Faru John ni TEST na kipimo tosha cha uwezo wa Serikali ya sasa kupambana na Rushwa na Ufisadi

Francis12

JF-Expert Member
Sep 30, 2016
7,533
22,276
Anaandika Comred Julias Mtatiro.
DRAMMA YA JOHN....

Pembe ya Faru husagwa na kutoa unga wenye thamani kubwa sana. Kilo moja ya unga huo huuzwa Dola za Marekani 68,000 (Tshs Milioni 148) na huko Vietnam kilo moja huuzwa kwa Dola za Marekani 100,000 (Tshs Milioni 220).


Faru John ambaye tunamsaka alikuwa na Pembe yenye uzito wa Kilo 7. Yaani waliomuua na kuchukua hiyo pembe, kama wameiuza hapa Tanzania wamevuna Dola 490,000 sawa na Tshs Bilioni 1.1 (Bilioni 1 na Milioni 100). Kama wameiuza Vietnam wamevuna dola 700,000 sawa na Tshs Bilioni 1.54 (Bilioni 1 na Milioni 540).

Nimekerwa sana kusikia Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro ilimuuza kwa hoteli ya Grumeti kwa Tshs Milioni 200. Jamaa waliouziwa wamepata faida ya Bilioni 1.34 (Bilioni 1 Milioni 340) chap chap.

Kinachofurahisha hapa Afrika ni kuwa, [HASHTAG]#Serikali[/HASHTAG] zetu zinawajua waliopiga hizo hela, inawajua kuliko hata maafisa wa Hifadhi ya Ngorongoro wanavyowajua. Kwa kawaida biashara haramu na kubwa kama hizo, za kupata faida ya bilioni 1 kufumba na kufumbia, hufanywa kwa "connection" kubwa ya watu walioko madarakani; Ikulu, Wizara mtambuka na Vyombo vya Ulinzi na Usalama.

Dramma ya John itakapoisha tutapiga makofi kuona maafisa waliomuuza kwa Mil. 200 wakitolewa kafara kwa kufikishwa mahakamani na hata kufungwa. Wale wakubwa "waliopiga" bilioni 1 na milioni 300 (faida ya kumuuza John wetu) hatutasikia wakitajwa popote. Haya yatatokea kweupe mchana, na JPM atayaona kwa macho yake na hatakuwa na cha kufanya!

John ni TEST na kipimo tosha cha uwezo wa Serikali ya sasa kupambana na Rushwa na Ufisadi. Ngoja tusubiri, tuone mwisho wake.
[HASHTAG]#JSM[/HASHTAG].
FB_IMG_1481287613905.jpg
 
Wenzetu South Africa wanawakata faru pembe ili kuwaepusha na majangili.......sijui serikali huwa inazipeleka wap pembe hizo baada ya kuzikata.

Inasemekana kuwa pembe za faru zinauwezo wa kuota pndi zinaokatwa kama ziivyo kucha za binadamu
 
Uzi huu wale wa buku mbili kama hawauoni vile... ukiona wamenyuti jua kuna ukweli.
 
Hii ni nyuma ya pazia lililo toa milolongo ya mabilionea utitiri bongo na madaraja mapana kt ya umaskini na utajiri wakati sisi ni mixid economy (centrolised + capital) doo hichi kipimo
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom