Faru wa JK wang’oa vigogo maliasili | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Faru wa JK wang’oa vigogo maliasili

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by nngu007, May 30, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  May 30, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading"][/TD]
  [TD="class: buttonheading, align: right"][/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"]Tuesday, 29 May 2012 21:17[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]

  Joseph Zablon

  WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki ameanza kutekeleza kwa vitendo kauli yake ya kuisafisha Idara ya Wanyamapori baada ya kuwasimamisha kazi wakurugenzi wanne na askari 28 wa Hifadhi ya Taifa Serengeti, Mara ili kupisha uchunguzi wa tukio la kuuawa kwa faru wawili na kung'olewa pembe.


  Faru hao ni miongoni mwa watano ambao Rais Jakaya Kikwete aliwapokea wakitokea Afrika Kusini, Mei 21, 2010 lakini Desemba 21, mwaka huo faru dume aitwaye george aliuawa na pembe zake zilinaswa Mwanza. Faru wengine wanne walipewa majina ya cleo, ethna, lunnar na dume pekee aliyebaki, benj.


  Wakati akipokea faru hao waliogharimu Sh7.5 bilioni kuanzia ununuzi hadi kuwasafirisha hadi nchini, Rais Kikwete alisema: "Afrika Kusini imeongeza uwezo kwa Tanzania kwa kuleta faru hao weusi na ongezeko hilo ni la manufaa kwa taifa. Hivyo, tutaimarisha huduma zao na ulinzi utakuwa wa kipekee zaidi yangu mimi."


  Lakini tofauti na ulinzi huo alioahidi Rais, kumekuwa na taarifa za kuawa kwa faru wengine wawili hivi karibuni na mamlaka husika zikaficha tukio hilo hadi liliporipotiwa na vyombo vya habari. Takwimu zinaonyesha tangu mwishoni mwa 2009 hadi Desemba 2010, faru 15 wamekwishauawa.


  Balozi Kagasheki alisema jana kwamba amechukua hatua hiyo kutokana na wakurugenzi hao kukaa kimya baada ya tukio hilo na askari hao wakidaiwa kukiuka mkataba wao wa ajira ambao unawataka watoe ulinzi kwa wanyamapori.


  "Mkataba wao upo wazi kuwa wanapaswa kuwalinda wanyamapori hao na lolote linalowapata liwapate na wao pia, lakini wanyama wameuawa mwezi mzima umepita na wiki mbili baadaye gazeti linaandika ndipo Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (Tanapa), wanachukua hatua," alisema.


  Waziri Kagasheki pia alisema wahusika hao wameundiwa tume huru ambayo itafanya kazi ndani ya siku 60 na watakaobainika kuhusika kwa namna moja au nyingine, watachukuliwa hatua zaidi za kisheria na wale ambao watathibitika kuwa hawahusiki taratibu nyingine zitafuatwa.


  Aliwataja wakurugenzi ambao wamesimamisha kazi kuwa ni Kaimu Mkurugenzi wa Uhifadhi, Justine Hando, Mkurugenzi wa Intelejensia katika Wizara hiyo, Emmly Kisamo, Mkurugenzi wa Hifadhi ya Serengeti, Mtango Mtahiko na Mkurugenzi Mratibu wa Mradi wa faru, Mafuru Nyamalumbati.


  Alisema anachukua hatua hizo ambazo ni tofauti na utaratibu wa kawaida kutokana na kukithiri kwa vitendo vya ovyo ambavyo vinaichafua wizara yake.


  "Kwanza niliwauliza baada ya kupatikana kwa habari za kuuawa kwa faru hao walichukua hatua gani? Jibu likawa tumewapa siku 14 wajieleze," alisema Kagasheki na kuongeza kuwa watendaji hao wakamwambia kuwa maelezo hayo yasiporidhisha hatua itakayofuata ni kuundwa tume.


  Kagasheki alifafanua kwamba alipohoji muda wa utendaji wa tume hiyo, aliambiwa ni siku 60 jambo ambalo alilikataa na kuchukua uamuzi wa kuwasimamisha ili kupisha uchunguzi huo na kudai kuwa watendaji hao kama wangeachwa wangeweza kuwa na athari zaidi kwa hifadhi na wanyamapori.


  Alisema wizara yake haiwezi kufanya kazi kwa woga na kusema yupo vitani akiahidi kupambana kuondoa uozo unaodaiwa kuigubika.


  Alisema anajua kuwa kuna mtandao wa ujangili ndani na nje ya nchi ambao una fedha nyingi lakini akasema hatarudi nyuma... "Faru ni moja kati ya viumbe hai ambavyo vipo hatarini kutoweka hivyo kilichotokea hakivumiliki."


  Alisema kuwa mara baada ya kuandikwa kwa habari hizo, walikwenda hadi eneo la tukio na kukuta miili ya wanyama hao wakiwa wameondolewa pembe zao na jirani kukiwa na maganda ya risasi... "Tumewakuta mama na mwanaye wameuawa na pembe zao kuondolewa. Inasikitisha sana."


  Mei 21 akizungumza Dar es Salaam katika uzinduzi wa Bodi ya Ushauri ya Wizara ya Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Balozi Kagasheki alionya kwamba angeifumua Idara hiyo ya Wanyamapori huku akipiga marufuku usafirishaji wanyama hai nje ya nchi.


  Alisema kama idara hiyo itasimamiwa vizuri kukusanya mapato, inaweza kusaidia kupunguza matatizo ya wananchi.
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  May 30, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Kagasheki ni Mchapa Kazi, Wakati akiwa Naibu Mambo ya Ndani na Waziri ni Lau; yeye ndiye aliyekuwa anafanya kazi zote

  Lau ni Makelele na kupenda kupigiwa Saluti
   
 3. Sniper

  Sniper JF-Expert Member

  #3
  May 30, 2012
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,944
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Huko TANAPA kumeoza, kuna watu wanajionaga ni ma mungu mtu huko
   
 4. Mkubwa ndevu

  Mkubwa ndevu JF-Expert Member

  #4
  May 30, 2012
  Joined: Feb 17, 2011
  Messages: 755
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 45
  Comment removed by mods
   
 5. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #5
  May 30, 2012
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  sina imani sana na Kagasheki.....ni upepo tu unapita ...
   
 6. Maarko

  Maarko JF-Expert Member

  #6
  May 30, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 1,030
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  Tatizo la maliasili ni kupeana kazi kwa kufahamiana waajiriwa huku ni ndugu/marafiki wa viongozi wakubwa serikali ambao hawana weledi.Lazima muheshimiwa Kagasheki ajue vita alivyovianzisha ni vikubwa maadui wengi wapo humohmo serikali na ni viongozi wenzake wakubwa.
   
 7. K

  KISAKA MORIS JF-Expert Member

  #7
  May 30, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 372
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mwache awang'oe maana hata yeye hatasalia maana muda si mrefu ataanza kuzitafuna.
   
 8. B

  Baba Wilbur Member

  #8
  May 30, 2012
  Joined: Jun 6, 2011
  Messages: 7
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  xxxxxxxxxxxxxx
   
 9. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #9
  May 30, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Mkuu Waziri amewasimamisha ili uchunguzi ufanyike siyo kwamba amewafuta kazi.

  Lakini pia suala la kushindwa kwenye medani na ku retreat kidogo hapo hauko sawa. Una retreat baada ya kupambana na katika mapambano kuna ushahidi wa kupoteza risasi na maisha siyo una retreat tu basi tunaamini kwamba umezidiwa nguvu. Ingekuwa hivyo wanajeshi wasingekuwa wanaenda mstari wa mbele.

  Hao wa Serengeti ni wapi wameonyesha kwamba walipambana na hao majangili na kuzidiwa nguvu. Najua unataka kusema kwamba majangili wana uwezo wa kuingia bila kuonekana na kuua hao wanyama. Lakini pia hii inatia shaka tena inatia aibu kwa kuwa mimi binafsi nilimsikia Rais akisema wale Faru waliotoka RSA watapewa ulinzi kuzidi hata ulinzi anaopewa yeye! Wanapouwawa na majangiri bila hao majangiri kukamatwa inatoa ujumbe gani?
   
 10. Ndekirhepva

  Ndekirhepva JF-Expert Member

  #10
  May 30, 2012
  Joined: May 18, 2012
  Messages: 377
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  mimi huyu waziri sina imani na mchakato alioanza kuuchukua kwa vile, kama ilivyo desturi, kamati itaundwa na itafanya uchunguzi na majibu yatapatikana, sema sasa issue inakuja nani wakumfunga paka kengele??????
  tuliona akina ngeleja, ngeleja hakuanza kupingwa kwenye hili bunge la juzi, alipingwa tokea bunge la february, lakini kwa shinikizo ndio bosi wake amempumzisha ila jamaa anaendelea kula bata mtaani, so mi naona ni mbwembwe tu, kwani Kagasheki hajui kwamba huo mradi ni wawatu wakubwa????
  JK atakua anahusika sana tu,haiwezekani faru wameuawa alafu hakuna taarifa iliyowafikia watu
   
 11. Kibanga Ampiga Mkoloni

  Kibanga Ampiga Mkoloni JF-Expert Member

  #11
  May 30, 2012
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 14,565
  Likes Received: 1,654
  Trophy Points: 280
  Mzushi tu huyu nakumbuka alienda kule MGODINI akakuta maji yenye sumu na ALILIA KUPITA PINDA, Lakini wapi hakuna alichofanya.
   
 12. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #12
  May 30, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  TANAPA ni majangiri yani sawa na fisi kumkabidhi bucha.
   
 13. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #13
  May 30, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Hii inasikitisha sana, juzi juzi tulisikia mtu wa usalama na mtu wa serikali wamekamatwa wakinyemelea nyara za serikali. Hatujakaa vizuri faru wa JK nao wameuwawa wote na sisi hatujapata taarifa.

  Kumbe walikuwa wanasubiri JK aondoke eneo la tukio na ulinzi ukome hapo hapo! kweli hii nchi ni ya vilaza wa hali ya juu. Angalau kutupa information ya yaliyotokea hamna!. Sasa watatu convince vipi kama wao hawahusiki na mtandao huu wa ujangili hao vigogo wa TANAPA ? Si nilisikia hawa FARU waliwekewa vifaa maalum vya ku monitor popote pale walipo wanajulikana? kwanini wahusika hao wa usalama wa wanyama pori hawakuwa wanafuatilia nyendo zao? Sasa itabidi tutote tena another 7.5 Billion tununue FARU wengine kutoka SA!!!!
   
 14. omujubi

  omujubi JF-Expert Member

  #14
  May 30, 2012
  Joined: Dec 6, 2011
  Messages: 4,144
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  kwenye red hapo ndilo tatizo la Watanzania sote, ni wachache kati yetu wanaoelewa madhara ya uharibifu wa urithi tulionao. Wenzetu Kenya wana matatizo kama haya lakini uelewa wa wananchi wa kawaida ni mkubwa kidogo katika kuhifadhi maliasili.

  Nenda Mikumi tu hapa mida ya saa mbili jioni uone jinsi nyama za swala, nyati, pofu nk zinavyouzwa hata kwa wapita njia na unaona wazi kuwa maaskari wanajua na wanapata mgao lakini ile sense kuwa wanyama wanaweza kutoweka haiko kabisa akilini mwao!
   
 15. p

  posa Member

  #15
  May 30, 2012
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 74
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 25
  Kama kadhamiria yeye mwenyewe ndio wa kumvika paka kengere. Tulimsikia Chami kuhusu suala la Mkurugenzi wa TBS, waziri anaweka visingizio kibao, mara hana uwezo wa kumsimamisha mpaka rais, mara ripoti haijafika kwangu, etc, mbona mwenzake hatukusia hayo ya rais aamue, mara alipoingia akachukua hatua.


  Kwa hiyo pia kama Kagasheki kadhamiria anatakiwa kuona mwisho wa jambo hili. Hasa tukinukuu maneno yake alipokuwa anaingia wizarai kwamba hatokuwa tayari kunyongwa yeye kabla hajamjonga mhusika.
   
 16. p

  posa Member

  #16
  May 30, 2012
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 74
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 25
  Kama kadhamiria yeye mwenyewe ndio wa kumvika paka kengere. Tulimsikia Chami kuhusu suala la Mkurugenzi wa TBS, waziri anaweka visingizio kibao, mara hana uwezo wa kumsimamisha mpaka rais, mara ripoti haijafika kwangu, etc, mbona mwenzake hatukusia hayo ya rais aamue, mara alipoingia akachukua hatua.


  Kwa hiyo pia kama Kagasheki kadhamiria anatakiwa kuona mwisho wa jambo hili. Hasa tukinukuu maneno yake alipokuwa anaingia wizarai kwamba hatokuwa tayari kunyongwa yeye kabla hajamjonga mhusika.

  Na huo ndio utendaji tunaousbiri kwa muda mrefu, jambo linatokea hatua zinachukuliwa hapo hapo, sio visingizio kibao, mara haki za binadamu, mara tutashitakiwa, etc
   
 17. Olaigwanani lang

  Olaigwanani lang JF-Expert Member

  #17
  May 30, 2012
  Joined: Apr 26, 2012
  Messages: 480
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  ..MARA YA KWANZANZA KABISA WALIPOLETWA WATAALAM WA UHUFADHI WALIOMBWA WAPENDEKEZE NI WAPI WAWEKWE...WALIPENDEKEZA KATIKATI YA HIFADHI KWANI ITAKUWA NI VIGUMU KWA MAJANGILI KUPENYA NA KUHATARISHA MAISHA YAO..LAKINI SEREIKALI YETU ILIVO YA KINAFIKI..IKAWAPELEKA KULEE GURUMETI AMBAPO NI SEHEMU KARIBU NA VIJIJI VINGI VINAVYOZUNGUKA HIFADHI NA MIMI KAMA MHIFADHI WA ULINZI NINAJUA VIJIJI HIVO NI VIJIJI VYA MAJANGILI, CHAKUSHANGAZA NI KUWA SIJUI SERIKALI ILIKUWA INAOMBA USHAURI WA NINI MWANZONI WAKATI HAWATAKI KUFATA MAELEKEZO YA WAHIFADHI,NA HILI TUMEGUNDUA WANAPUUZA USHAURI HUKU WAKIFATA MASILAHI (INTEREST) ZA WALE MABWANA WENYE MAHOTELI MAARUFU YA KIFAHARI KULE GURUMETI..,ILI WAWAFANYIE BIASHARA ZAO KWA WATALII WAO...,KAMA MNAKUMBUKA SERIKALI ILIPUUZA USHAURI WA WATAALAM KUHUSU UJENZI WA SOPA LODGE TARANGIRE,SOPA LODGE NGORONGORO KWENYE UKUTA WA KRETA...HAYA MAMBO YAMEKUWA YAKIJITOKEZA SASA NA MADHARA YAKE NDO TUNAYAONA SASA..... HIVO MNATAKIWA MJUE KUWA SERIKALI HII HAIKO RADHI KUFATA USHAURI WA WASOMI WAKE..AMABAO WENGI WAO ILIWASOMESHA WAO ILI WAISAIDIE NCHI YAO LAKINI NDO HALI HALISI SASA ILIVO..... MWISHO WA YOTE NATAKA NITAHADHARISHE KUWA ITAKUJA KUBAKI HISTORIA TUU KWA WANYAMA WETU KWAMBA WALIKUWEPO.. (KWA KWELI SIASA NA UHIFADHI NI KAMA NYOTA NA BAHARI)kagasheki atakiwa ajue kuwa kuna hayo na ndoo aanze huko......badala ya chini
   
 18. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #18
  May 30, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Mkuu Maundumula sasa hao wanaoitwa game wakukamate na kakitoweo ka swala tu ndugu yangu umeisha! Kuna watu wamekula nyama ya swala ikiwa mbichi. Lakini kwa majangiri ati hawaonekani! Hawa TANAPA wana vifaa vya kisasa vya monitoring na hata ndge za patrol wanazo lakini Faru wanauawa.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 19. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #19
  May 30, 2012
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 720
  Trophy Points: 280
  huyu kagashek ni mtu hatari sana.....ni mla rushwa mkubwa na jizi lilokubuhu...hapo anataka kuinstall watu wake ili waanze kuiba sawa sawa
   
 20. A

  Aswel Senior Member

  #20
  May 30, 2012
  Joined: May 1, 2012
  Messages: 114
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Safi sana wazembe lazima wawajibishwe, lakini tunaomba isiwe nguvu ya soda.
   
Loading...