubwa ndio umebakia na maji kidogo kabisa, hali hii ni hatari,” alisema.

Olomi alisema mbali ya uharibifu ndani ya hifadhi, katika kipindi cha nyuma wananchi walikuwa wakikata miti kwenye mashamba yao hivyo kuongeza hali ya 'jangwa'.

Pamoja na maelezo ya diwani huyo, NIPASHE ilishuhudia uchimbaji wa mchanga katika mto Umbwe hali inayochangia zaidi uharibifu wa mazingira.

Alisema katika mkakati wa upandaji wa miti, wananchi kwa kushirikiana na asasi ya kiraia ya Lepaje, imekwishapanda miti 4,000 ndani na nje ya hifadhi hiyo.

“Uchimbaji wa mchanga unaathiri sana mazingira na tunawazuia japokuwa sio moja kwa moja kwa sababu wapo wazazi wengine wanasomesha watoto wao kwa biashara hiyo,” alisema Olomi.

NIPASHE pia ilizungumza na Mhifadhi Mkuu wa Kinapa, Nyamakumbati Mafuru, kuhusiana na uharibifu huo, lakini alijibu kwa jazba kwamba: “Wewe si Mtanzania? Kama ni hivyo, basi ujue unalo jukumu la kulinda mlima Kilimanjaro.”

“Kama umeona mtu anapasua mbao si ungemkamata? au unataka tu kuichafua Kinapa? Lazima tujue kwamba hili ni jukumu letu sote. Kwanza mimi siruhusiwi kusema chochote. Mtafute Shelutete (Pascal), ambaye ni msemaji wa Tanapa, atakuwa na majibu ya kina,” alisema Mafuru.

Aliongeza: “Utaratibu ni kwamba unatakiwa kuandika maswali, uyapeleke Tanapa Arusha. Halafu kama wakikujibu sawa au wakiniambia nizungumze na wewe nitafanya hivyo. Niache kwa sasa nina majukumu makubwa ya kiofisi natakiwa kufanya...huu sio muda wa kuongea na waandishi wa habari.”

NIPASHE ilipomtafuta Shelutete na kumweleza hali hiyo, alijibu kwamba yupo likizo hivyo asingeweza kusema chochote.

Mwandishi wa habari hizi alimwomba Shelutete amwelekeze kwa mtu, ambaye angeweza kutoa ufafanuzi wa suala hilo kwa niaba yake, lakini alikataa kwa madai kwamba hakumwachia mtu yeyote nafasi yake.

Wakati wakubwa hao wa Tanapa na Kinapa wakieleza hayo, katika eneo la Uru inadaiwa kwamba ndiko hasa biashara ya mbao inafanyika, ambako mnunuzi huagiza mbao asubuhi akiwa Moshi mjini na analetewa 'mzigo' usiku ambapo pia analipia.

“Kama uko serious unataka mbao sema ni kiasi gani na uelekeze unakotaka zishukie; jioni nakuletea mzigo wako, lakini utaletewa mbao mchanganyiko yaani za miti mbalimbali,” alisema mfanyabiashara mmoja ambaye hakutaja jina lake.

Katika eneo hilo, uharibifu ni mkubwa na unafanana na vijiji vingine vinavyopakana na hifadhi hiyo.

Wilayani Hai, ambako kuna geti la Machame, ukiwa ndani ya msitu huwezi kuona tofauti ya msitu na mashamba ya kawaida ya wananchi kwa kuwa kumebakia viwanja na vichaka vidogovidogo.

NIPASHE iliingia ndani ya msitu huo kupitia kijiji cha Nkuu Ndoo, kilichopo Kitongoji cha Nkweshoo, Kata ya Machame Mashariki na kushuhudia uharibifu mkubwa, ikiwamo ng'ombe na mbuzi kupata malisho ndani ya msitu.

Mzee Sindanaeli Kileo (71), ambaye shamba lake linapakana na hifadhi ya mlima, alisema: “Miaka mitano ijayo huu msitu utakuwa umeisha. Mimi nilishapeleka hadi majina ya wanaopasua mbao kwa askari, lakini upasuaji unaendelea.”

“Miezi miwili iliyopita niliwaeleza watu wa Kinapa kuhusiana na hii hali wakaniambia nisiwaelekeze kazi kwa sababu wanalinda mlima sio msitu. Ndio maana unaona msitu unaendelea kuteketea,” alisema Mzee Kileo ambaye pia aliwahi kuwa Mwenyekiti wa Kitongoji cha Nkweshoo.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kitongoji hicho ambaye pia ni mwanaharakati wa masuala ya mazingira kijijini hapo, Twalib Mallya, alisema inasikitisha kwamba wananchi wenye mapenzi mema wanapanda miti, lakini wahalifu wachache wanakata miti na kuchunga ng'ombe kwenye hifadhi bila kuchukuliwa hatua.

“Kutoka hapa hadi hapo getini hakuna umbali wowote, lakini unaweza kuona jinsi watu wanavyopasua mbao wakati wowote tena bila wasiwasi,” alisema.

Alisema kitongoji hicho kinakusudia kutunga sheria ndogondogo ili watakapomkuta mhalifu akikata mti ndani ya hifadhi wanamkamata na kumpeleka kituo kikuu cha polisi mjini Moshi badala ya sasa wanavyomkabidhi kwa askari wa Kinapa na kuachiwa.

“Sisi hatuna imani kabisa na Kinapa kwa sababu hawachukui hatua zozote kudhibiti hali hii,” alisema.

Diwani wa Machame Mashariki (CCM), Rajab Nkya, alikiri kuwapo kwa hali hiyo na kueleza kuwa: “Nasikia tu kuna Kinapa na Tanapa. Sina hakika kama wapo. Maana sioni wanachofanya. Kwa sababu sisi wananchi wa kawaida tunaona watu wanapasua mbao, lakini Kinapa haijafanikiwa kuwaona."

Aliongeza: “Nafikiri kama msitu ungekuwa mali ya mtu binafsi miti isingekatwa mbona ndizi huku shambani haziibwi? nimeshakamata fuso mbili zikiwa zimesheheni mbao nikapeleka polisi na nyingine serikali ya kijiji lakini wahalifu wapo na Kinapa hawachukui hatua zozote."

Alisema juhudi za kupambana na uhalifu huo unakwama kwa sababu wapasuaji wakubwa wa mbao ni baadhi ya viongozi wa vijiji ambao wanalindwa na askari wa Kinapa.

Alisema hali hiyo imesababisha kukauka kwa mito Waramu, Makoa na Weruweru pamoja na mifereji yote iliyokuwa ikitumiwa na wananchi kumwagilia mashamba wakati wa kiangazi.

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Leonidas Gama, alipoulizwa kuhusiana na hali hiyo, alionyesha kusikitishwa na kuahidi kufuatilia kwa kina ili kuona namna ya kulitatua.

SOURCE: NIPASHE
 
Kweli hawa mungu wao ni pesa yaani wananuka hawafai bora haya mashirika yafutwe mali asili zikabiziwe kwa wananchi wenyewe
 
Serengeti national park wanashangaza sana, badala ya kulinda faru wao kazi yao ni kupambana na driver guides, wapi wamekanyaga majani!!!!!!!!
 
WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki ameanza kutekeleza kwa vitendo kauli yake ya kuisafisha Idara ya Wanyamapori baada ya kuwasimamisha kazi wakurugenzi wanne na askari 28 wa Hifadhi ya Taifa Serengeti, Mara ili kupisha uchunguzi wa tukio la kuuawa kwa faru wawili na kung’olewa pembe.

Faru hao ni miongoni mwa watano ambao Rais Jakaya Kikwete aliwapokea wakitokea Afrika Kusini, Mei 21, 2010 lakini Desemba 21, mwaka huo faru dume aitwaye george aliuawa na pembe zake zilinaswa Mwanza. Faru wengine wanne walipewa majina ya cleo, ethna, lunnar na dume pekee aliyebaki, benj.

Wakati akipokea faru hao waliogharimu Sh7.5 bilioni kuanzia ununuzi hadi kuwasafirisha hadi nchini, Rais Kikwete alisema: “Afrika Kusini imeongeza uwezo kwa Tanzania kwa kuleta faru hao weusi na ongezeko hilo ni la manufaa kwa taifa. Hivyo, tutaimarisha huduma zao na ulinzi utakuwa wa kipekee zaidi yangu mimi.”


Lakini tofauti na ulinzi huo alioahidi Rais, kumekuwa na taarifa za kuawa kwa faru wengine wawili hivi karibuni na mamlaka husika zikaficha tukio hilo hadi liliporipotiwa na vyombo vya habari. Takwimu zinaonyesha tangu mwishoni mwa 2009 hadi Desemba 2010, faru 15 wamekwishauawa.

Balozi Kagasheki alisema jana kwamba amechukua hatua hiyo kutokana na wakurugenzi hao kukaa kimya baada ya tukio hilo na askari hao wakidaiwa kukiuka mkataba wao wa ajira ambao unawataka watoe ulinzi kwa wanyamapori.

“Mkataba wao upo wazi kuwa wanapaswa kuwalinda wanyamapori hao na lolote linalowapata liwapate na wao pia, lakini wanyama wameuawa mwezi mzima umepita na wiki mbili baadaye gazeti linaandika ndipo Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (Tanapa), wanachukua hatua,” alisema.

Waziri Kagasheki pia alisema wahusika hao wameundiwa tume huru ambayo itafanya kazi ndani ya siku 60 na watakaobainika kuhusika kwa namna moja au nyingine, watachukuliwa hatua zaidi za kisheria na wale ambao watathibitika kuwa hawahusiki taratibu nyingine zitafuatwa.

Aliwataja wakurugenzi ambao wamesimamisha kazi kuwa ni Kaimu Mkurugenzi wa Uhifadhi, Justine Hando, Mkurugenzi wa Intelejensia katika Wizara hiyo, Emmly Kisamo, Mkurugenzi wa Hifadhi ya Serengeti, Mtango Mtahiko na Mkurugenzi Mratibu wa Mradi wa faru, Mafuru Nyamalumbati.

Alisema anachukua hatua hizo ambazo ni tofauti na utaratibu wa kawaida kutokana na kukithiri kwa vitendo vya ovyo ambavyo vinaichafua wizara yake.

“Kwanza niliwauliza baada ya kupatikana kwa habari za kuuawa kwa faru hao walichukua hatua gani? Jibu likawa tumewapa siku 14 wajieleze,” alisema Kagasheki na kuongeza kuwa watendaji hao wakamwambia kuwa maelezo hayo yasiporidhisha hatua itakayofuata ni kuundwa tume.

Kagasheki alifafanua kwamba alipohoji muda wa utendaji wa tume hiyo, aliambiwa ni siku 60 jambo ambalo alilikataa na kuchukua uamuzi wa kuwasimamisha ili kupisha uchunguzi huo na kudai kuwa watendaji hao kama wangeachwa wangeweza kuwa na athari zaidi kwa hifadhi na wanyamapori.

Alisema wizara yake haiwezi kufanya kazi kwa woga na kusema yupo vitani akiahidi kupambana kuondoa uozo unaodaiwa kuigubika.

Alisema anajua kuwa kuna mtandao wa ujangili ndani na nje ya nchi ambao una fedha nyingi lakini akasema hatarudi nyuma... “Faru ni moja kati ya viumbe hai ambavyo vipo hatarini kutoweka hivyo kilichotokea hakivumiliki.”

Alisema kuwa mara baada ya kuandikwa kwa habari hizo, walikwenda hadi eneo la tukio na kukuta miili ya wanyama hao wakiwa wameondolewa pembe zao na jirani kukiwa na maganda ya risasi... “Tumewakuta mama na mwanaye wameuawa na pembe zao kuondolewa. Inasikitisha sana.”

Mei 21 akizungumza Dar es Salaam katika uzinduzi wa Bodi ya Ushauri ya Wizara ya Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Balozi Kagasheki alionya kwamba angeifumua Idara hiyo ya Wanyamapori huku akipiga marufuku usafirishaji wanyama hai nje ya nchi.

Alisema kama idara hiyo itasimamiwa vizuri kukusanya mapato, inaweza kusaidia kupunguza matatizo ya wananchi.

Mwananchi

Source: Joseph Zablon, Gazeti la Mwananchi

VIJIMAMBO: Faru wa JK wang'oa vigogo maliasili
 
serengeti national park wanashangaza sana, badala ya kulinda faru wao kazi yao ni kupambana na driver guides, wapi wamekanyaga majani!!!!!!!!

kwa hiyo ndugu unataka serengeti wakuachie uharibu mazingira?
 
Mkuu Maundumula sasa hao wanaoitwa game wakukamate na kakitoweo ka swala tu ndugu yangu umeisha! Kuna watu wamekula nyama ya swala ikiwa mbichi. Lakini kwa majangiri ati hawaonekani! Hawa TANAPA wana vifaa vya kisasa vya monitoring na hata ndge za patrol wanazo lakini Faru wanauawa.

Mkuu, umeleta ponti muhimu sana.
Uuaji wa tembo na faru kwa ajili ya vipusa ni coordinated crime, inashirikisha watu wengi sana. Tukitaka tutatua kadhia hiyo inabidi tuanzie mbali sana, sio kwenye hifadhi tu. Kama tuna ndege, vionambali, fensi zenye umeme ili kulinda faru, inakuwaje majangiri wanafika kadi walipo faru ambapo pana walinzi 24/7?
 
pembe za faru ni dawa ya kurudisha heshima ya ndoa hasahasa wazee.
 
Back
Top Bottom