Faru na Binadamu kipi bora Tanzania?

Oct 5, 2015
88
476
Serikali ya ovyo ipo bize kujadili, kujisemeza, kujinajisi na mambo ya kijangili ya Faru John kuliko maiti za watu 6 zilizokutwa zimetupwa bonde la mto Ruvu.

Waziri mkuu ameguswa sana na kutoweka kwa Faru John, na kutoa maagizo ya kimamlaka. Lakini haoni sababu yoyote ya kuzungumzia uhaia wa watanzania ulioporwa na watu wasiojulikana. Kwani mtanzania ana thamani gani zaidi ya Faru?

Ndipo unapojua, kumbe katika Tanzania unaweza kufanyiwa unyama wowote watu wakaendele na shughuli zao. Unaweza kuuawa na kutupwa mtoni ili uliwe na mamba. Na hata mkono wa malaika ukikushukia ili angalau upewe heshima zako za kuwahi kuwa binadamu, bado wenye mamlaka watahakikisha unafukiwa haraka kama mzoga ili usiwaachie harufu kali ya uozo wako.
[HASHTAG]#Tanzania[/HASHTAG]
 
Back
Top Bottom